IZENGOB
JF-Expert Member
- Jun 28, 2014
- 323
- 317
Mimi ni mfanya biashara nina maduka mawili,duka moja nakaa mimi duka jingine nimeajiri mtu ambaye anakuwa anauza na kuniletea hesabu kila siku,nafanya hesabu kila baada ya miezi miwili,tatizo ni kwamba dogo ananiibia sana nimekuja kugundua mchezo anaoufanya ni wa aibu,anawaagiza mateja wanamletea balb na taa zingine za umeme ambavyo ni chakavu alafu anavipaki kwenye maboksi nikija kufanya hesabu nakuta kuwa hesabu iko sawa lakini mapato yanapungua na nikikaa mimi mapato yapo.
Mapato ya mwanzo alikuwa anauza mpaka 80,000 kwa siku na sasa kuporomoka mpaka 30,000 kwa siku,ukweli natafuta njia ya kuukomesha wizi huo je nifanyeje?kumtoa siwezi kwani kuna baadhi ya mambo anayoyafanya ni adimu kupata kwa mwingine,anajituma sana anafungua saa 12:30 hana Jumamosi wala Jumapili wala hajawahi kuaga kuwa anaumwa na nilifikiria kufunga CCTV camera nasikia ni gharama kubwa pia mpaka niwe karibu na ofisi ili nipate taarifa kama yupo anayejua CCTV ambazo ni Wiress anijuze,kama kuna njia nyingine nipeni nishauriwe karibuni.!