Msaada: Jamani jinsi ya kuandika project plan tafadhali

abou89

Member
Jan 1, 2016
18
7
Habari zenu wana jamvi
Naomba kwa mtu mwenye uelewa mzuri sana wa jinsi ya kuandaa PROJECT PLAN anisaidie.nikipata hints inatakiwa iwe na vitu gani na vitu gani na katika kila hivyo vitu kunashauriwa kuwe vipi itakuwa msaada mkubwa sana wadau
Nawasilisha Asante
 
Andaa Milioni Mbili watu tukudraftie kitu cha uhakika
if you are good at something never do it for free
 
Project plan inategemea na aina ya biashara na mlengwa. Je unataka plan ya kuombea mkopo au unataka plan kwa ajili ya mkandarasi au mtekelezaji wa mradi?
 
Ni PM nikusaidie kwa gharama kidogo

Andaa Milioni Mbili watu tukudraftie kitu cha uhakika
if you are good at something never do it for free
Wakuu!

Mleta mada amesema anaomba msaada ! Anaomba hits kuwa project plan iwe na vitu gani na haiweke vipi....

Sasa na sisi wanajamvi wengine tunataka tupate knowledge ! Hivyo kwa heshima kabisa tunaomba mfunguke hapa hapa....

Don't charge us please...
 
Hebu google sample kibaao. Usipende msaada wa hivyo. Somaaaa. Usiombe samaki omba kufundishwa kuvua
 
Wakuu!

Mleta mada amesema anaomba msaada ! Anaomba hits kuwa project plan iwe na vitu gani na haiweke vipi....

Sasa na sisi wanajamvi wengine tunataka tupate knowledge ! Hivyo kwa heshima kabisa tunaomba mfunguke hapa hapa....

Don't charge us please...
Vyovyote vile ni elimu itatolewa. TZ elimu bure ni darasa la 1-12 (Msingi na Sekondari).
 
Wakuu!

Mleta mada amesema anaomba msaada ! Anaomba hits kuwa project plan iwe na vitu gani na haiweke vipi....

Sasa na sisi wanajamvi wengine tunataka tupate knowledge ! Hivyo kwa heshima kabisa tunaomba mfunguke hapa hapa....

Don't charge us please...



unataka knowledge ya wewe kwenda kupiga hela kwa free?? over my dead body
 
Habari zenu wana jamvi
Naomba kwa mtu mwenye uelewa mzuri sana wa jinsi ya kuandaa PROJECT PLAN anisaidie.nikipata hints inatakiwa iwe na vitu gani na vitu gani na katika kila hivyo vitu kunashauriwa kuwe vipi itakuwa msaada mkubwa sana wadau
Nawasilisha Asante


Kitu cha kwanza kabisa cha kuangalia ni washindani. Je washindani wako kwenye hiyo biashara unayotaka kuifanya ni kina nani? Kujua hili tafuta wafanyabiashara wanaofanya biashara kama ya kwako na uwatembelee kama mteja na kuangalia huduma zao wanavyotoa, ubora wa bidhaa zao, bei zao na makubaliano mengine kama vile kuuza kwa mkopo, discount unaponunua kwa wingi, n.k.


Tathmini hiyo hapo juu itakuwezesha kupanga mikakati ya kuendesha biashara yako katika hali ya ushindani.



Baada ya hapo watembelee wateja wa bidhaa hiyo na waeleze nia yako ya kuanza biashara ya uzalishaji wa bidhaa wanayoitumia na uwaombe wakufahamishe ni mapungufu gani wanayoyaona kwenye huduma na bidhaa wanazotumia sasa ili uweze kuboresha kwenye biashara yako. Hii ni pamoja na bei ya bidhaa na utaratibu wa malipo, huduma baada ya kununua (After sales services), n.k.



Hapo utakuwa umepata picha ya soko unalotaka kuliingia katika pande zote mbili za soko yaani upande wa wauzaji na upande wa wanunuzi na utakuwa una picha ya kiwango cha mauzo unachoweza kukifanya kwa mwezi.



Baada ya hapo angalia mapungufu yako na uwezo wako ukilinganisha na nguvu ya soko kisha angalia fursa ulizoziona na vihatarishi ulivyoviona kwenye mazingira ya biashara husika unayotaka kuifanya (SWOT Analysis). Tathmini hii itazaa listi ya vitu unavyotakiwa kuvifanya ili uweze kushindana vyema kutokana na tathmini ya soko uliyoifanya.



Baada ya hapo fanya mchanganuo wa gharama za uwendeshaji wa biashara husika. Kwanza gharama za ufunguaji wa biashara yenyewe (Business incorporation and licensing).



Kisha gharama za Fixed Assets na Current Assets zinazohitajika kuendesha biashara husika; pamoja na gharama za uendeshaji wa kila siku wa biashara husika. Fixed Assets ni assets zinazodumu kwa mda mrefu na gharama yake inasambazwa kwenye gharama ya biashara yako kila mwezi kwa kipindi cha zaidi ya mwaka mmoja au zaidi ya kipindi cha mzunguko mmoja wa biashara yako (business cycle) kama kipindi cha mzunguko mmoja wa biashara yako unazidi mwaka mmoja. Mfano jengo la biashara (kama utajenga jengo lako mwenyewe badala ya kukodisha), mashine za uzalishaji, magari kwa ajili ya staff au kwa ajili ya kubeba malighafi na bidhaa za biashara yako, viti, meza, komputer, n.k.


Kisha angalia gharama ghafi (Production Expenses) zinazohitajika kuendeshea biashara kama vile kodi ya jingo la uzalishaji, malighafi, wafanyakazi wanaohusika na uzalishaji, umeme, maji safi na maji taka yanayohusika na uzalishaji, usafiri, mawasiliano n.k. vinavyohusika moja kwa moja na gharama za uzalishaji


Kisha angalia gharama za kuendesha biashara kila siku (Operating expenses). Hizi ni kama mishahara ya wafanyakazi wasiohusika na uzalishaji, kodi ya jengo lisilo la uzalishaji, umeme, maji safi na maji taka yasio ya uzalishaji, usafiri, mawasiliano, n.k. visivyohusika moja kwa moja na shughuli za uzalishaji.



Baada ya hapo utatengeza mchanganuo wa mahesabu utakaochanganua matarajio ya mauzo dhidi ya gharama za uendeshaji na kuona kama biashara itapata faida au la.


Kama faida haitapatikana, utaangalia ni maeneo gani unaweza kupunguza gharama bila kuathiri ufanisi wa biashara yako ili biashara iweze kutengeneza faida. Ikishindikana basi achana na biashara hiyo tafuta nyingine.


Kama faida itapatikana basi utaendelea hatua ya kuangalia ukwasi wa biashara yako (Cash Flow) umekaa vipi?



Ukwasi wa mda mfupi utapunguzwa na mikopo (credit sales) unayoitoa, malipo ya advance (kama vile pre-paid insurance) unayoyafanya, bidhaa ulizonazo kwenye stock yako ambazo hazijauzwa, n.k.



Ukwasi wa mda mfupi utaongezwa na advances ulizopata (mfano mikopo uliyopata kutoka kwa suppliers wako – credit purchases), malipo uliyoyachelewesha kuyalipa bila kuvunja mkataba kwa mfano malipo ya kodi mbalimbali ambazo mda wa kisheria wa kuyalipa malipo hayo haujaisha, malipo ya advances yaliyolipwa na wateja wako kabla hawajachukua bidhaa kutoka kwako, n.k.



Ukwasi wa mda mrefu utaongezeka kutategemea na mtaji wa pesa na vitu utakavyoanzia biashara yako (mfano kama una jengo tayari la biashara).



Ukwasi wa mda mrefu utapunguzwa na manunuzi ya Fixed Assets zinazohitajika kuendeshea biashara husika.



Baada ya tathmini hiyo hapo juu ya ukwasi, utakuwa kwenye nafasi ya kujua kama mtaji wako uliokuwa nao unatosheleza kuanza biashara husika au la. Kama mtaji hautoshi, utaangalia uwezekano wa kufanya yafuatayo:


· Kuongeza mtaji kama utaweza

· Kupunguza ukubwa wa biashara unayotaka kuianza kwa kupunguza matarajio ya mauzo na hivyo kupunguza fixed assets pamoja na gharama za uendeshaji wa biashara husika;

· Kuomba mkopo wa mda mfupi (Short term loan au Overdraft kutegemea na kipindi cha upungufu wa ukwasi) benki ili kuziba pengo la ukwasi katika kipindi au vipindi ambapo matarajio ya mapato ni madogo kuliko matarajio ya matumizi

· Kuomba mkopo wa mda mrefu kwa ajili ya kuziba pengo la upungufu wa ukwasi katika kugharamia gharama za mda mrefu (Fixed Assets) au gharama zingine zisizo fixed assets lakini zinahitaji mda mrefu (zaidi ya mwaka mmoja au kipindi cha mzunguko wa biashara) au zote kwa pamoja.
 
Back
Top Bottom