Msaada hivi vipele vimekuwa changamoto.

Msaada hivi vipele vimekuwa changamoto.

igihumbi

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2017
Posts
571
Reaction score
548
habari wapendwa nasumbuliwa na hivi vipele naomba msaada kwa anaejua dawa nimezunguka mahospitalini bila mafanikio.

Facebook_creation_04332EB1-2EF9-492F-B56A-3DEBF0C6FEDD.jpeg
 
Huu ni ugonjwa wa ngozi Hidradenitis,

Mara nyingi husababishwa na issue ya immune system dysregulation,uvutaji wa Sigara,Uzito uliopitiliza ''Obesity'' au issue ya family history,

Chakufanya sasa hivi,Kama unavuta Sigara acha,punguza uzito ''Weight loss'' tumia antibiotics na harmony therapy.

Angalizo,

Kabla ya kutumia dawa ya aina yeyote ile,pata vipimo au ushauri wa daktari,

Wajuzi wataongezea zaidi.
 
habari wapendwa nasumbuliwa na hivi vipele naomba msaada kwa anaejua dawa nimezunguka mahospitalini bila mafanikio.
Maji ya baridi sana (ukiweza lala au ingia ndani ya pipa la maji kaa humu muda hata wa dakika 30)
Sabuni yaan medicated soap yoyote
Dawa ya kutuliza maumivu especially ibuprofen utaandikiwa kunywa vidonge 2 mara 3 kwa siku, ila tafuta vile ambavyo ni vitamu km pipi ndio vizuri kumeza hauhitaji maji unamung'unya tu mdomoni bila maji unameza vingine ni vichungu km kroloqwini
Kuna lotion zipo pharmacy pia za calamite unaweza kupaka

Kunywa maji mengi yawe maji ya baridi ukiweza ya barafu yatakua mazuri zaidi sio ya moto, usitumie tena kunywa ya maji ya moto wewe ume-overheat yaan umewaka mwili wako umewaka sio kawaida

Yaan hakikisha mwili wako ngozi yako unapigwa na maji ya baridi ukiweza weka mabarafu kabisa mpaka utetemeke kaa humo hata lisaa limoja, kamwe usioge maji ya vuguvugu au maji ya moto acha kabisa

Usitumie vitu vya moto moto sijui maji ya moto, chai ya moto, kahawa ya moto, uji wa moto hata chakula usile cha moto sana kiwe kimeshapoa la sivyo utapandisha tena temperature juu na hali itaendelea kurudi, subiri hadi upone ndio utumie vitu vya moto, wewe ni moto unapoongeza moto moto unakua mkali zaidi yaani ni km unachochea moto kwa hio tumia vitu vya baridi baridi, vitu vya moto moto achana navyo kwa kipindi hiki hadi hali ikae sawa kwanza

Ngozi yako inahitaji ifyonzefyonze maji ya baridi sana ili mwili upoe ndio kupona kwako huko, usiogope kwanza ukioga maji ya baridi huwezi hisi km ni ya baridi sababu wewe ni wa Moto umewaka balaa yaan ume-overheat body temperature ipo juu muda wote unahitaji coolers ili uirudishe temperature chini ndio hivyo vilivyoziba hayo matundu ya majasho vitayeya vyenyewe

Ndani ya wiki hali inaanza kukaa sawa, issue ya huo ugonjwa ni uvutaji wa Sigara km alivyokwambia mdau hapo juu, km huwezi kuacha kuvuta punguza ila fanya nilivyokwambia utapona
 
Huu ni ugonjwa wa ngozi Hidradenitis,

Mara nyingi husababishwa na issue ya immune system dysregulation,uvutaji wa Sigara,Uzito uliopitiliza ''Obesity'' au issue ya family history,

Chakufanya sasa hivi,Kama unavuta Sigara acha,punguza uzito ''Weight loss'' tumia antibiotics na harmony therapy.

Angalizo,

Kabla ya kutumia dawa ya aina yeyote ile,pata vipimo au ushauri wa daktari,

Wajuzi wataongezea zaidi.
shukrani sana mkuu
 
Umeugua kwa muda gani? Sometimes insulin resistance, inflamation zinaleta body reaction tofauti kwa kupata magonjwa sugu. Hata ukipata dawa kama hujabadili diet unakuwa huponi .

Kama unaweza basi fanya diet moja kati ya hizi kwa siku 90 nina imani utapona au ugonjwa utapungua kwa zaidi ya 90%. Ketogenic,ketovore au carnivores diet itakusaidia.
 
Hii Hali inatokea sehemu yote ya mwili au baadhi ya sehemu?? Kama ni baadhi ni sehemu ipi hiyo? Umri wako upoje kwa Sasa?
Nijibu hapo ili nione pa kuanIa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom