Msaada juu ya tatizo la liver shrinking (cirrhosis)

Msukule Msafi

Member
Oct 10, 2018
55
45
Habari wakuu naomba kujuzwa hili tatizo linatibika au ni namna gani linaweza kua solved
Historia fupi :

Mwenye tatizo hili ni dada yangu ameanza kuumwa tu bile kujua tatizo tangu mwaka 2019 mwanzoni kabisa alikua na tendemcy ya kuvimba vimba sehemu mbalimbali za mwili mara miguu,uso,mikono na hata tumbo pia anavimba vimba tukaenda hospital ya mloganzila akafanyiwa vipimo awali walisema tatizo lipo kwenye figo (Nephrology) akaanza clinic pale ila hali ilikua ni ile ile kila mwezi yeye ni wa kulazwa tu hospital kwa kutokana na kuvimba vimba na kushindwa kupumua halikusaidia lolote zaidi ya wakawa wanamyoa maji tu kisha anapata nafuu tunarudi ila mwisho wa siku baada ya muda hali inarudi tukamuhuamishia muhimbili pale wakaanza upya vipimo nao wakaja na majibu yao kuwa ana NEPHROTIC SYDROME na kusema tatizo lipo mwenye figo hii ilikua ni mwaka 2020 kikubwa nao wakamwanzishia clinic ya figo huku akiwa na tatzo lile lile la kuvimba na kujaa tumbo na miguu wanachofanya ni kumtoa maji tu

Kila mwezi ni wa hospital mwaka huu mwanzoni watu wa clinic ya figo wakasema kua hana matatizo kabisaaa kwenye figo na figo zake zipo safi kabisa wakapima tena vipimo na wakasema ana tatizo la ini kusinyaa (cirrhosis) sasa wakaanza clinic nao ila majibu ndo hayaeleweki na wamempa miezi 3 akaenyumbani ndo aje clinic hiyo ilikuwa mwezi wa January mwaka 2021 mpka nazungumza sasa ameshaenda kutolewa maji na kulazwa muhimbili mara 4 hadi sasa .

Naomba msaada wa kujuzwa vyema hili jambo wapi naweza saidia nimeambatanisha na baadhi ya dawa na majibu ya vipimo NAWASILISHA

20210122_203925.jpg
20210122_203925~2.jpg
20210122_203953.jpg
 
Tanzania kuna changamoto kubwa sana ya madaktari,na ninaamin kuna watu wengi sana hufariki si kwa sababu ya kutokumwona daktari bali ni kukutana na daktari ambaye si sahihi ambaye huwapa tiba ambayo si sahihi-Binafsi naona changamoto kubwa inaanzia kwenye right diagnosis ya ugonjwa,unaweza fika hospitali doctor anakusikiliza for a second alafu anakukatisha na kuanza kukuandikia mavipimo na dawa wakati the full history ya mgonjwa hajaisikiliza.

Be patient, Jaribu kufanya utafiti wako binafsi wa Ma specialist wa kihindi either Regency au Hindu mandal wanaohusika na hzo issues,sema changamoto za hao madaktari ni kwamba appointment zao unaweza kukuta ni 4 -6 months mbele hvyo subira huhitajika,Kuna mama alienda hindu mandal wakamwekea appointment ya mwezi 5 kwa huyo super specialist hindu mandal nitajitahd kumjua jina ili niweze kukupatia kama utakuwa interested.
 
Tanzania kuna changamoto kubwa sana ya madaktari,na ninaamin kuna watu wengi sana hufariki si kwa sababu ya kutokumwona daktari bali ni kukutana na daktari ambaye si sahihi ambaye huwapa tiba ambayo si sahihi-Binafsi naona changamoto kubwa inaanzia kwenye right diagnosis ya ugonjwa,unaweza fika hospitali doctor anakusikiliza for a second alafu anakukatisha na kuanza kukuandikia mavipimo na dawa wakati the full history ya mgonjwa hajaisikiliza.....
Nitashukuru mkuu katika hili
 
Nitashukuru mkuu katika hili
For the time being-Epukeni madawa ya kienyeji kwa kadri muwezavyo na matumiz ya paracetamol bila ushauri wa Daktari.
*Madawa ya kienyeji yamewapelekea watu wengi kupata complications za Ini na figo au kuongeza ukubwa wa tatizo-Zingatia sana hili utanikumbuka.
 
Linatibika kwa sababu liver ndo organ pekee inayo regenerate yeyewe. Aache pombe kama anakunywa, apunguze sukari, na ingia google, fanya research. Hiyo Ascites ni fluids zinazojaa tumboni. Ingia soma, usiogope.

Kuna liver transplants yote yakishindikana. Anakatwa mtu mwenye ini zima, kipande kidogo tu na anapandikizwa mgonjwa. Aliyetoa kipande ini lake linaota pale palipopunguzwa na kurudi kuwa zima, na huyu aliyepandikizwa ka kipande, kale kakipande kanaota mpaka kanakuwa ini kamili.

Ushauri pia wa bure, dawa yeyote unayopewa na daktari kabla hajaitumia, ingia google ichambue ujue inavyofanya kazi, athari zake na inareact vipi pamoja na dawa zingine anazotumia tayari.
Tusipende kuamini madaktari wetu hawa, wanaopitia shule za kukariri ili wafaulu mitihani.
 
Pole sana kwa kuuguza.

Baadhi ya Madkatari wa kibongo ni hatari ,hata yule Dada Hawa Nitarejea bongo walimwambia anaumwa ini ila alivyoenda india kumbe tatizo la moyo.

Hospital inatakiwa kuwe na maspeshelist ambao ndio wanatakiwa wawaattend wagonjwa wenye matatizo makubwa na sio hawa waliokuwa field au freshers!!
 
Pole sana mkuu,
Mwanangu alianzwa na tatizo hilo nikaleta Uzi humu jf,alitolew maji na akaambiwa ana liver cirrhosis, vipimo tulifanya Aghakan Arusha nikapanga kwenda Nairobi Aghakan hawakupokea simu nikaghairi.

Tuliambiwa INI limesinyaa pale FAME arusha.kabla ya hapo alipewa vidonge vya mwezi mzima vya vidonda vya tumbo hapo hapo FAME.Tulihamia Rabininsia akaanziwa vipimo upya,wakagundua ana Cancer(lymphoma).

Ushauri mpeleke dada yetu Rabininsia memorial hospital akamuone Dr Primus Saidia ni Oncologist anaweza kumsaidia.Ni expensive kidogo vipimo na kumuona specialist kama huyo ni Tsh 30,000.Bima wanapokea usijali,kama sio Dada Josephine kwingine.

ningekwama,namshukuru na kumuombea kila Mara Mungu amfanyie wepesi katika mambo yake. Dada Josephine asante kwa msaada.
Kuna mdau amesema ma Dr ni changsmoto kufanya wrong diagnosis simpingi ni kweli ila wakati mwingine wrong diagnosis inapatikana kutokana na maelezo mabaya ya sisi wagonjwa.

Wagonjwa wengi hatujui kujieleza,tunawaogopa ma Dr.Unaweza kwenda na shida Dr akawa anakuzunguusha una umwa na hapa,je hapa je kule,mwisho pale pa mwanzo akirudi unakataa hapaumi.Wagonjwa tubadilike tuwe wawazi kwa Ma Dr tuondoe aibu na uoga.Kila LA kheri na Dada na MPE pole zangu za dhat.

Niliwahi kufuatilia liver transplant, mwaka 2018/2019 sikumbuki mwaka excactly,the cheapest was l think between U.S $ 30,000-45000 in India hapo hujainclude vitu kibao hiyo ni hospital charges tu.
 
Pole sana mkuu,
Mwanangu alianzwa na tatizo hilo nikaleta Uzi humu jf,alitolew maji na akaambiwa ana liver cirrhosis, vipimo tulifanya Aghakan Arusha nikapanga kwenda Nairobi Aghakan hawakupokea simu nikaghairi...
1-Mkuu huko kuambiwa ni tatizo la INI wakati mtoto anachangamoto ya Cancer hiyo tayari ni wrong diagnosis ninayoisemea.
2-Kupewa dawa za vidonda vya tumbo wakati inahitajika treatment ya cancer hyo ndo wrong prescriptions ninayoizungumzia.
3-Hivyo vyote hupelekea ugonjwa kukua na kuwa complicated na kupelekea kifo as i said.
 
Tatizio LA INI alikuwa ni kweli analo lilikwluwa limesinyaa.kitu kingine mkuu madaktar wana stress nadhani maana pia wanaujuaji mwingi.Nakumbuka nilikazania mtoto atizamwe appendix ndipo wakagundua maji tumboni.
Kingine umaskini wetu unachangia hayo yote
 
  • Thanks
Reactions: Ilu
Tanzania kuna changamoto kubwa sana ya madaktari,na ninaamin kuna watu wengi sana hufariki si kwa sababu ya kutokumwona daktari bali ni kukutana na daktari ambaye si sahihi ambaye huwapa tiba ambayo si sahihi-Binafsi naona changamoto kubwa inaanzia kwenye right diagnosis ya ugonjwa,unaweza fika hospitali doctor anakusikiliza for a second alafu anakukatisha na kuanza kukuandikia mavipimo na dawa wakati the full history ya mgonjwa hajaisikiliza.

Be patient, Jaribu kufanya utafiti wako binafsi wa Ma specialist wa kihindi either Regency au Hindu mandal wanaohusika na hzo issues,sema changamoto za hao madaktari ni kwamba appointment zao unaweza kukuta ni 4 -6 months mbele hvyo subira huhitajika,Kuna mama alienda hindu mandal wakamwekea appointment ya mwezi 5 kwa huyo super specialist hindu mandal nitajitahd kumjua jina ili niweze kukupatia kama utakuwa interested.
Tatizo ni pale daktari ankutana na case complicated halafu anataka kila kitu amalize yeye bila ku involve multispecialization kuita usaidizi Kwa mwingine.
 
Tatizio LA INI alikuwa ni kweli analo lilikwluwa limesinyaa.kitu kingine mkuu madaktar wana stress nadhani maana pia wanaujuaji mwingi.Nakumbuka nilikazania mtoto atizamwe appendix ndipo wakagundua maji tumboni.
Kingine umaskini wetu unachangia hayo yote
Mtoto kupitia changamoto hz inauma sana-Kama mzazi pole sana.
Binafsi nilikuwa naumwa sana Acid reflux bila kujua,kwenda hospital daktari akaniandikia madawa ya koo ambayo kumbe side effect ya hzo dawa ni kupelekea ubaya wa tatizo langu.Tatizo lilipokuwa linazid kuwa baya zaid nikahamia hospitali nyingine ambapo Dr. akaniambia ni H pylori tumboni anasababisha,nikaamia kwenye hospitali nyingine kuthibitisha ndo nikakutana na Dr.Primus naye akaniambia ni H pylori,hapo at least confidence ikaja.
Kwa Tanzania,Referral hospital nzuri naona ni KCMC, Muhimbili mizunguko mingi sana.
 
Tatizo ni pale daktari ankutana na case complicated halafu anataka kila kitu amalize yeye bila ku involve multispecialization kuita usaidizi Kwa mwingine.
Upo sahihi sana- Doctor siyo lazima ajue kila kitu kikubwa ahusishe wenzie na awe muwazi.Lakini nilichokiona madaktari wa kizungu na kihindi wako honest sana,hili nalisema kama mtu niliyewah kuumwa.

Mdogo wangu alikuwa anaumwa jicho,kufika KCMC akakutana na daktari wa kizungu,yule mzungu alichomwambia ni kwamba hawana ujuzi wa kumtibu ugonjwa huo kwa sasa na kwamba atachukua sample ya huo ugonjwa na kuwashirikisha wenzake Marekani ili kupata solution.
 
Habari wakuu naomba kujuzwa hili tatizo linatibika au ni namna gani linaweza kua solved
Historia fupi :

Mwenye tatizo hili ni dada yangu ameanza kuumwa tu bile kujua tatizo tangu mwaka 2019 mwanzoni kabisa alikua na tendemcy ya kuvimba vimba sehemu mbalimbali za mwili mara miguu,uso,mikono na hata tumbo pia anavimba vimba tukaenda hospital ya mloganzila akafanyiwa vipimo awali walisema tatizo lipo kwenye figo (Nephrology) akaanza clinic pale ila hali ilikua ni ile ile kila mwezi yeye ni wa kulazwa tu hospital kwa kutokana na kuvimba vimba na kushindwa kupumua halikusaidia lolote zaidi ya wakawa wanamyoa maji tu kisha anapata nafuu tunarudi ila mwisho wa siku baada ya muda hali inarudi tukamuhuamishia muhimbili pale wakaanza upya vipimo nao wakaja na majibu yao kuwa ana NEPHROTIC SYDROME na kusema tatizo lipo mwenye figo hii ilikua ni mwaka 2020 kikubwa nao wakamwanzishia clinic ya figo huku akiwa na tatzo lile lile la kuvimba na kujaa tumbo na miguu wanachofanya ni kumtoa maji tu

Kila mwezi ni wa hospital mwaka huu mwanzoni watu wa clinic ya figo wakasema kua hana matatizo kabisaaa kwenye figo na figo zake zipo safi kabisa wakapima tena vipimo na wakasema ana tatizo la ini kusinyaa (cirrhosis) sasa wakaanza clinic nao ila majibu ndo hayaeleweki na wamempa miezi 3 akaenyumbani ndo aje clinic hiyo ilikuwa mwezi wa January mwaka 2021 mpka nazungumza sasa ameshaenda kutolewa maji na kulazwa muhimbili mara 4 hadi sasa .

Naomba msaada wa kujuzwa vyema hili jambo wapi naweza saidia nimeambatanisha na baadhi ya dawa na majibu ya vipimo NAWASILISHA

View attachment 1704570View attachment 1704571View attachment 1704572
Mkuu pole sana endelea kumtibia hospitali ikishindikana nione kwa wakati wako ili nipate kumtibia dada yako ili aweze kupona maradhi yake auguwe pole .
 
Pole sana mkuu,
Mwanangu alianzwa na tatizo hilo nikaleta Uzi humu jf,alitolew maji na akaambiwa ana liver cirrhosis, vipimo tulifanya Aghakan Arusha nikapanga kwenda Nairobi Aghakan hawakupokea simu nikaghairi.

Tuliambiwa INI limesinyaa pale FAME arusha.kabla ya hapo alipewa vidonge vya mwezi mzima vya vidonda vya tumbo hapo hapo FAME.Tulihamia Rabininsia akaanziwa vipimo upya,wakagundua ana Cancer(lymphoma).

Ushauri mpeleke dada yetu Rabininsia memorial hospital akamuone Dr Primus Saidia ni Oncologist anaweza kumsaidia.Ni expensive kidogo vipimo na kumuona specialist kama huyo ni Tsh 30,000.Bima wanapokea usijali,kama sio Dada Josephine kwingine.

ningekwama,namshukuru na kumuombea kila Mara Mungu amfanyie wepesi katika mambo yake. Dada Josephine asante kwa msaada.
Kuna mdau amesema ma Dr ni changsmoto kufanya wrong diagnosis simpingi ni kweli ila wakati mwingine wrong diagnosis inapatikana kutokana na maelezo mabaya ya sisi wagonjwa.

Wagonjwa wengi hatujui kujieleza,tunawaogopa ma Dr.Unaweza kwenda na shida Dr akawa anakuzunguusha una umwa na hapa,je hapa je kule,mwisho pale pa mwanzo akirudi unakataa hapaumi.Wagonjwa tubadilike tuwe wawazi kwa Ma Dr tuondoe aibu na uoga.Kila LA kheri na Dada na MPE pole zangu za dhat.

Niliwahi kufuatilia liver transplant, mwaka 2018/2019 sikumbuki mwaka excactly,the cheapest was l think between U.S $ 30,000-45000 in India hapo hujainclude vitu kibao hiyo ni hospital charges tu.
Mkuu hana bima hili nalo nilikua nataka nijue utaratibu maana tunapoteza pesa kiasi na uchumi si mzuri kwa kweli ukizingatia ni miaka kama miwili mtu anaugua hii ni kichomi kwa kweli .Pia nashukuru sana naomba maelekezo ya kwenda hapo FAME na wanapatikana wapi?
 
Mtoto kupitia changamoto hz inauma sana-Kama mzazi pole sana.
Binafsi nilikuwa naumwa sana Acid reflux bila kujua,kwenda hospital daktari akaniandikia madawa ya koo ambayo kumbe side effect ya hzo dawa ni kupelekea ubaya wa tatizo langu.Tatizo lilipokuwa linazid kuwa baya zaid nikahamia hospitali nyingine ambapo Dr. akaniambia ni H pylori tumboni anasababisha,nikaamia kwenye hospitali nyingine kuthibitisha ndo nikakutana na Dr.Primus naye akaniambia ni H pylori,hapo at least confidence ikaja.
Kwa Tanzania,Referral hospital nzuri naona ni KCMC, Muhimbili mizunguko mingi sana.
Hakika its very painful hadi kuna muda unakufuru unatamani uumwe wewe yeye awe mzima
 
Mtoto kupitia changamoto hz inauma sana-Kama mzazi pole sana.
Binafsi nilikuwa naumwa sana Acid reflux bila kujua,kwenda hospital daktari akaniandikia madawa ya koo ambayo kumbe side effect ya hzo dawa ni kupelekea ubaya wa tatizo langu.Tatizo lilipokuwa linazid kuwa baya zaid nikahamia hospitali nyingine ambapo Dr. akaniambia ni H pylori tumboni anasababisha,nikaamia kwenye hospitali nyingine kuthibitisha ndo nikakutana na Dr.Primus naye akaniambia ni H pylori,hapo at least confidence ikaja.
Kwa Tanzania,Referral hospital nzuri naona ni KCMC, Muhimbili mizunguko mingi sana.
It was a very painful journey ila Allahu Akbar.
 
Mkuu hana bima hili nalo nilikua nataka nijue utaratibu maana tunapoteza pesa kiasi na uchumi si mzuri kwa kweli ukizingatia ni miaka kama miwili mtu anaugua hii ni kichomi kwa kweli .Pia nashukuru sana naomba maelekezo ya kwenda hapo FAME na wanapatikana wapi?
We uko wap mkuu tuanzie hapo.
Kuhusu bima usitangaze ugonjwa wa Dada wakati unamtafutia bima.kata bima ya NHIF japo hataipata kwa wakati ila huko mbeleni itamsaidia.
 
Nipo kigamboni dsm mkuu na je bima ya NHIF gharama yake ipoje,?
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom