Msaada: Jinsi ya kuwa na roho ngumu mbaya

Sigara Kali

JF-Expert Member
May 28, 2017
3,623
8,428
Wana MMU

Kiukweli nilizaliwa na kulelewa katika mazingira ya kistaarabu, ya kujali utu , nimekua naishi na watu vizuri kwa wakati huo still nipo na wazazi

But wazazi walipotangulia mbele za haki watu wakaanza kunigeuka hasa ndugu so tangu nipo mdogo nasoma form 1 nkaanza kuishi ghetto hadi nafika university,wakati wote huu nimekua nikikumbana na maumivu mbalimbali ya kimaisha na kimapenzi na wanawake nliowahi kutoka nao

Nimekuja kugundua ukimya wangu na upole wangu watu wananiona bwege hasa hawa wanawake na huyu mwanamke nliemzalisha, ananiletea jeuri na dharau za kijinga kisa tu ana kijikazi chake na salary halafu anataka aje awe mke wangu,kiukweli ananiumiza kwa vingi

Sasa nasema imetosha ,nipeni mbinu za kuwa na roho mbaya ngumu nianze kwenda nae kibabe manake nimembeleza na kumpeti peti naona ameniona boya.Kama hataki mapenzi na Mimi aseme kuliko kuniletea masuala ya kuumiza roho

Sigara kali
 
roho mbaya kwa ajili ya mwanamke mmoja tu? chukua maamuzi ya kawaida tu, tunaita uamuzi wa kiume
 
Mungu hawezi kukupa roho mbaya maana anajua matokeo yake si mazuri.

Ishi kigumu ili uyamudu maisha magumu. Usiishi kwa roho mbaya utajimaliza mwenyewe.

Mshirikishe Mungu ili akuondolee utata wako maishani mwako.
Amini, mambo yako yanavyokuwa magumu kwa Mungu ndivyo yanavyozidi kuwa mepesi.
 
Pole sana...

Haina haja ya kujibadilisha vile usivyo...

Fanya unaloona sawa, achana na unaloona halifai, usiumize kichwa...

cc: mahondaw
 
Ukijielewa utajua nini cha kufanya,hata uwe na roho mbaya ya Kuua paka kwa magoti Haito saidia
 
Ya kwanza na umuhimu...tafuta mwanamke mzuri zaidi yake na mwenye sifa tofauti na yeye,kama yeye mweusi tafuta mweupe,kama yeye mwembamba tafuta bonge,kama anasura ngumu tafuta mrembo...anzia hapo halafu utaleta mrejesho
 
Wana MMU

Kiukweli nilizaliwa na kulelewa katika mazingira ya kistaarabu, ya kujali utu , nimekua naishi na watu vizuri kwa wakati huo still nipo na wazazi

But wazazi walipotangulia mbele za haki watu wakaanza kunigeuka hasa ndugu so tangu nipo mdogo nasoma form 1 nkaanza kuishi ghetto hadi nafika university,wakati wote huu nimekua nikikumbana na maumivu mbalimbali ya kimaisha na kimapenzi na wanawake nliowahi kutoka nao

Nimekuja kugundua ukimya wangu na upole wangu watu wananiona bwege hasa hawa wanawake na huyu mwanamke nliemzalisha, ananiletea jeuri na dharau za kijinga kisa tu ana kijikazi chake na salary halafu anataka aje awe mke wangu,kiukweli ananiumiza kwa vingi

Sasa nasema imetosha ,nipeni mbinu za kuwa na roho mbaya ngumu nianze kwenda nae kibabe manake nimembeleza na kumpeti peti naona ameniona boya.Kama hataki mapenzi na Mimi aseme kuliko kuniletea masuala ya kuumiza roho

Sigara kali
Mkuu kuna uzi hapa jamvini ulisema ni mjamzito. Mvumilie labda huo ujauzito ndio unamsababisha awe na usumbufu huo.
 
Back
Top Bottom