Msaada jamani juu ya tatizo hili linachanganya sana

Hellow Mkuu pole kwa kuuguza, naelewa hali mnayopitia.

Ila ningependa ueleze zaidi, Huyo mgonjwa yuko Mkoa gani?, TB ya mifupa ya wapi?
Aligundulika kwa kipimo gani?
Alikua na dalili zipi?
Hospitali gani?

Maana hiyo TB ya mifupa ni very rare labda unamaanisha TB ya Mifupa ya Uti wa mngongo ambapo mtu upooza na hushindwa kubana choo(Ndogo/kubwa).

By the way TB nje ya mapafu huwapata watu ambao kinga yao ipo chini, hilo lisipoangaliwa pia huyo Dada atabaki kudhoofu tu.

Lakini pia ni muhimu mngemkatia Bima ya afya walau ya kuweza kumudu walau huduma basics, huenda hajaweza kutana na daktari wa kumpa tiba sahihi.

Mtu ambae hawezi kusimama vizuri kwa ugonjwa wowote ule mwishoni uhitaji mazoezi Tiba(Physiotherapy) kumrudisha katika hali yake ya kawaida. Huduma hizo ni gharama kidogo.

I bet kuwa huyo mtu hakuwa na TB ya mifupa kama unavyodai bali alikua na ugonjwa unaoathiri mishipa ya fahamu, naomba uni prove wrong kwa kutoa maelezo zaidi.
 
Hawa ndio watu wanaohitaji misaada sio huyu Rebecca anatuletea watu wanaomba msaada wa kwenda kusoma uchina
 
Dada yangu alianza kuumwa mwaka 2018 mwezi 4 na alipelekwa hospitaliti mwaka huo huo mwezi wa 9 na aligundulika ana TB ya mifupa.

Kipindi hicho alikuwa hawezi hata kusimama sababu mwili ulidhoofu sana, alianza kutumia dozi takribani miez 6 - 9 hivi lakin hali yake haikuimarika sababu afya yake haikurudi mpaka mpaka sasa na pia toka mwaka 2018 bado hajaweza kusimama hata kutembea.wiki Jana hali yake ilianza kuwa mbaya.

Tafadhali, msaada wa mawazo , ushauri au hata kwa anaejua mashirika yanayoweza kutoa msaada wa matibabu kwa sababu familia ina uwezo duni na imekata tamaa.Tafadhali Tunaomba msaada wenu sana jf.Ahsanteni
Hiyo sio TB ya mifupa
Probably ana vitu Kati ya hivi
Transverse Myelitis
Multiple Sclerosis
Brain Space Occupying Lesion

Anatakiwa kufanyiwa
Brain and Spine MRI
Lumbar Puncture for CSF Analysis
 
Hiyo sio TB ya mifupa
Probably ana vitu Kati ya hivi
Transverse Myelitis
Multiple Sclerosis
Brain Space Occupying Lesion

Anatakiwa kufanyiwa
Brain and Spine MRI
Lumbar Puncture for CSF Analysis
Comments zako ni nzuri Ila zinaniacha mshangao kwa sababu, kwa uelewa wako unahisi kila mtu anaelewa lugha yako ya kitabibu, ni sawa umesoma Ila sio kila mtu anaelewa ulichosomea, kama una moyo wa kutoa msaada uwe unatoa kwa kiswahili mtu anapata mwanga kwa kile unachokusudia kusema
 
Comments zako ni nzuri Ila zinaniacha mshangao kwa sababu, kwa uelewa wako unahisi kila mtu anaelewa lugha yako ya kitabibu, ni sawa umesoma Ila sio kila mtu anaelewa ulichosomea, kama una moyo wa kutoa msaada uwe unatoa kwa kiswahili mtu anapata mwanga kwa kile unachokusudia
Noted
 
Back
Top Bottom