Frank Wanjiru
Platinum Member
- Apr 12, 2012
- 25,726
- 46,992
Kwa hilo swala lako anza kwanza kucheki Plugs kama wadau walivyoshauri hapo juu.
Yawezekana ni tatizo la ‘air intake' fanya kama nitakavyo kuambia hapa (ila hii ni gari yangu – make/ model ni tofauti na yako):
1. fungua bonnet/ hood ya gari yako halafu soma kwa ndani karibu na kwenye lock yake lazima utakuta minimum na maximum rpm (itakuwa kwa Kijapan lakini namba na neno rpm litakuwa kwa kiingereza nadhani) [kama hakuna jaribu ku-google], na huwa inaandikwa plus/ minus – mfano -/+ 700
2. kwenye engine ya gari yako tafuta vitu vifuatvyo – (a.) idle air control valve (hii inatembea automatically), (b.) idle control piston (iko kama bolt ambayo una-screw in and out - hii ni manual {hapo juu kuna watu wanaiita ‘silencer'}), na (c.) ‘valve cover air recirculation' au ‘valve cover air breather' {tafuta kwenye valve cover}
3. (a.) na (b.) [ambavyo vinakaa pamoja] zinakawaida ya kujaa carbon i.e. moshi wa gari ambao unaoshwa kwa kutumia mchanganyiko wa ‘injector cleaner' (kama huko Dar zimejaa tele pale Game – Mlimani city) na ‘petrol' {ratio sikumbuki vizuri); ukifungua (b.) wakati wa kufunga utakua unaangalia rpm mpaka ifikie ile iliyoandikwa kwenye bonnet {utafanya jambo ili wakati engine ina-run}. Kama issue ni (c.), inabidi ununue kingine kipya i.e. you replace it with the new one. Ili kujua kama (c.) hiko vizuri, kitikise kama kina ‘click' basi kiko vizuri, kama kimya basi kwisha kufa. Halafu hii kitu ni one-way.
4. Sijawahi kucheza na ‘EGR', na sijui kama gari yangu ina hiyo valve.
5. air intake ikiwa ndogo Umeme wa gari unakuwa chini, na AC inataka Umeme mwingi, hivyo AC ananyang'anyana Umeme na engine hivyo wote wanaishia kukosa na gari kuzimika; kama ukiwasha gari linawaka vizuri ujue issue ni hii nilivyoelezea hapa.
NB: mbona haya mambo yote yako kwenye mtandao – kuanzia Google – mpaka ‘YouTube'. Soma na kutazama hizi videos. Nikipeleka gari kwa fundi ujue sina vifaa au sitaki kuchafuka, au sina muda lakini sio kutegemea ‘ubongo' wake 100% kutatua tatizo la gari yangu.
https://youtu.be/9uqYTxduqio (cleaning)
https://youtu.be/GEGItKeg970 (checking)
How to Clean the Idle Air Sensor Control Motor - HowStuffWorks (cleaning)
Kwenye red siyo sahihi.Angalia na silencer kama ipo sawa, ikiwa chini ukiwasha AC lazima gari izime! Naamini haikuwahi kushushwa ili kubana matumizi ya mafuta kama wanavyofanya wengi wenye masix cylinder!!!! Mafundi watakusaidia
Kwenye red siyo sahihi.
hili ndo jibu sahihi...mkuu hapa una tatizo kwenye AC system, kwa kifupi AC compressor ikianza kufanya kazi[ukiwasha AC] inaleta mzigo mkubwa kwenye engine hivyo kwenye hali ya kawaida engine inajiongeza rpm[ mara nyingi kutoka 600/700-1000/1200 revolution per minute] ili kuipa engine nguvu zaidi ya kuhimili mzigo wa ac compressor.
inaonesha hapa gari yako haijiongezi rpm ukiwasha AC INABAKI ile ile 600/700 rpm hivyo engine kushindwa kubeba mzigo wa ziada kutoka kwa ac compressor,gari itazima. ukiwa kwenye mwendo haizimi kwasababu ukikanyaga mafuta rpm itakuwa juu ya 1500 kwa hali ya kawaida.
ninachokushauri nenda kwa mafundi wa AC waangalie system nzima kwenye gari yako,inawezekana compressor imeanza kufa au tatizo lingine kwenye idle control.