msaada jamani

Depretty

JF-Expert Member
Jun 14, 2013
241
225
habari...sio mara ya kwanza kupost humu jukwaani... nimehitimu kidato cha 4 mwaka 2011 kipindi hicho wazo langu lilikua kusomea kozi ya utangazaji wa radio na tv yaan kua Mwandishi wa habari ni kitu ambacho nilikipenda sana lakini baadae matokeo yalivyotoka na kutokana na kua na kipindi kile kigumu cha matokeo yaan huwa mtu unapokea ushauri wa watu bila at kujua nini mimi nataka..nikaenda kusomea kozi nyingine kabisa tofauti na kile nilichokua na kiwekea dreaming katika future yangu nasiku zimepita mengi yametokea..now natamani nirudi shule tena nirudi kusomea kile nilichokua napenda kutoka moyoni naimani sijachelewa....
nachotaka kutoka kwenu mnisaidie kunijuza ni chuo kipi kinatoa mafunzo ya uandishi wa habari na utangazaji kwa hapa dar es salaam au Songea,pamoja na ada ili niweze kujiwekea akiba na niweze kujilipia ada mwenyewe...kwan hapo nyuma nilikua nalipiwa lakin kwa sasa mambo yamebdlika watu wanafamilia zao hivyo yapaswa nihangaike mwenyewe..ili nijisomeshe...
..msaada wa mawazo yenu tafadhal naimani ntafikia lengo langu..matokeo yngu nilipata d4..yaan civics, English, Swahili, geography...
Kama ntapata wa kunifadhili ntashukuru pia
shukran
 
GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
36,887
2,000

Vyuo vya Habari vipo Mkuu ila kwa sasa hivi vingi vya hapa Dar es Salaam ni dhohofuli hali hasa Kiufundishaji.
  • A3 kilikuwa kinakuja vizuri ila sasa hivi kimeshindwa Sokoni na wameamua kufuta kabisa na Kozi yenyewe ya Uandishi wa Habari kwani wameona hailipi japo ndiyo Chuo pekee ambacho kilikuwa ni Kizuri na kina kila kitu cha kumuwezesha Mwanafunzi kusoma na kufanya Practicals za Kutukuka hadi akaiva.
  • DACICO cha Kimara sikushauri uwende labda kama unataka ukatapeliwe Kitaaluma nenda.
  • Mlimani School of Professional Studies cha Mtangazi wa Clouds 360 Hassan Ngoma kinakuja vizuri japo bado kinasuasua Kimaendeleo na pengine ndiyo maana hata Yeye kama mmiliki sasa anatangatanga tu katika Ofisi za Wenzie wakati ana yake. Pia hakina Wakufunzi Competent zaidi ya wanaobahatisha bahatisha tu na ndiyo maana hata Products zao ni ngumu mno kuzipata katika Media Outlets zilizopo nchini.
  • DSJ na TSJ ambavyo vyote viko Ilala na ndiyo Vikongwe hapo nyuma vilikuwa juu mno ila vingi vilikimbiwa na Walimu wao wa Kutukuka na Wabobezi kabisa kutokana na Management zao kujisahau ila hata hivyo kwa sasa vinarudi tena katika Chati hivyo kwa kukushauri tu anza kwanza na DSJ kisha choice yako ya pili iwe TSJ. Ni vyuo vizuri ambavyo bado vinajitambua na vinaheshimika.
  • PSJ ( Practical School of Journalism ) kilichopo Tegeta mkabala na Kituo cha Basi cha Azani cha Mwandishi wa Habari Nguli na mmoja wa Wanahisa wa Chuo cha TSJ Mzee Mshana Kiondo aliyekuwa Mhariri Mtendaji wa Magazeti ya Mzee Mengi ni chuo Kizuri kwa uwepo wa Vifaa ila kina upungufu mkubwa wa Wakufunzi na hata waliopo wanababia babia / wanabahatisha katika Ufundishaji.
Ukisikia kuna Chuo kingine kipo Dar es Salaam halafu sijakitaja hapo juu jua ni cha Magumashi / Utapeli mtupu Mkuu. Ni matumaini yangu makubwa kuwa nitakuwa nimekusaidia angalau kukupa mwangaza kidogo japo naamini Uamuzi wote upo moyoni mwako kama siyo rohoni mwako. Ungesema unataka kufanya Degree ya Mass Communication haraka haraka nisingechelewa na ningekuambia kuwa wahi kachukue Fomu yako Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine ( SAUT ) Mwanza ili upikwe na upikike hasa Kiakili, Kitaaluma na Kiueledi ili nawe uje kuwa Kipanga wa Kutukuka katika masuala mazima ya Mawasiliano na Uandishi wa Habari.

Kazi Kwako!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar threads

Top Bottom