Msaada jinsi ya kuongeza "confidence"

Ukitaka comfidence iongezeke (1) jifunze kuongea chochote kila mara kwa mtu yoyote hasa kwa wale unaosoma nao , kila mmoja jaribu kumzoea kuwa kama rafiki , tafuta mada yoyote uwe unaongea (2) Mazoezi ya kukimbia na pushap yatakuwezesha uwe na pumzi na kujiamini (3) uwe mtu wa kusoma chochote vitabu au masomo au Udaku itakusaidia (4) kaa kwnye magroup ya watu wanao ongea kama Vigenge na Sehemu za watu wanao cheza draft utabata Ubunifu wa kujifunza vitu vingii (5) muombe MUNGU hii itakuwezesha kuwa strong in faith

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
1. Usiwe na mawazo hasi (negative thoughts)
2. Usijilinganishe na mtu yoyote. Jua kua umeumbwa tofauti na mtu yotote hapa duniani
3. Jitambue. Tafuta mambo unayoweza na unayopenda kufanya kisha yafanye. Utajiona mshindi
4. Saidia wengine. Jinsi wanavyokushkuru itakufanya uongeze confidence kua unafanya jambo la maana kwenye jamii inayokuzunguka
5. Vaa vizuri (modesty). Ni chaguo lako, lakini vaa nguo utakayojiskia huru. Obviously hapo ni nguo zisizoleta maswali kwa jamii mf. Fupi, tight, inayoonyesha, mlegezo nk. Utajiona huru kwakua hautavutia macho ya watu (negatively)
6. Soma kwa bidii (kama bado) au kazana ktk kazi ili ufanikiwe. Hautajiskia kudharaulika kama una kazi yako nzuri au biashara.
7. Usiogope kukosolewa. Na kama mtu anakukosoa mambo ya uongo usitilie maanani. Kama ni ya kweli jirekebishe.
8. Usiwe mlalamishi. Watu wakisoma una hiyo tabia watakuonea na utaendelea kukosa confidence
9. Soma vitabu vya Mungu. Kama ni mkristo, biblia ina maneno mengi ya kukufariji.
10. Google, soma vitabu utapata zaidi
 
Tiba yake inaitwa face your fear!yaani pale ukihisi kukiogopa kitu flani basi jilazmishe ukifanye utakuta unajengea ubongo kwamba ulikuwa unaogopa bure tu!hayo matatizo yanapata wengi hata ambao walikuwa hawaadhibiwi sana nyumbani hupoteza kujiamini.ubongo uko flexible sana unavyoufanyia ndivyo unavyofuata ukiuzoesha kujiamini utajiamini ukijishusha wenyewe unakushusha hadi kina cha mwisho!
Kikubwa unahisi labda ukiongea mbele za watu utaonekana umesema pumba
 
1. Usiwe na mawazo hasi (negative thoughts)
2. Usijilinganishe na mtu yoyote. Jua kua umeumbwa tofauti na mtu yotote hapa duniani
3. Jitambue. Tafuta mambo unayoweza na unayopenda kufanya kisha yafanye. Utajiona mshindi
4. Saidia wengine. Jinsi wanavyokushkuru itakufanya uongeze confidence kua unafanya jambo la maana kwenye jamii inayokuzunguka
5. Vaa vizuri (modesty). Ni chaguo lako, lakini vaa nguo utakayojiskia huru. Obviously hapo ni nguo zisizoleta maswali kwa jamii mf. Fupi, tight, inayoonyesha, mlegezo nk. Utajiona huru kwakua hautavutia macho ya watu (negatively)
6. Soma kwa bidii (kama bado) au kazana ktk kazi ili ufanikiwe. Hautajiskia kudharaulika kama una kazi yako nzuri au biashara.
7. Usiogope kukosolewa. Na kama mtu anakukosoa mambo ya uongo usitilie maanani. Kama ni ya kweli jirekebishe.
8. Usiwe mlalamishi. Watu wakisoma una hiyo tabia watakuonea na utaendelea kukosa confidence
9. Soma vitabu vya Mungu. Kama ni mkristo, biblia ina maneno mengi ya kukufariji.
10. Google, soma vitabu utapata zaidi
Well said, kama wewe ni KE unafaa sana sababu una ushauri mzuri sana!
 
CONFIDENCE:
a state of being aware.

CONFIDENCE APPROACH
Ⅰ.Recognise your insecurities.
Ⅱ.Always remember no one is perfect.
Ⅲ.Identify your success
Ⅳ.Discover things at which you excell and focus on your talents
Ⅴ.Take pride in your talents…
 
Habari zenu wanajamvi,

Leo ningependa kufundishwa njia zitakazo niwezesha kuwa mtu wa kujiamini niwapo mbele ya watu. Nasikitika sana juu ya tatizo hili ambalo toka utotoni mwangu hii nimegundua jinsi malezi yangu yalikuwa ndiyo chanzo cha kupungua kujiamini kwani nilikuwa napigwa sana hivo kuuliza kitu ama kuongea ilikuwa ngumu kwangu hivo mpaka sasa nimekuwa muhanga mkubwa.

Naomba kujuzwa mbinu zitakazonifanya niwe bora zaidi katika kujiamini,
Kwani now najiandaa kwenda chuo nikiwa na tatizo hili ndani ya kichwa changu.

  1. Shiriki sana katika Midahalo.
  2. Penda sana kujumuika na Watu na changia bila kujishtukia.
  3. Penda sana kuwafuatilia wale wote ambao kwako unawaona ni Mfano wako wa Watu wanaojiamini.
  4. Jenga tabia ya kuwa mbishi au kuanzisha ubishi hasa katika kadamnasi ya Watu.
  5. Jifunze kuwa Mtu wa utani utani mwingi.
  6. Hakikisha knowledge bank yako ni ya kutosha kwani 99.9% Confidence hunogeshwa na IQ kubwa ya Mlengwa.
  7. Jikite mno katika kufanya mazoezi ya kati au magumu kwani mara nyingi Confidence hujengwa na uimara wa mwili kwani mwili legelege huzaa " jitu " lisilojiamini siku zote.
 
Vuta bangi kidogo just once, fanya hivyo mara moja kwa wiki, kwa wiki 4.. . Alafu tumia korosho za kukaanga kwa muda wowote... hutaona uwoga au aibu au kujiona weak...

If ur a man, una upungufu mkubwa hormone za kiume...!!

you are said to have confidence when you believe that you are capable of doing something worthwhile.
mkuu confidence inaanza tu pale utakapo amini uko tofauti na yeyote,zingatia hvi 1:tambua hujaja duniani kwa ajali umekuja dunian kwa makusudi yakuchangia vitu vzur vitendeke dunian
2:kila unapofanya jambo zingatia na kufikiria matokeo lazma yawe mazuri
3:acha kujifananisha na kujidharau
 
Usitazame ulipotoka kwanza ili uondoe lawama kwa makuzi yako na uliweke suala hili kama jukumu lako ......

Usiwe na hofu katika kukosea maana tunajifunza kupitia makosa mbalimbali hivyo, kuondoa hofu hii ili uyajue madhaifu yako ni hatua ya kwanza
"MFICHA UCHI HAZAI".

Tafuta maarifa kwa kusoma kwa bidii ili uweze kuyapangilia mawazo yako katika mtiririko mzuri na wenye kuvutia.....

Jitahidi kuchangamana na watu hasa wenye uelewa mzuri wa mambo yakuvutiayo na utakayo kuyafanya kwa usahihi kwa kuwa
" TUNAJIFUNZA MAMBO MENGI KUPITIA WATU"

Usiwe mbinafsi Bali uwasaidie wenzio pale uwezapo ili uongeze thamani ya maisha yako kwa watu wengineo maana kukubalika huongeza kujiamini , kujielewa , kujikubali na kujithamini.......
 
Ni kweli suala la confidence ni changamoto kubwa sana hasa kwa watoto na vijana wengi Africa ikiwemo Tanzania. Mila, desturi, uelewe duni, umaskini na changamoto za malezi zimechangia kwa kiasi kikubwa vijana pindi wanapokua kukosa kujiamini. Ukiwasoma kina Erick Erickson na Piaget katika andiko la hatua za ukuaji, hasa stage namba 3-Initiative vs Guilt, Stage 4-Industry (competence) vs inferiority na Stage ya 5-identity vs identity confusion, utaona ni jinsi gani kama walezi na wazazi wasipojitambua katika malezi wanaweza moja kwa moja kuathiri mtoto kijiamini, kujisimamia, kujiamua, na kadhalika.

Mtoto anataka kushika remote control ya TV, baba/mama unamkemea achaaa, ntakupiga, au hata kumpiga kabisa. Mtoto anajaribu kuongea au kushiriki mhadala wa familia, anaambiwa nenda chumbani; akikosea matamshi anachekwa; mtoto anarudi shule amefeli somo, anapigwa, anaambiwa maneno ya kuudhi kama vile Kichwa maji, bongolala, nk. Mambo kama haya yanaathiri mtoto, hawezi kujiamini, na hata mwisho wa siku, uwezo wake wa kuvumbua ama kugundua mambo unadhoofika. Jinsi utakavyoandaa mtoto wako ndivyo atakavyokuwa baadaye.
 
Ukienda chuo naamini kuna somo la communication skills na mada ya presentation itakuwepo watakufundisha namna ya kupresent mada zako na namna ya kujiamini.
 
CONFIDENCE:
a state of being aware.

CONFIDENCE APPROACH
Ⅰ.Recognise your insecurities.
Ⅱ.Always remember no one is perfect.
Ⅲ.Identify your success
Ⅳ.Discover things at which you excell and focus on your talents
Ⅴ.Take pride in your talents…
Kwy 5! Unaweza kufuatilia vizuri mfn timu unayoipenda labda simba,yanga,kauzu,au manu au juve,chelsea alafu ijua vizuri iyo team,list y wachezaji etc alafu nenda kwy kibanda umiza au bar siku wakiwa na mechi kaa mbele au katikati anza kubishana na watu kwa fact then ukitoka hapo utaona levele yako ya confidence imepanda!fanya mara kwa mara utajikuta inakupa kujiamini,unaweza kuongelea hata siasa na kwy kundi kubwa la watu itakusaidia! Ukifika chuo gombea uongozi wowote pia etc itakusaidia!
 
Ndugu uko chuon Kuna presentation ambayo unajianda mapema one week kabla ya hiyo siku komaa na part yako. Lakini kitu cha msing confidence utaipata unapokutana na lecture nuksi Ana point mtu yeyote kuanza ku present. But kama Kuna DEBATE CLUB jiandikisha. Hii debate ingebidi kushirika wakati uko secondary form 1
 
Back
Top Bottom