Msaada, hii movie inaitwaje?

Bechede

JF-Expert Member
May 3, 2020
800
2,187
Kwema wakuu?
Nisiwachoshe, niende kwenye kiini cha uzi.

Hii movie ina nadharia ya comedy, nilipata kuiona katika moja ya channel DSTV. Lakini sikubahatika kuimalizia mpaka mwisho.

Inaanza watu wanaenda kwenye house party, sasa kuna vijana nafikiri wawili (sina uhakika), wanawahi kufika kwenye party na kumkuta huyo host wa hiyo party ameshafariki halafu haijulikani ni nani amemuua.

Kwa kuogopa jumbabovu lisije kuwaangukia, wakazuga kuwa huyo host hajafa. Kwa hiyo wakamvalisha miwani halafu wakakaa nae kama vile marehemu yupo hai

Ikitokea marehemu akiulizwa kitu na mtu, mmoja wao labda anakitikisa kichwa cha marehemu au mkono kuashiria marehemu yuko safi kumbe ashadanji kitambo. Wakawa wanazunguka tu na maiti huku waalikwa wanaamini marehemu yuko hai, mara wamempandisha boti n.k katika harakati za kumtafuta muuaji halisi ni nani?
 
Kama ni series basi tafuta kwenye torrents site, google itakusumbua utaishia kuzungushwa kwenye ads kibao.
Google nilitaka kufahamu jina specific la hiyo movie, baadae nikatafute huko youtube nione trela halafu ndio niingie huko torrents. Sasa jina nililopatiwa hapo juu sijaona movie yoyote yenye jina hilo.
 
Back
Top Bottom