snochet,
Hakikisha vitu vifuatavyo viko vema. Ni sehemu tu ya sababu
1. Usitembee gia isyolingana na mwendo. Kila ukiona mwendo umeongezeka ongeza gia na kinyume chake
2. Usipande mlima na gia isyostahili (1 recommended but 2 kwa vijimlima) tumia akili ya kuzaliwa kujua wapi upande na nini
3. Hakikisha hausimami na breki ghafla isipokuwa imebidi. Jifunze kupunguza mwendokasi unapolelekea kusimama (decelerate). Breki za ghafla hutumia nishati ya ziada kusimama na kuibadili kuwa joto na hupoteza ile uliyotumia kukimbia.
4. Hakikisha unanunua mafuta ktk "sheli" zenye majina matukufu na sio ovyoovyo tu.
5. Kama unafanya jambo fulani zima gari usiiache ktk silent mode. Zima hata kama utatumia dakika kumi.
6. Hakikisha gari ipo vizuri: ina mafuta, oil, maji, na upepo ktk tairi wa kutosha
7. Katika safari ndefu usikimbie sana maana utakuwa unashindana na ukinzani wa upepo na hivyo kutmia nishati zaidi. Oanisha mwendo na ukinzani.
8. Kwa sababu na 7 funga vioo na utumie AC badala ya upepo. Sababu ni ukinzani wa upepo na kupoteza upendeleo wa sheria za mwendo-hewa!
..............