Msaada: Ipad2 3G - Kununua kifurushi cha Internet

Msaada: Ipad2 3G - Kununua kifurushi cha Internet

Mchana

Senior Member
Joined
Sep 27, 2007
Posts
183
Reaction score
16
Wakuu ninayo Ipad2 3G ,inatumia line ya Airtel Microsim card. Microsim yenyewe ni simcard ya kawaida ambayo imekatwa kuipunguza,,kwani wao hawana sim card hizi ndogo. Tatizo ni kuwa ipad haina function ya simu ili niongeze salio na kununua kifurushi cha internet let say 400MB. Kabla sijaikata na kuiweka kwenye Ipad ilikuwa inatumika kwenye simu ya kawaida ambapo nilikuwa nimenunua kifurushi cha internet. Hivi sas kifurushi kimekwisha na siwezikuirudisha line kwenye simu ya zamani kwani imeshakatwa na haitakaa tena simu ya kawaida. Je wataalamu, ikiwa ni pamoja na watu wa Airtel humu jamvini mnanishaurije? Naomba msaada!
 
mtaalam vp ukitumia super glue kuuuunganisha kipande ili iwe na size unayotaka ?
 
Ni kweli tatizo Hilo lipo na makampuni ya simu yatafute njia ya kutuwezesha kupata huduma hii
 
transfer credit kutoka simu nyingine. yaani tafuta Airtel nyingine na ujirushie kwenye hiyo line nyingine
 
transfer credit kutoka simu nyingine. yaani tafuta Airtel nyingine na ujirushie kwenye hiyo line nyingine
Tatizo linabaki palepale mkuu, jee nitanunuaje bundle la internet?
 
Nina mapendekezo matatu:-
1. Tafuta kitu kinachoitwa Microsim adapter ambacho ni kifaa unaweka microsim yako na unakuwa ni size ya sim card ya kawaida. Inapatikana kwenye ebay kwa bei poa tu. Kwa hiyo utaweza kuitumia sim card yako kwenye simu kama kawaida

2. Nunua iPhone 4 ambayo hayo inatumia microsim. kwa hiyo utakuwa unahamisha microsim kwenye iPhone kila unapotaka kuweka kifurushi.

3. Sali, mpaka Mungu akubali ombi lako la Airtel kuwa na huduma muafaka ya kuweka kifurushi kwenye iPad au tablet kwa ujumla.

La tatu ni bora zaidi lakini pia ni gumu zaidi.
 
Ni pm namba yako hiyo uliyoikata kama bado hujapata msaada,kama unataka kifurushi cha 400mb basi hakikisha una zaidi ya 2500 (tuseme) 3000 japo utakatwa 2500...fanya hivyo mkuu
 
Back
Top Bottom