Msaada jamani: je ni sawa?


kaka, una jambo lolote umeamua kulifanya? ​
 
Ni mtazamo wangu; alikupenda kwasababu ya pesa zako sasa zimepotea anaona humfai tena jipange upya usimtegemee sana
 
kaka, una jambo lolote umeamua kulifanya? ​

kwa kweli bado sijaamua hasa ukizingatia ndoa zetu za kiktisto!! Tulishafika mpaka kwa mchungaji lakini haonyeshi kubadilka!
 
Ushauri wa bure: akunyimae kunde akupunguzia mananihii.

kuliko akupitishe kila mahali kukuchoresha, bora ni mstaarabu walau kiduchu, anakukalisha nyumbani. Fanya hivi, tafuta mpango mkae pamoja. Utazijua mbivu, mbichi na zilizooza.
 
Mh! miezi 6 ya ndoa keshajuta kuolewa? Basi labda alikuwa anataka ndoa na si wewe kwa hiyo mawazo yake yalikuwa kwenye ndoa bila kujali nani anamuoa; sasa matarajio yake yameenda kinyume baada ya kuanza kuishi uhalisia. Dalili ndo kama hizo za kukuambia ubadili mitindo ya nguo n.k. Ukiona mwaka wa kwanza kwenye ndoa unakuwa mgumu basi ujue hiyo ndoa ilijengwa kwenye msingi mbovu, vinginevyo mwaka wa kwanza unatarajiwa kuwa wa asali kama mlijenga ndoa yenu kwenye msingi imara. Mapenzi peke yake hata yawe yale ya kuonana kwenye glasi hayatoshi kujenga uhusiano imara. Mahusiano mengi tu yanavunjika watu wakiwa bado wanapendana. Sasa kwenu kuna moja kati ya haya mawili: 1). Umechagua mke sahihi na mkeo kachagua mume sahihi ila hampendani kiusahihi kwa maana kwamba jinsi yenu ya kuwasiliana haiko sawa, wote hamjui namna ya kuwekana karibu au mmoja anajua, mwingine hataki, hamsemi wazi mnachokitaka matokeo yake mnahisi hamtakani, mmoja wenu, hasa mkeo haupi uhusiano uzito unaotakiwa. 2) Uko na mtu asiye sahihi kwako:-jinsi yenu ya kupenda na mtindo wa maisha havifanani, itikadi zenu haziendani kwa kiasi kikubwa n.k.

Umbali mara nyingi unaleta matatizo pale wahusika wanapokuwa mbali mbali halafu wakaja kuoana na kuishi pamoja. Hapa kila mmoja anaanza kuzijua rangi za mwenzie maana zamani walikuwa wakitemebeleana wanaonyeshana mazuri tu, lakini kwa hawa waliotengana baada ya ndoa tena kidogo tu maana simu zipo na wanatembeleana umbali ulitarajiwa uwe kiungo cha mahaba. Kumisiana kutamu jameni. Sasa si vizuri kukimbilia kuhisi anachepuka ingawa uwezekano upo. Nenda mdogo mdogo baba ujue tatizo nini. Ukishalijua lipime, kama linarekebishika hewala, kama halirekebishiki basi kila mmoja akae mkoa wake kivyake vyake atafute wa kufanana nae. Hukufunga ndoa na wakati, ulifunga na mtu. Yale mambo ya milele mimi nayaheshimu sana lakini huwa tunatamka kwa imani bila kujua kesho italeta nini.
 

siyo miezi 6 ni mwaka na miezi 6, mwanzo wa ndoa nilidhani ni mimba lakini baada ya kujifungua bado yuko hivyo hivyo..! Kununa umekuwa ni ugonjwa wake, hata liwe jambo la utani tu!!
 
siyo miezi 6 ni mwaka na miezi 6, mwanzo wa ndoa nilidhani ni mimba lakini baada ya kujifungua bado yuko hivyo hivyo..! Kununa umekuwa ni ugonjwa wake, hata liwe jambo la utani tu!!

ok. Ni kosa la kiuandishi kaka ila mengine niliyoaandika hayajabadilika kutokana na kosa hilo. Kama shida ni kununa tafuta jinsi ya kumfanya aongee ili mfikie muafaka nyie wawili kama hata wachungaji wameshindwa. Na kama wachungaji wenu wamejaribu wameshindwa, basi peaneni breki kidogo hata ya miezi miwili mtafakari kila mmoja kwa nafasi. Duh! sasa hiyo breki sijui mnapeana vipi wakati tayari mnaishi mbali mbali. Basi nenda au umpigie simu umpe pendekezo la kupeana muda wa kutafakari - yaani msitembeleane na upunguze simu. Wakati mwingine labda anajihisi kushinikizwa kila unapomuuliza tatizo nini.
 
Lkn awe na kifua, usijemsababishia stroke akaacha wenzake wanafaidi
 
Nyumba hujengwa kwa mapenzi na sio cheti cha ndoa. Inaonyesha mkeo hana mapenzi tena na hii ndoa. Nadhani chanzo ni umbali ambao umekuwepo kati yenu kwa muda mrefu, hali iliyompelekea kujenga mazingira mapya, na pengine penzi jipya pia, kiasi cha pengo lako kuzibwa kabisa.

Mwenendo wake na maneno yake yanaashiria hivyo. Wewe bado ni kijana mdogo, hoja ni je, kama hatajirekebisha utaweza kuhimili suluba hii kwa umri wako uliosalia? Huoni kwamba mwishowe itakupelekea kutoka nje kutafuta unachokikosa? Na kama ulivyosema, ndoa yako ni ya kanisani, ikishindikana kabisa utafanyaje? Tutakupa ushauri mwingi lakini uamuzi wa mwisho ni wako mwenyewe.

Kaa naye umpe hali halisi akupe msimamo wake kuhusu ndoa yenu. Kama haeleweki bado ni mapema, usiharibu umri wako uliosalia. Mapenzi yako peke yako hayatoshi kudumisha ndoa. Ndoa ni hesabu nyepesi: 50+50=100. 50 yako pekee haikamilishi 100!

Ukiona haeleweki mpe muda wa kutafakari, hata miezi sita; ikishindikana chukua maamuzi magumu. Nakushauri hivi lakini hayo 'magumu' mwenyewe sijui ni yapi ila uamue hatima ya mustakbali wako bila kuathiriwa na maoni ya yeyote. Pole sana mkuu!
 
Lkn awe na kifua, usijemsababishia stroke akaacha wenzake wanafaidi
ha ha mkuu bora ukathibitisha na kujua kuwa unasalitiwa,na kuchukua hatua KULIKO kuhisi unamegewa,utakonda bila ugonjwa mwilin.MAPENZI NI UGONJWA HATARI TENA HAUNA TIBA WALA DAKTARI.
 
ha ha mkuu bora ukathibitisha na kujua kuwa unasalitiwa,na kuchukua hatua KULIKO kuhisi unamegewa,utakonda bila ugonjwa mwilin.MAPENZI NI UGONJWA HATARI TENA HAUNA TIBA WALA DAKTARI.

Mkuu, hii ni ndoa. Akishajua kuwa anasalitiwa atafanyaje? Matarajio ya ndoa ni kuishi pamoja umri wote. Ndoa ya miezi 18 ikiingia usaliti na mapenzi kuisha kiasi hicho, utarajie nini? Atajafanya kitu aishie lupango umri wake wote uliosalia!

Kijana mdogo, umri mdogo, bado ana future kubwa mbele. Busara kubwa kabisa ni kukubali maji yamemwagika yanapokuwa yamemwagika.

Sisemi avunje ndoa, la; ila awe makini. Ndoa ni ya kanisani haivunjiki, lakini kama mwanamke atasimamia msimamo huo huo afanyeje? Mwishowe atamchanganya vibaya huyu bwana na matokeo itakuwa kuwindana kila siku.

Muhimu tutarajie muafaka kwa vile ndoa hii bado changa, lakini bado hatujajua chanzo cha mkewe kubadilika hivi. Huyu bwana awe mpole bado, aongee na mkewe kwa busara na upole ili kama itashindikana asijelaumiwa kwa maamuzi yoyote yatakayotokea mbeleni.
 
Nina wasiwasi huko aliko katangaza hajaolewa
 
Nina wasiwasi huko aliko katangaza hajaolewa

Mkuu inawezekana kabisa, na naona kama kuna kitu kavumbua huko aliko kutokana na kukaa mbali na mumewe, kitu ambacho hakuwahi kupata kwa mumewe tangu aolewe.

Bro, kuna watu wanajua kuchanganya watu! Na akijisahau akaachika tu, huyo mshenzi naye anaingia mitini mazima! Majuto mjukuu!
 
kumpenda nampenda ila yeye nitatizo sasa! Maamuzi bado kwa kweli...

Kumbuka; hakuna kanuni kwamba ni lazima fulani awe mkeo, mwanamke yeyote anaweza kuwa mke kwako na wanawake wako wengi. Pia si lazima fulani awe mume kwa mwanamke fulani, mwanamume yeyote anaweza kuwa mume, na wanaume wako wengi.

Hii yote hutegemea maelewano na maafikiano tu; usishikilie sana kamba inayokatika, utaangukia ndani ya shimo!
 
inavyoonekana we ndo ulitaka ndoa sana na wala si yeye umbali si kigezo mimi niko dar kazini my husband yupo mkoa na ni mfanyabiashara na sijawahi kumfanyia huo upuuzi anaofanya huyo dada Mungu ndo shahir yake.Kaka hapo hupendwi uliingia choo kibovu huyo we
an mtu na alijua akiwa na mfanyabiashara kawin na anakusaidia mana hana jinsi ila utajuta.Hv nimnunie mme wangu for 3 days kweli sidhani km kafundwa huyoo..afu hata kutoka na wewe hataki jamani...!
 
siyo miezi 6 ni mwaka na miezi 6, mwanzo wa ndoa nilidhani ni mimba lakini baada ya kujifungua bado yuko hivyo hivyo..! Kununa umekuwa ni ugonjwa wake, hata liwe jambo la utani tu!!

Hakutaki na amekuchoka huyo mwanamke...ngoja nikupe kasiri cha baadhi ya wanawake tulivyo na haswa ukimchoka mwanaume au humtaki

1. Kununa hakawii ,usimatanie kanuna au kakasirika

2. Hataki kusemeshwa mara kwa mara anaona una mghasi

3. Kosa dogo kwake kubwa hata kama ukikosea ww mwanaume ndio uombe msamaha

4. Kila mara atakutoa kasoro ,mara hujui kuvaa, mara unaongeaje siku hizi? Unatembeaje wewe? Yaani full kasoro

5. Atakuomba kitu cha gharama ili ukishindwa tu kutimiza atakununia mpka utaomba po!

6. Ukiomba penzi utajibiwa leo sijisikii tena kwa uso ulio kunjwa mpk ubembeleze sanaa

7. Kila mkigombana haachi kujuta kwa nini uko nawe na kujiuliza sijuhi nimekukubalia nini wewe na msinyooo

Mkuu hizo ni baadhi tu kama anayo haya jua una kazi ya ziada

From my own experience
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…