Msaada: Gari yangu inaishiwa nguvu (vitara no made)

Ukaridayo

JF-Expert Member
Oct 8, 2012
508
470
Kwa wenye uelewa na hii ishu mana juzi nilienda nalo mahali (safari fupi hapa na pale) niliporudi nikalipaki (saa sita ya mchana) lakini jioni (kumi na mbili jioni) nikakuta na mabadiliko haya:

1. Nilipoliwasha nikaona gari ina vibrate yaani silence isiyotulia.

2. Muungurumo wa gari ni wa kwa kwa kwa kwa kwa siyo wa kutulia hauna radha, ni kama unalipuka lipuka.

3. Wakati mwingine hapo kabla nilkuwa naona gari inaishiwa nguvu(power) kwenye kilima cha kawaida sana ambacho hata mwenye byskeli anapita kwa kusimamia tu baiki yake. Hilo nalo likaanzaga kunishangaza.

4. Sasa hivi ukiliwasha then ukiweka "D" mshale wa Rpm unashuka chini sana na gari inazima hapo hapo wkt mwingine ndiyo hivyo gari inakuwa nzito kwamaana ya power.

3.gear ya reverse haina nguvu kabisa na ndiyo inayozima gari pindi ukiweka gear hiyo na hata ikirudi inarudi kwa kukanyaga sana accelerator gari inaoenekana kama nzito.

4.Accelerator naiona kama inachelewa hivi mana wkt mwingine unaweza kuwa umekanyagia hivi then effect zake zikadelay for some minute huko kwenye mwendo wa injini; ninachomaanisha pale unapokuwa umekanyaga accelerator hapo hapo(on the spot) uone mabadiliko ya kile ulichokifanya kwenye gari yako kama gari zingine ili nihisi uwepesi wa gari.

Ni hayo tu mana hii ya kwa kwa kwa kwa kwa tena gafla inanikera sana wakuu.
 
Cheki air hose kama inapitisha hewa baada ya cleaner. Air hose mara nyingi hupasuka/kukatika.
 
Anza na Air cleaner... kaipigile upepo au weka mpya... kama bado, cheki Fuel filter...badilisha nyingine na usinunue feki kwa unafuu wa gharama... ka bado angalia Plug ipi haichomi vizuri, hapo fundi anahusika... kama bado jipange kwenye Fuel pump kuipiga chini...
 
  • Thanks
Reactions: Dyf
Kama plugs zikiwa sawa tatizo linaweza kuwa ECU, niliexperience tatizo kama hilo katika Rav 4 Ya 2002 yenye engine ya D4 ambapo ukiiwasha ilikua inaanzia gia namba 3 na unakuta inakosa nguvu ya kupanda hata mguu tu wa binadamu, hali hii ilikua inatokea kunapokua na baridi au joto kali, kukiwa na moderate temperature inapiga mzigo tu, ilinilazimu kununua ECU mpya japo nilipata tabu kuipata.. Kwa vile gari yako ni vitara sina uhakika kama hii advice itaendana ila nimeshauri hivyo kwa sababu tatizo ni kama linalingana na nililowahi kulipata
 
Nitalifanyia kazi mkuu... now najichanga nikishazikamata nitaleta mrejesho hapa... thanks kwa ushauri wako.
 
Nitalifanyia kazi mkuu... now najichanga nikishazikamata nitaleta mrejesho hapa... thanks kwa ushauri wako.
mkuu achana na hilo wazo hapo juu hiyo gari haina tatizo la ECU huyo juu ya rav 4 hilo ni tatizo na ugonjwa wa kidunia na kama ww ndio mnunuaji wa kwanza unategenezewa bure na toyota.

coz nauelewa juu ya hilo 100 asilimia
 
Huyu alikua anahitaji ushauri, kwa hiyo kunarrow problem ndio maana tukampa ushauri wa possible problems...halafu watanzania wachache sana tunaonunua gari mpya kabisa (0km), hivyo hiyo ya kutengenezewa bure na toyota ngumu sana kuitumia
 
Back
Top Bottom