Msaada jamani wa kimawazo na ushauri

future mind

JF-Expert Member
Dec 13, 2016
221
229
Naombeni msaada wa ushauri jamni Mimi jina langu lilikosewa wakati wakuandikishwa shule ya msingi na kwa bahati mbaya lilitumika hilo hilo hadi nilipomaliza kidato cha nne katika majina yangu matatu lilikosewa ni jina la kati "ukoo" ila majina mengine yako poa..Mimi kama mimi nimeona kutumia surname ambalo siyo sahihi yaani sio ukoo wangu halisi sio vizuri na pia sipendi nimeenda mahakani na kuapa ili kulirasimisha jina langu sahihi nakufanikiwa

>Sasa shida inakuja saivi nipo Chuo nataka niandike barua kuomba kutambulika kwa jina langu sahihi na sio linalosomeka kwenye cheti cha kidato cha nne kisheria naruhusiwa maana nina kiapo cha mahakama ila shida kubwa vyeti vyangu vyote vina hilo jina la kimakosa sasa je haitakuja kuniletea shida zaidi baadaye ya kuonekana utofauti wa majina kwenye vyeti vyangu?
@ niashe nimalize masoma kwa jina hili hili au niandike barua tu nibalishiwe?
 
Ubadilishe la nn sasa acha tu ilo ilo ulilokuwa unatumia labda kama na cheti cha kuzaliwa kina jina tofauti na lililoko kwenye vyeti
 
Hpn mm nikushaur kwamba ungepeleka na hivyo vyeti vikabadilishwe na kwasababu hukufanya hivo tumia jina lako kamili ila Mara baada ya kuandika barua nenda sasa ukabadilishe
 
Ubadilishe la nn sasa acha tu ilo ilo ulilokuwa unatumia labda kama na cheti cha kuzaliwa kina jina tofauti na lililoko kwenye vyeti
Cheti cha kuzaliwa kina jina ilo ilo la kimakosa na ndio lipo pia kwenye cheti za form four
 
Mpaka unafka chuo huoni kama unatumia jina tofauti? Mm nilikosea jina primary mbona nilirekebsha hukuhuko! Sahv itakula kwako unafkr Hata baraza watabadl jna kwenye vyeti? Ukija kuwa mtumishi hewa ndo utajua sasa, hilo jna kwenye vyeti ndo lako, hilo la ukoo walijue kwenu!

Jina la ukoo linasaidia nn kwenye vyeti? Wengine wanatumia majna tofauti yote shulen sembuse ww mengne yako! Acha mbwe mbwe nakupoteza muda, SOMA.
 
Yaani jina limekosewa toka kwenye cheti cha kuzaliwa! Wewe hukujali ukaendelea tu na maisha yakasonga mbele,

Leo hii umeshafika chuo ndio unakuja kutaka kuweka jina lako sawa eti lilikosewa?!

Mkuu hebu jaribu kua muwazi nadhani kuna jambo unajaribu kulificha hapa!
 
Hpn mm nikushaur kwamba ungepeleka na hivyo vyeti vikabadilishwe na kwasababu hukufanya hivo tumia jina lako kamili ila Mara baada ya kuandika barua nenda sasa ukabadilishe
Vyeti kama cha kuzaliwa na cha kidato cha nne akibadilishiki wakishatoa wametoa
 
Kubadilisha unaruhusiwa ukipeleka kiapo cha mahakamani unaambatanisha na barua Ya maombi utakapomaliza chuo utapewa Cheti chenye jina lako sahihi ,vyeti vya zaman vinabaki hvyo hvyo
 
umeambiwa jina unalotumia linamkosi utakosa kazi? nyie ndio mnajitafutia majanga ya kuanza kufuatiliwa historia yako kipindi chenyewe cha Magu hiki unahangaika kubadili jina la kazi gani?u mwanafunzi hewa?
 
JINA halimbadili mtu mkuu we hata ukitumia hilo mbona siyo mbaya
Nahisi ulifanya mtihani aidha kwa jina la mtu au cheti chake. Cheti cha kuzaliwa kikosewe, primary, secondary, A level mpaka chuo kikuu hujashtuka tu. Cheti cha kuzaliwa naamini ulichukuliwa na wazazi wako, hawakuona haya makosa? Wewe sio wa kwanza, eleza ukweli upate haki yakk.
 
Uko sahihi, huyu jina sio lake.

Ila atupe mrejesho.
 
Back
Top Bottom