Msaada: Jinsi ya kupata Visa - Dubai

Msaada: Jinsi ya kupata Visa - Dubai

Maajent ni wengi mkuu.
Maajent wengine watakwambia upate mdhamini kama hujawah kufika dubai jaribu kumwambia unakwenda kibiashara mambo mengine utafanya ukifika duba.
Ahsante kiongozi,ngoja nijaribu kesho,maana nimetoka Airport saa hizi,nimeambulia patupu,maagent wengi ni wa 14 days tu,sijafanikiwa.
 
Ongea nao vizuri ukihitaji visa kuanzia miezi3 au miezi 6 unaweza kuongezewa harama.

Nakushauri chukua visa ukifika dubai kila kitu unafanya kuongeza muda.
Ndio maana nimekuja hapa kuuliza Mkuu,maagent wengi wananiambia wanatoa visa ya siku 14 tu(Tourist Visa),na hakuna kuongeza siku pia si ruhusa kutafuta kazi kwa hiyo Visa.
 
duke wewe nenda hata kama utapewa viza isiyohitaji kutafuta ajira ukifika tafuta hakuna atakayekufuatilia kuangalia kama unatafuta.


ya miezi 3 au miwili inakutosha kutafuta kazi.
 
duke wewe nenda hata kama utapewa viza isiyohitaji kutafuta ajira ukifika tafuta hakuna atakayekufuatilia kuangalia kama unatafuta.


ya miezi 3 au miwili inakutosha kutafuta kazi.
Ahsante sana kiongozi,kwa hiyo nisigusie kabisa suala la kazi kipindi natafuta Visa si ndio Mkuu Daby?
 
Ahsante Mkuu!!.
Cha muhimu ni wewe kupata data za uhakika kama ukienda na ya siku 14 unaweza kupata kazi, na kama ukipata kazi watakukubalia kubadilisha na kubaki huko huko. Ni vizuri sana upate mtu aliyeko huko akuelezee. Usikubali kuondoka bila kuwa na uhakika kwani utajikuta umerudishwa Bongo na fedha zako zimepotea bure.
 
Shukrani Boss!!.
Halafu mkuu kuna huyu member wa JF yeye alifuata mkondo huo huo unaotaka kufuata. Soma hii thread aliyoeleza jinsi alivyokwenda na masaibu aliyopata ili ufanye uamuzi wa busara. Jaribu ku-PM ni mtu member ambaye anaona yuko wazi sana atakakupa maarifa zaidi. Thread yake ni hii: Hatua nilizopitia mpaka kufika Ukraine, na bado niko njiani kwenda nchi ya ahadi Norway

Baadhi ya maelezo yake ni haya, lakini nenda kwenye thread yake niliyokuwekea link utaona kwa kirefu zaidi.
''Nikapita sehemu nikakuta kuna watu wanasema visa za Dubai, lilikuwa Tangazo, mwanaume nikawauliza wakasema visa ni laki 3 ya miezi mitatu, ila kwakuwa wewe hatukujui tutakupa ya wiki mbili, nikasema sawa, nikadhani Dubai ni kama Morogoro unaenda tu unafika unaanza kutafuta kazi, kumbe kuna hata muda unaoruhusiwa kukaa kwenye visa, sikuwa najua neno overstay wala nini, nikaenda Kigamboni nikauza shamba langu kwa milion 2.8 lilikiwa nimeshapataga value, nikapata visa 150 USD na hela ya ticket 400 USD Emirates lilikuwa msimu wa punguzo wa ramadhani, nikapanda mpaka Dubai , hapo sijui mtu yeyote uko naenda tu.

Nikafika nikapata hotel nikalala siku moja alafu nikaamua kusaka chumba cha kupanga, aisee kumbe hakuna chumba cha kupanga wana Bed spaces mnashare rooms, ni AED 500 Sawa na laki 3 ya Tanzania kwa mwezi, hela yangu ilikuwa ndogo sana nikalipa week mbili nkidhani kwamba nitapata kazi mapema nihame, week mbili zikaisha na visa ya week mbili inaisha hakuna kazi nilipata ilikuwa ni ni presha mno.

Agent aliyenikatia Visa akaanza kunipigia na vitisho juu akaanza kulaumu kwamba una overstay nimefungiwa visa mpya nazo apply.

Hapo tarehe ya ndege ya kurudi ishapita sina nauli ya kurudi Tanzania, nikafikiria nifany e nini, nikaanza kusaka kazi ndani ya overstay days, nikapata kazi moja ya mauzo kampuni ya Alhairay Printing services.

Nikawapa makaratasi yangu yote wakaenda kuapply work permit ikabounse maana nilikuwa kwenye overstay fines, wakasema hatuwezi kukuajili wewe uko kwenye overstay......'


Mzee mmoja wa Pakistan akasema nitakusaidia akanilipia nauli nirudi Tanzania ila nikamuomba kwamba naomba unilipie niende Rwanda maana Tanzania wale ma agent walisema wamefungua kesi kesi niwalipe fidia za kukosesha kazi zao kwa u overstay miez miwili na nusu.

Lakini suala ni kwamba airport lazima ulipe fine.

Kwa kila siku unayozidisha ni 100 AED Sawa na 60,000 ya Tanzania na hapo nishaoverstay karibia siku 80, na sina kitu ilibidi nilipe kama milioni 3 ya Tanzania,

Nikajitosa kwamba naenda hivo hivo, nikafika airport wakanizuia kwamba nilipe fine au niende ku surrender wanajifungu watu wanifunge miezi Mitatu kama sina faini dahhhhhhh
!''
 
Cha muhimu ni wewe kupata data za uhakika kama ukienda na ya siku 14 unaweza kupata kazi, na kama ukipata kazi watakukubalia kubadilisha na kubaki huko huko. Ni vizuri sana upate mtu aliyeko huko akuelezee. Usikubali kuondoka bila kuwa na uhakika kwani utajikuta umerudishwa Bongo na fedha zako zimepotea bure.
Kwl Mkuu,ndiyo maana nimeandika kama kuna mtu aliyeko Dubai angenipa taarifa kamili ingenisaidia sana!!.
 
Ni wazo zuri kiongozi,nimeshajaribu pia,kuhusu kujenga uchumi wa nchi yangu,naimani hata nikiwa huko bado naweza kuujenga,si lazima niwe hapa hapa nchini Mkuu!!.
Achana na nchi yako. Kajenge uchumi wako binafsi. "nchi" ni mwanamke mgumu sana na wanamtumia vibaya sana. Pambana mkuu, na hivi bado upo single, time ni sasa.
 
Back
Top Bottom