Who Cares?
JF-Expert Member
- Jul 11, 2008
- 3,507
- 3,364
kwa kweli kama doc ziko kamili sioni kwa nini utoe rushwa. Kwa sasa unajua unachotakiwa kulipa na una hiari ya kuweka pingamizi iwapo haukubaliani na hesabu ya afisa wa kodi, zamani ingekuchukua wiki nzima malalamiko yako kushughulikiwa jambo ambalo liliongeza gharama za storage.
Angalizo: Iwapo invoice value ni kubwa kuliko tra calculation, invoice value will apply.
Sasa kuwepo ama kutokuwepo kwa rushwa bandarini ni mjadala mwingine, kumbuka bandari ni taasisi tofauti na tra.
Sijui kama diy - "do it yourself" inawezekana ila nijuavyo mfumo wa sasa unakulazimisha kupitia kwa clearing agent coz ndiye mwenye leseni ya uondoshaji mizigo idara ya forodha.
Niliwahi kusikia kwamba muda nao ni pesa, kutoa gari bandarini inachukua wastani wa siku 7. Ikiwa nitafanya mwenyewe manake zaidi ya siku 7 nisimamishe ratiba zingine. I would rather pay someone for that.
Hoja yangu ilizungumzia kukopa ili kuongeza kipato/ufanisi (sio kuwa pale pale) na imekaa kijasiriamali zaidi ambapo inakosa mashiko ukiitazama kwa jicho la "ponda mali kufa kwaja"....
Mwisho wa siku kila mtu amejiwekea kanuni za kiuchumi/maisha. Kwa nini unahitaji gari ndio itakuwa sababu ya kununua gari...
umewahi kusoma/kusikia nadharia ya hierarchy of needs???
kiongozi salute..nisameehe kama nitakuwa naonyesha kiwango cha juu cha uvivu wa kumtafuta elimu...hivi hii kitu niliyobold in blue katika mada yako ndio umei-present kwa hiyo pyramid diagram hapo chini?...ni kitu gani hasa na inahusiana nini na maisha ya kila siku ya kila mwanadamu anayeishi chini ya jua?
Shukrani mbele..na kuuliza sio ujinga bali njia ya kujifunza zaidi.