mkuu hili tatizo lipo sana simu za Tecno na ndugu zake, sina uhakika sana ni nini, ila ninavyohisi ni kwamba Tecno wanataka kukufanyia kila kitu kwenye simu yako mwisho wa siku apps zinakosa permission na yanatokea mambo kama hayo.
hapo itakuwa playstore haina access na storage ndio maana haizioni hizo gb 14, hebu jaribu kwenda setting then apps (application au application manager) then itafute playstore au play service then nenda permission angalia kama inaweza kuandika na kufuta kwenye storage.
au cheki ile app yao inayokuja na simu kama hi manager (sijui kwenye infinix kama ipo) angalia kama kuna permission kule