Ndugu zangu habari za wakati huu. Naomba kupata ushauri na msaada toka kwenu. Hivi karibuni nilinunua mshine ya hiti kwa ajili ya kuprint express passport size. Sasa wakati naiwasha tu kwa mara ya kwanza ile controller yake ikawa haiwaki. Nikaenda kwenye ofisi ya jirani anamshine kama hii kujaribu controller yake ikafanya kazi hivyo nikajua kuwa tatizo ni controller na siyo machine. Kesho yake nikarudi kwa muhindi niliponunua cha kushangaza muhindi akasema hizo mashine hazina warrant so hawezi kunisaidia. Kwa kweli tulivutana kidogo lakini baadaye nikaona niwe na imani kidogo nimwachie MUNGU japo niliumia sana kwa kweli hiyo hela nimeipata kwa shida sana.
Sasa ndugu zangu kama kuna yoyote ambaye anatumia mashine hizi na nanajuzi juu ya mafundi au kama naweza kupata controller nyingine anijulishe.
Natanguliza shukrani kwenu nyote kwa mawazo na ushauri wenu