Msaada juu ya malipo ya minara | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msaada juu ya malipo ya minara

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Kiumbe duni, Feb 20, 2012.

 1. K

  Kiumbe duni Senior Member

  #1
  Feb 20, 2012
  Joined: Dec 3, 2011
  Messages: 100
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wana jamvi, naombeni mwenye kufahamu malipo ya makampuni ya cm yakiweka mnara kwenye uwanja wako.
   
 2. Entrepreneur

  Entrepreneur JF-Expert Member

  #2
  Feb 21, 2012
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 1,092
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Inategemea na mahali ulipo, kwani gharama za viwanja zipo tofauti kulingana na sehemu husika. Vilevile inategemea na mahitaji yao kwa hilo eneo lako (kama hawana option). But in any case isipungue laki tano
   
 3. K

  Kiumbe duni Senior Member

  #3
  Feb 21, 2012
  Joined: Dec 3, 2011
  Messages: 100
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ahsante mkuu
   
 4. F

  Fmewa JF-Expert Member

  #4
  Feb 23, 2012
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 294
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Kuna jinsi ya kuongelea suala hilo, unaweza kukodisha au kuwauzia eneo. Ila mie huwa naona ni vema ukawakodishia
   
 5. M

  Mama Joe JF-Expert Member

  #5
  Feb 24, 2012
  Joined: Mar 30, 2009
  Messages: 1,507
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Minara kimeo sana, labda uwe na eneo kubwa usilolihitaji
  niliwahi kukutana na mama mmoja rafiki yangu anahangaika na mkataba wao kwa mawakili, walipoingia mkataba kwenye mwaka 2005 hivi walimwambia malipo laki 5 kwa mwezi wanamlipa kwa mwaka mzima. Akasaini mkataba wa miaka 25, si unajua wanakuja kujenga mnara wao hivyo miaka ilingane na gharama ya ujenzi ili wasipate hasara, Tatizo kodi ni fixed kwa miaka 25, then waliamka tu siku moja na kumwambia wao wanakatwa kodi kubwa kwenye biashara hivyo na wao kuanzia leo ile malipo yao wanaikata kodi mama wa watu li mnara liridhia lijengwe mbele ya nyumba anayoishi hivyo akabaki hana hata sehemu ya kujenga kibanda apangishe au aafuge au kulima bustani, pili hakuna privacy tena unawapa access ya kuingia walinzi wao na kujaza mafuta nk. Mbaya zaidi madhara mengine kama moto na tusiyoyajua kutokana na kuwa na mnara jirani na nyumba
  Mpaka leo yule mama kawa kama amechanganyikiwa, malipo yameshuka hadi laki 3 kwa mwezi na hadi miaka 25 ijayo, labda mwingine atupe experince yake
   
 6. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #6
  Feb 24, 2012
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,121
  Likes Received: 615
  Trophy Points: 280
  Hao mawakili wa huyo mama vimeo! Hivyo ni vitu basic kabisa, ilitakiwa contract iwe inaconsider inflation rate na iseme kama laki 5 ni kabla au baada ya kodi.

  Mimi namjua mtu alipewa ofa ya milioni kadhaa nadhani ilikuwa 2 ila sikumbuki vizuri, ila akakataa kwa kuogopa radiation. effect.
   
 7. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #7
  Feb 24, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Hapa pa kuingia mikataba waTZ wengi tuu wabovu huwa tunakimbilia kusaini pasipokuisoma kwa makini kwanza kabla ya kuanguka saini
   
 8. M

  Mama Joe JF-Expert Member

  #8
  Feb 24, 2012
  Joined: Mar 30, 2009
  Messages: 1,507
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Inawezekana, lakini issue ni kuwa kampuni imejitenga na malipo yakaanza kufanywa na wengine ndio hao waliomweleza habari ya kodi
  tatizo akijaribu kuomba kumuona meneja wao anakataa au wanamzuia kwakweli kama alikuja fanikiwa kupata haki ni baada ya usumbufu sana
  pili kinachoogopesha miaka 25 kwa fixed rate!

   
 9. M

  Mama Joe JF-Expert Member

  #9
  Feb 24, 2012
  Joined: Mar 30, 2009
  Messages: 1,507
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  bora umesema, halafu kama ni matapeli, wanaweza kukwambia page zilikuwa nyingi hukusoma, ogopa sana!
   
 10. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #10
  Feb 24, 2012
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,121
  Likes Received: 615
  Trophy Points: 280
  Kama mkataba ungekuwa uko sawa kungekuwa hakuna haja ya kumwona mtu yoyote, lakini ameshasign mkataba mbovu wanajua kufanya lolote itakuwa ngumu ndo maana wanamyanyasa.

  Hiyo fixed rate ndo nasema ni makosa ya wakili wake kutomshauri, kulitakiwa kuwe na adjustment kila baada ya kipindi fulani ili kuweka sawa at least kulingana na inflation rate.
   
 11. M

  Mama Joe JF-Expert Member

  #11
  Feb 24, 2012
  Joined: Mar 30, 2009
  Messages: 1,507
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Asante kwa kutujuza, ni kweli watu wanasaini tu kwa sababu ya shida ila baada ya muda inakuwa kitanzi hasa.
   
 12. Entrepreneur

  Entrepreneur JF-Expert Member

  #12
  Feb 24, 2012
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 1,092
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  [FONT=&amp]Mama Joe uko sahihi kabisa na umenikumbusha ghiliba zinazofanywa na makampuni ya wajanja wachache ili kujinufaisha wao. Hivi unajua mikataba hii huandaliwa na kampuni husika? Ni kwa nini nikataba hii inaandaliwa kwa lugha lugha ya kimombo? Lugha ambayo kwa baadhi ya jamii zetu haieleweki vizuri? Je ni kweli kwamba mtu anaposaini mkataba huu na haya makampuni ya simu anajua kilichoandikwa?[/FONT][FONT=&amp] Ni kweli kwamba sheria inaamini kuwa pale pande mbili husika katika mikataba zinapoingia mkataba baina yao basi mkataba huu ni muhimu uheshimiwe kwa sababu sheria huamini kuwa wahusika hawa wanakuwa wameshapima na kuzifahamu bayana faida na athari za kile wanachokifikia uamuzi[/FONT]

  [FONT=&amp]Lakini, hakuna ambaye hafahamu pia kuwa si mikataba yote huingiwa kwa nia nzuri kwa sababu mara kwa mara kuna upande fulani unaingia mkataba kwa minajili ya kufanya hadaa, hila, udanganyifu au kwa dhamira na makusudi mazito, kuupunja upande mwingine wa mkataba.[/FONT][FONT=&amp]Katika hili, sheria imeingilia kuulinda upande dhaifu na hivyo kukubali kupindisha kidogo kanuni ya kawaida kuwa kila mkataba ni vema uheshimiwe kama ulivyo. Sasa tuangalie ni nyakati gani ambapo sheria au mahakama inaweza kusema kuwa 'hapana…mkataba huu si halali.'[/FONT][FONT=&amp] Katika dhana hii sheria inasema kuwa ithibitikapo kuwepo kwa ulaghai ama udanganyifu wa ina nyingine yoyote katika makubaliano yanayozaa mkataba, basi mkataba huu si halali kwa vile upande uliodanganywa haukufanya maamuzi yake ukiwa huru ki-akili au katika mazingira yaliyosababisha ulazimike kuingia mkataba huu.
  [/FONT]
  [FONT=&amp]Uthibitisho wa hili ni ile kesi ya Sluis Brothers (E.A) Ltd Dhidi ya Mathias na Tawari Kitomari ambayo ilitolewa hukumu na Mahakama ya Rufaa ya Tanzania, mwaka 1979. Kampuni hii ilikuwa imeandaa mikataba iliyoandikwa katika lugha ya kimombo na ambapo wakulima wasio na kisomo walikuwa wakisaini na walifanya hivyo bila kujua kile kilichoandikwa.[/FONT][FONT=&amp] Na uamuzi uliotolewa mahakamani ulionyesha kuwa kampuni hii ilifanya hivyo makusudi kwa lengo la kuwanyonya wakulima hawa kwa vile iwapo mikataba hii ingekuwa imeandikwa katika lugha rahisi ama wangefafanuliwa zaidi kile kilichoandikwa humo pengine wasingekubali kuisaini na kutekeleza matakwa ya mikataba hiyo. [/FONT]
   
 13. Entrepreneur

  Entrepreneur JF-Expert Member

  #13
  Feb 24, 2012
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 1,092
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  MKuu uko sahihi, ni kweli kwenye mikataba watu wengi tunakimbilia kusaini, (nadhani ni sababu ya njaa) lakini tuna tatizo kubwa zaidi, Je ni wangapi wanaelewa kile kilichoandikwa kwenye mikataba hiyo kama lugha ni ya kimombo?

  Mikataba mingi ya minara niliyoiona imetayarishwa na kampuni husika ya simu kwa lugha ya kimombo. Je hizi si ghiliba zinazofanywa na makampuni ya wajanja wachache ili kujinufaisha wao binafsi. Nadhani umefika wakati wa kutumia ile pleading ya [FONT=&amp]Non est factum[/FONT][FONT=&amp], (it is not my deed)[/FONT] kwa wale tusiojua lugha iliyotumika kwenye mkataba
   
 14. K

  Kiumbe duni Senior Member

  #14
  Feb 25, 2012
  Joined: Dec 3, 2011
  Messages: 100
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ahsanteni sana kwa mawazo mazuri, kitu nilichogundua ni kwamba wazungu wameshagundua udhaifu wetu kwa hiyo hawatumii nguvu kutulaghai, wanawatumia watanzania wenzetu kutulaghai. Huwa wanakubali kupewa kitu kidogo ili kutushawishi kuingia mikataba mibovu, wanaona ni bora wapokee kidogo kuliko kukusaida ufaidike.
   
 15. d

  dav22 JF-Expert Member

  #15
  Feb 25, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 1,902
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  wazungu washatuona kimeo aisee...yaani mnara unawekwa kwenye kiwanja chako alafu unalipwa laki tano kwa mwezi wakati mnara huo mmoja unaingiza zaidi ya mamilioni kadhaa kwa kampuni husika alafu wewe uliye karibu na mnara unadhidi kuathirika na radiation effect ambazo makapuni hayataki kuziweka wazi kila siku...,.this is bull shit..!!
   
Loading...