Msaada: Jinsi ya kuvuta maji kutoka kisimani

Msaada: Jinsi ya kuvuta maji kutoka kisimani

KISHINDO

JF-Expert Member
Joined
Jun 23, 2013
Posts
2,203
Reaction score
1,957
Habari ya kazi ndugu yangu.

Mahali nilipo hapana umeme na nimefunga mfumo wa maji nyumba nzima hivyo naomba msaada wa kujua nini kinachohitajika ku-supply maji toka kisimani kati ya MOTOR au WATER PUMP.

Kama vitahitajika vyote kwa pamoja naomba msaada pia.

Natanguliza shukran zangu za dhati.
 
Wajuzi wanakuja!

Huku magomeni tunatumia mabomba ya Magufuli hatuna visima.
 
ukienda kwa duka, ukasema nataka 'water pump' utaulizwa ni ya aina gani

akiwa na maana, pump inahitaji 'prime mover(PM)' kuendeshwa

1. ya umeme (wa tanesco au solar), inatumia motor kama prime mover

2. ya petrol, inatumia gasoline engine kama PM

3. ya mkono, mchawi mkono wako
etc

kwa matumizi madogo kama ya nyumbani, pump hua zinaungwa PAMOJA na PM, kama HII

so ukisema , nahitaji water pump ya umeme, AU ya petrol, inatosha
 
Hapo mkuu unaweza kununua submersible pump inayoendeshwa na solar panel.

Ukiwapata jamaa wa sim-solar watakiwlekeza vizuri sana. Ila gharama yake sasa itabidi uombepo!

Vinginevyo pata water pump za Honda yenye uwezo wa kuvuta let say 5-10m kutoka ardhini na kupandisha mita kadhaa kwenda kwenye tangi.
 
Habari ya kazi ndugu yangu.

Mahali nilipo hapana umeme na nimefunga mfumo wa maji nyumba nzima hivyo naomba msaada wa kujua nini kinachohitajika ku-supply maji toka kisimani kati ya MOTOR au WATER PUMP.

Kama vitahitajika vyote kwa pamoja naomba msaada pia.

Natanguliza shukran zangu za dhati.
Ngoja nikutumie PM namba za jamaa wa simu-solar uongee naye atakupa maelekezo mazuri sana
 
Ukihitaji Sola nitafute(Betri na Panel),ninazo za Watt 120 na Watt 200 Mpya na Used,nauza bei poa sanaaaa karibu na bure,yaani bei zangu huwezi kuzipata mahali popote Tanzania hii,0620333409
 
Ukihitaji Sola nitafute(Betri na Panel),ninazo za Watt 120 na Watt 200 Mpya na Used,nauza bei poa sanaaaa karibu na bure,yaani bei zangu huwezi kuzipata mahali popote Tanzania hii,0620333409
Bei mkuu
 
Unaweza ukajitengenezea mfumo wako wa umeme pia kwa kutumia oil chafu, makaa ya mawe, pumba au maranda ya mbao.
Au tumia solar , au generator.
 
Utahitaji pump, iwe ya umeme au engine. Pump ya umeme inakuja pamoja na motor yake na utahitaji umeme wa solar. Pump ya engine inakuja na engine yake ya kuiendesha na utahitaji mafuta (diesel) ya kuendeshea. Then fanya setup kama hiyo hapo chini. Maji unajaza kwenye tank, then pressure ya matumizi ya ndani unapata kwa gravity. Kwa namna hiyo pump utatumia kujazia tank tu. Na muda mwingi inakuwa imepumzika. Pia utapunguza matumizi ya nishati (umeme au diesel) ya kuendeshea pump hiyo.
download.jpg
 
Back
Top Bottom