Msaada jinsi ya kuondoa tumbo la uzazi

uniquelady

JF-Expert Member
Apr 3, 2015
420
177
Habari zenu mabibi na mabwana ,kwa yeyote mwenye uzoefu jinsi ya kuondoa tumbo baada ya kujifungua naomba anielekeze ili niweze kurudia hali yangu ya kawaida .
Mchango wako ni wa muhimu sana ,karibuni
 
Watalamu njooni tumsaidie mwenzetu. But wazo langu ingia kwenye mtandao uliza utapata majibu na ukiyafuata yatakusaidia.
 
Habari zenu mabibi na mabwana ,kwa yeyote mwenye uzoefu jinsi ya kuondoa tumbo baada ya kujifungua naomba anielekeze ili niweze kurudia hali yangu ya kawaida .
Mchango wako ni wa muhimu sana ,karibuni

Lina mda gani? Toka umejifungua na unakilo ngapi Kwa sasa ?
 
Kwa njia za asili bibi zetu waliwafunga mama zetu kanga au kaniki kwa muda maalumu mpaka tumbo lirudi mahala pake, lakini kwa sasa kulingana na maendeleo ya sayansi na teknolojia kuna belt za mtumba na za dukani kwa shilingi elfu arobaini tu, unatumia ndani ya wiki mbili tu!
 
Kula kiasi, maji ya kutosha, pia ukikamilisha wiki 8 Fanya na mazoezi
 
Habari zenu mabibi na mabwana ,kwa yeyote mwenye uzoefu jinsi ya kuondoa tumbo baada ya kujifungua naomba anielekeze ili niweze kurudia hali yangu ya kawaida .
Mchango wako ni wa muhimu sana ,karibuni
Acha kula kula nyingi. Jibane na hasa visusio, mikia, vyuku na mabia
 
Sh.ngapi? Haina side effects kuhusu kuzaa baadae?kama ushatumia dada
sijui kama kuna side effect kuna belt original kuanzia laki na nusu mpaka mingine wanauza 40 ambayo siyo original ,, ingia Instagram utaona matangazo
 
Funga kanga kutokea chini unakua kama unalipandisha Kila unapotoka kuoga
Pia usile viporo kwa mda huo pata supu ya Moto sana ndani ya mwezi 1 tu

Ila kama ulipasuliwa usifunge jitahidi kubalance kula unywe maji mengi pia
 
Nakaribia kufikisha siku arobaini ,kilo sijapima toka nijifungue

Kipindi hii umejifungua ungekua unakula healthy tu yaani supu za mboga na Samaki uji kiasi unakula Mara Kwa Mara yaani inasaidia sana kupungua na tumbo nalo litatoka sasa kama unajishindilia misosi mmh itakua kazi... Mimi mpaka natoka arubaini nilikata kg 10 tena hapo nanyonyesha mfululizo simpi kitu mtoto
 
Asante ntajaribu kufuatilia ,be blessed
Ukijifungua kwa njia ya kawaida, jitahidi ufunge tumbo kama una belt sawa ila ule muda unakaa ndani hata kanga inafaa....
Kula ndizi sana hazileti tumbo, usifukie ugali wala viporo
 
Back
Top Bottom