Tatizo la AC kwenye gari langu aina ya Nissan Xtrail ya 2009

matinel

Member
Dec 31, 2022
12
18
Nimebaini gari langu nikiwasha ac inaanza kutoa ubaridi kama kawaida lakin nikienda distance flani mbele ac inaanza kupoteza ubaridi labda mpaka niizime kwanza ac nakuiwasha tena ndo itaanza tena kutoa ubaridi kwahiyo inakuwa mda wote ambao inakuwa haitoi ubaridi inakuwa inapuliza feni tu.

Nilijaribu kupeleka kwa fundi mmoja yupo pale kinondoni makaburini alichofanya yeye ilikuwa kubadilisha kitu flan kipo kama aircleaner hivi aligungua upande wa dashboard anakokaa abiria na kukitoa kweli kilikuwa kimechafuka na akasema hiki ndicho kinasababisha lakin wakati tuko pale pale baada ya kureplace hicho ambacho kipo kama aircleaner akafungua boneti tukawa tunacheki pamoja jinsi compressor inavyofanya kazi tukagundua kuwa kile kinacho bana na kuachia kwenye compressor kuna wakati kinabana na kuna wakati kinachia kikiachia yani kama hakizunguki na compressor ubaridi hauji na kikibana ubaridi unakuja.

Akasema hapa itakuwa kuna shida nyingine hivyo ikawa jioni sana so nikamwambia ntakuja siku nyingine lakin nimeogopa kwenda tena kwake kwasababu naona kama anabashiri kosa badala ya kuchunguza kwa umakini na alipima gesi akasema gesi ipo ya kutosha tu

Sasa mim naombeni ushauri wenu au kama kuna sehemu naweza kupata fundi anaeleweka bila nyenje nyenje aniambie nimpelekee gari wakubwa na buttoni ya kuonesha umeswitch on ac inakuwa inaonyesha vile vile tu ila ubaridi ndo unakuta hauji
 
Mwambie apime Kwanza mfumo wote wa Ac kuanzia kwenye condenser Hadi mtungi wake pia inawezekana kuna kifaa kimekufa .... Nenda Tu kesho Kwa huyo fundi ila kuwa na karibu ili uone wewe mwenyewe
 
Back
Top Bottom