Muccobs wanatoa Procurement and supplies management na nadhani TIA pamoja na CBE wanatoa hiyo hiyo. Ila Mzumbe,kama sikosei wanatoa Procurement and Logistic. Ila haijalishi unasoma wapi. Kwani mwisho wa siku ili uweze kutambulika itakupasa kufanya mitihani ya PSPTB ambayo ni bodi inayosimamia hizo course. Na ukifanya ukafaulu utakabidhiwa CPSP. Ambayo itakuwa inakutambulisha kama mtaalamu wa Manunuzi na ugavi. Wewe usijali nenda soma hapo hapo,usiyumbishwe.