Nenda Ubalozi wa Uingereza utapata taratibu zote.
Kabla hawajatoka kwenye Umoja wa Ulaya ilikuwa inatumika viza ya Shenghen ambayo mtu alikuwa anaendai katika nchi zaidi ya 20 za Umoja wa Ulaya bila kuulizwa.
Ili mtu aipate hiyo Shenghen Visa alipaswa awe na:-
1. Barua ya mwaliko kule aendako
2. Returning air ticket
3. Bima
4. Booking Hotel
5. Passport
Lakini pamoja na hivyo vyote mhusika alipaswa aende ubalozini kujaza form, alipe Tsh. 162, 000 na asailiwe. Pale atakapofaulu usaili ndo ataweza kupewa Visa.
Binafsi nilipitia mchakato huo na nikaipata ingawa walinisumbua kutaka nyaraka kadha wa kadha ili wawe na uhakika kama ntarudi Tz mbali na hizo nilizoorodhesha hapo juu.
Haikuwa vigumu kwangu kuwapatia nyaraka hizo kwa sababu nilikuwa nazo.
Mwisho wa siku wakanipatia Visa nikasepa zangu kwa Malkia.