Msaada juu ya kuwasha PC power supply

Srebrina

JF-Expert Member
Jan 28, 2012
944
405
Habarini wakuu, wikiendi nzima mpaka Leo nimekuwa nikihangaika na project ya kutengeneza portable lab power supply and universal power adapter

Katika project yangu hii Nilikuwa nikitumia Dell PS-5301-7D ambazo ni toleo la zamani kidogo kama 1998 mpaka 2000

Power supply hii huwa haiwaki mpaka iwe imekonectiwa na motherboard ivo nilifanikiwa Ku google na kupata PS_ON ambayo ni Grey wire connected with Black ground wire. Kwa mwanzo nilifanikiwa kuiwasha na Ku boot laptop yangu inayotumia volt 19.5 lakini shida ikaja output voltage ilikuwa ni 18 volt ivo ikawa iki load window ina restart tena.

Hapo nikawa na idea ya kuchukua +12v na -12v nipate 24v then nichukue 24v ambayo itakuwa positive na +5 nipate 19v

Sasa shida imekuja baada ya kuizima kila nikiiwasha inashtua multimeter inasoma 19v mpaka 20v alafu inazima. Nimegoogle jibu nikaambiwa nifunge load ili iwork kama nilivofanya mwanzo nikarudia kwa kuweka LED lakini kazi ikawa inastua na kuzima

Color za wire ni
Black = GND
Yellow = +12v
Blue = -12v
Red = +5v
White = -5v
Grey = PS_ON
Orange = +3.3v

Pia hizi sizijui kazi yake

Purple
Blue mixed with White

Naombeni msaada wenu nifanyaje ili iwake na ikae constant bila kukaa in standby mode?

Samahani kwa kuandika mambo mengi
 
Back
Top Bottom