Mkuu hiyo kwenye nyekundu kwa matumizi uliyotaja haiwezekani kabisaaaaaaaaaaaaaaaa! Utafikiri una kiwanda? Au nyumba ni ya wapangaji wengi na kuna wanaotumia umeme umeme kufanyia welding wakati wa mchana mkiwa kazini? Au Kuna mpangaji ana kijibwawa cha samaki (Aquarium)?. Mimi napikia umeme, nachemshia maji birika la umeme, natumia pasoi ya meme, friji iko on masaa 24, TV iko on almost masaa 16 kwa siku, taa 4 (tube light) zinawaka kuanzia saa 1 jioni mpaka saa 12 asubuhi na bill yetu kwa mwezi haizidi 50,000. Kama ni kweli na unatumia mita za Tanesco kuja kusoma kila mwezi, fanya mpango fasta ufunge LUKU.