JituParaTupu
Member
- Nov 20, 2008
- 92
- 9
mkuu kwani ni total au partial loss?
Ninamiliki gari ambayo nilikatia bima ya Comprehensive ya kuwa compensated 9m/- na nimekuwa nikikata bima hii kwa takriban miaka 6. Gari yangu ilipata ajali na kesi kufanyika na makosa kuonekana kwa yule aliyenigonga. Nimeshangazwa kwa kulipwa chini ya milioni moja kinyume na matarajio yangu ya kulipwa 9m au 8m. Naomba kuelimishwa jinsi ya kudai haki yangu. Nawakilisha nikitegemea kusaidiwa gaps jamvini.
Swali la msingi sana! Pia sielewi issue ya kesi inaingiaje kwenye comprehsnsive insurance, kwa kuwa hata kama wewe una kosa, so long gari yako ina comprehensive cover kampuni yako ya bima lazima ukulipe.
Hivi kuna umuhimu kweli wa kufanya bima ya magari binafsi kuwa ya lazima? Naona ingefanywa hiari kwa anayetaka..ni wazo tu wadau
Mkuu nchi nyingi kama sio zote bima za magari ni lazima kutokana na kwamba madhara yanaweza kumpata mtu wa tatu (Third paty) ambae hausiki.. for instance, wewe unatembea barabarani alafu kwa bahati mbaya gari likakugonga hapo unatakiwa kupewa compensation. mfano mwengine, umekaa mahali labda kuna ujenzi unaendelea kwenye jengo tuseme gorofa alafu nyundo ikakudondokea(Public liability)
mkuu unalipwa kilicho haribika. kama gari haifai kuingia barabarani ndo unalipwa gari jipya. gari yako hata ikitengenezwa kuna gharama hata wewe itakupasa kutoa, 10% ya gharama ya matengenezo utatoa wewe wengine ni zaidi au pungufu ya hapo inategemeana na kampuni ya bima. hiyo gharama ni kama tozo la kukufanya usijiachie barabarani eti kwa kua una bima. hata wewe unachangia gharama. mia
.Maelezo mazuri lakini kasoro ipo hapo kwenye kulipya gari jipya.most ya magari yetu ni used so utalipwa kulingana na uchakavu wa gari yako.Kama umenunua gari mpya kutoka kwa dealer eg D.T Dobie na bahati mbaya ukapata ajali ndani ya mwezi mmoja hapo unalipwa gari jipya kwa sababu depreciation itakuwa very minimalmkuu unalipwa kilicho haribika. kama gari haifai kuingia barabarani ndo unalipwa gari jipya. gari yako hata ikitengenezwa kuna gharama hata wewe itakupasa kutoa, 10% ya gharama ya matengenezo utatoa wewe wengine ni zaidi au pungufu ya hapo inategemeana na kampuni ya bima. hiyo gharama ni kama tozo la kukufanya usijiachie barabarani eti kwa kua una bima. hata wewe unachangia gharama. mia
Ndugu zangu jamvini nachukua fursa hii kwa wote waliochangia na kushauri kwa njia moja au ingine. Nimeweza kuelewa kila kilichoandikwa nanyi katika kutaka kunisaidia. Kesho naahidi kuja na full information kuhusiana na ajali na tatizo langu katika ujumla wake na nadhani kuanzia hapo mtaweza kunipa ushauri mzuri kuelekea kulipwa bima yangu. Izingatiwe kwamba ni mara yangu ya kwanza kupata ajali ya barabarani tangu nianze kumiliki chombo cha moto mnamo mwaka 1986. Asanteni sana ...ni hapo kesho.