MillionHairs
JF-Expert Member
- Jul 31, 2013
- 803
- 406
Rudia tu kitecno chako
Naona unatujulisha kijanja kua umehongwa cm mpya.kwanini usiwaulize dukan?na kwanini unanunua kitu bila kupeleleza?ok tumekusikia
mtu anaomba maelezo nyie mnaleta kejeli
ahsante kwa mchango wako. Kama mimi ni mtu wa kwanza kuja hapa jukwaani na kuomba msaada wa kitu fulani basi ni kweli natafuta sifa...ila kama mimi si wa kwanza basi jibu unalo. Pia hii simu sikuinunua hapa bali niliiagizia tu.
Anyways, kwa jinsi ninavyoziona trend za simu za samsung hazileti value for money.
Wao ni kama wanakurupuka kujaza soko ila hakuna kinacholeta impression yeyote.
Sijawahi itumia Note 4 kwa muda mrefu ila nilichoona haina kipya ukilinganisha na Note 3.
Ni miezi miwili sasa tangia nimeanza kutumia hii simu(Samsung Galaxy Note 4) ila bado sijaona faida yeyote kwa kutumia hii simu...maana sioni tofauti yeyote ya kimatumizi. Kama kuna mtu yeyote hapa jukwaani anaejuwa matumizi na mbwembwe zote za hii simu naomba anielekeze hapa ili iwe faida kwangu mimi na wanajamvi wengine wanaotumia simu hii.
Mfano kuna hii S Pen (kalamu ya kuandikia) kusema kweli nimejitahidi na kujaribu sana niweze kuitumia hii pen lakini nimechemsha. Sasa nimekuta najiuliza peke yangu hivi kwanini nilinunua hii simu? Maana sioni tafauti yeyote ya kimatumizi kama S4,IPhone 5 au Nokia Lumia...sasa naona inaniongezea uzito mifukoni kwangu maana hii simu ni kubwa sana na ni ndefu pia.
Nawaombeni wana jamvi kama kuna mtu atanielekeza na kuniambia jinsi ya kutumia hii simu na faida zake basi nitashukuru sana tukianzia na hii S Pen. Maana kama haina chochote cha ziada zaidi ya sifa za kuwa eti unatumia Note
4 basi kwahilo siko teyari na ni bora ni iuze na nirudi kulekule kwenye S4 yangu au IPhone.
Am done: michango yenu nyinyi ndio itakayo amua nibaki na hii simu au ni iuzilie mbali uko.
Nenda YouTube, search how to use s pen. Other features pia jinsi ya kuzitumia kwenye hio sim utaelezwa uko
pana jirani yangu ana hiyo Note 4 na alisha wahi tumia simu nyingi sana iphone, HTC, n.k. mwisho amerudi kwenye samsung galaxy Note 4, na ni duos ina line mbili,, kwa kweli anaijulia sana na kuisifu sana na mm ndio mpango nilionao kuinunua nimeipenda sana, mfano mmoja tu ni ukipewa Business Cards "unaipiga picha tu" snap shot simu yenyewe inakujazia all Information za contacts automatically kitu ambacho kilinishangaza sana hadi leo,, just 1 min jina namba za simu zote hata kama ni 4, mtaa n.k.
Ahsante sana mkuu...je hiyo Note 3 umewahi kuitumia? Na kama ni ndio...je hii S Pen inatumikaje?
Je ninaweza kumuandikia au kuchati na mtu kwa kutumia hii S Pen na yeye akapata au akasoma maandishi kama nilivyoyaandika kwa kutumia S Pen?
Nasuburia maelezo ya matumizi ya s pen,sioni mwenye kutoa jibu lenye likidhi haja.Nafikiria nitoke kwenye bb 10,nijaribu Note 3 au 4,nikishawishika
kaka note 4 ni moja kati ya simu bora kwa sasa hasa kama unataka kuwa productive. hivi ni baadhi ya vitu ambavyo unaweza fanya kwenye phablet ya samsung.
split screen au multi window
kwa sababu simu yako ina kioo kikubwa utaweza kufungua app mbili kwa mpigo huku unaziona zote. kioo kitagawanywa nusu kila app ikitumia upande wake.
-chukulia mfano unafanya mahesabu then unaweza fungua app ya kutake note na calculator then ukawa unapiga mahesabu huku majibu unaandika juu kwenye app ya note.
-au unachat na mtu huku upo jamiiforums unaperuzi habari vinaweza kufanyika kwa pamoja
na hii multi window ya note 4 inakubali kudrag picha pia kwa wale watu wa creative kama una edit picha kwenye image editor unadrag na kudrop tu.
kui enable hii feature soma maelezo haya hapa
How do I use Multi Window™ (Multitasking) Mode on Samsung Galaxy S® 4? : AT&T Cell Phones | Samsung
function za kalamu
kitu kinachotofautisha note 4 na simu za makampuni mengine ni kwamba inakuja na kalamu, hii kalamu inaongeza productivity yako. ngoja nikupe situation unazoweza kuitumia.
-kubadili mwandiko wako kuwa maneno kama yaliyoandikwa na keyboard. mfano upo darasani au kwenye kikao then unatake notes haraka haraka basi unaweza tumia kalamu kuandika na mwandiko wako mwenyewe then simu itabadilisha kama umechapwa na keyboard. kuenable hii feature fanya kama unagusa kioo na kalamu yako ila usikiguse kabisa pitishia kwa juu (hover) then utaona alama ya T inatokea iguse kuanza kutumia.
-kalamu pia hutumika kuchora au kutengeneza rough figure pamoja na kunavigate kwenye simu yako. kwa wale artist wanatoa vitu vizuri unaweza kushangaa mwenyewe
wide angle front camera
kitu chengine special kuhusu note 4 ni kwamba camera yake ya mbele inauwezo wa ku cover eneno kubwa. unaweza kuitest wewe na rafiki zako kadhaa mkapiga selfie moja utaona jinsi wote mtakavyotokea bila kukatwa.