Msaada: Imeletwa barua ya posa huku walishatiana mimba, nichukue hatua gani?

Ngaliba Dume

JF-Expert Member
Oct 6, 2010
1,710
3,669
Wakuu ukubwa ndio umeshaingia.Tusaidiane maana najua hakuna jambo linaloweza kushindikana humu ndani.

Hapa imeletwa barua juu ya meza, kijana kaleta barua ya posa, lakini barua inakuja wakati washamtia mimba binti. Sasa mimi kama Anko mkubwa nimepewa jukumu la kuikabili hii barua ya posa.

Naomba kuuliza wakuu...
1)Hivi ni hatua gani zinachukuliwa ukiletewa barua ya posa ukizingatia mimi ndio kama mzazi?

2)Hivi ni hatua gani za kufuata pale ambapo posa inaletwa wakati washatiana mimba?

3)Nini nashauriwa kufanya ili kupeleka mambo katika mtiririko sahihi?
 
Hili swala ungeuliza wazee wakwenu, kila jamii ina taratibu zake, mpare anataratibu zake, msukuma ana zake, mtu wa kwenu ndio anaweza kukupa jibu vizuri
Kweli kabisa. Lakini wengine wanapigisha faini kwa huko kumimbana
 
Ni sawa kabisa, now una uhakika wa kupata mjukuu

Kwa sasa ni mimba posa baadae
 
Unashindwa kuamuwa hata hilo?

Kwanza inafaa ifahamike wazi je binti yupo tayari kuolewa?

Pili je kijana anayemuowa anaweza kutunza familia anayotaka kuanzisha?

Ukishapata jibu ya hayo maswali machache endelea na mipango inayofuata
 
Chukua pesa wabebe mzigo wao wakaangaike nao hilo swala lisikusumbue kichwa kama mtu wa enzi za nyerere fanya mambo magum kuwa rahisi kwa sababu huna kingine cha kufanya ila kama utang'ang'ania ni wewe na usipo angalia ataa mimba ya pili itakuja uko nae apo apo kama utabaki nae
Note:think twice
 
Asipokusikia ajue kala hasara.
 
Wakuu ukubwa ndio umeshaingia.Tusaidiane maana najua hakuna jambo linaloweza kushindikana humu ndani.

Hapa imeletwa barua juu ya meza,kijana kaleta barua ya posa,lkn barua inakuja wakati washamtia mimba binti.Sasa mimi kama Anko mkubwa nimepewa jukumu la kuikabili hii barua ya posa.

Naomba kuuliza wakuu...
1)Hivi ni hatua gani zinachukuliwa ukiletewa barua ya posa ukizingatia mimi ndio kama mzazi?

2)Hivi ni hatua gani za kufuata pale ambapo posa inaletwa wakati washamimbana?

3)Nini nashauliwa kufanya ili kupeleka mambo katika mtiririko sahihi?
Ukizingatia kama mzazi vip wakati wewe ni mjomba?
 
Mkuu chukua Posa, panga mahari kidogo na kambuzi ka faini km 50000/=
Halafu wabebane wakaleane hukooo!!!
 
Kwanza mshukru kijana kajitokeza kutoa posa ili amuoe. Hii itamfanya asihangaike na wachumba hapo baadae maana atakuwa tayari kashazaa. Hivo possibility ya kujaza watoto wengine akiwa nyumbani ni kubwa. Kikubwa ipokee barua. Baada ya kuipokea barua wasiliana na wazee wa kwenu. Hii INA maana kwamba kama wewe ni mhehe,msukuma,mchaga,kuna hatua za kufuata ili kumwajibisha kijana na wakati huo huo hauathiri makubaliano kati ya huyo binti yako na mmewe mtarajiwa.
 
Yaani wewe umeheshimiwa sana na huyo kijana kwakuleta hiyo posa kwani kwa sasa posa zimekuwa adim sana njia inayotumika sasa nikumimbana halafu utasikia ngoja tukajaribu maisha hapo imeshatoka
 
Pokea ,fungua uisome na uijibu,ukiendelea kupoteza muda kwa kung'ang'ania hizo mila jiandae kutuongezea ma single mother alafu uje kua single babu na kupiga makelele humu,kikubwa hapo ni heshima mliyopewa baada ya vijana kuteleza
 
Wakuu ukubwa ndio umeshaingia.Tusaidiane maana najua hakuna jambo linaloweza kushindikana humu ndani.

Hapa imeletwa barua juu ya meza,kijana kaleta barua ya posa,lkn barua inakuja wakati washamtia mimba binti.Sasa mimi kama Anko mkubwa nimepewa jukumu la kuikabili hii barua ya posa.

Naomba kuuliza wakuu...
1)Hivi ni hatua gani zinachukuliwa ukiletewa barua ya posa ukizingatia mimi ndio kama mzazi?

2)Hivi ni hatua gani za kufuata pale ambapo posa inaletwa wakati washamimbana?

3)Nini nashauliwa kufanya ili kupeleka mambo katika mtiririko sahihi?
Acha mila za zamani ambazo hata ninyi hamziishi kwa sasa.
Huyo ana nia njema kabisa, hivi leo harusi zinafungwa na mimba ishakuwa kubwa kabisa.
Pokea posa cha msingi kila mwana familia apate taarifa juu ya hilo na bibi athibitishe mwenye huo ujauzito na bwana athibitishe kama ni wa kwake.
Kisha wanaweza kuandikisha walichothibitisha kwenye maandishi kwa ajili ya kumbukumbu na kutiwa saini na mashahidi kisha pokea posa.
Kama utaendekeza mila za kusikia utakuwa baba wa huyo mtoto mtarajiwa
 
Mpaka imefikia hatua ya kuleta Posa ina maana kijana kesha test kama mtoto anabeba mimba ili aje aoe, sasa hapo uncle nyie kabila lenu na mila zenu mtu akipewa mimba nje ya ndoa mnafanyaje? Ukipata majibu ndio utajibu hiyo Posa ya kijana
 
Back
Top Bottom