Msaada: Fertilizer Trees or Plants.

Tundapori

JF-Expert Member
Aug 12, 2007
645
260
Zenu wakuu?

Naomba kama kuna anayefahamu namna ya kuongeza uzalishaji wa mahindi shambani kwa kutumia mbolea asili ya miti iitwayo "Fertlizer Trees" anisaidie.

Hii miti huwa inabadirisha Nitrogen iliyoko hewani kuwa Nitrates ardhini, kwa hiyo mahindi hupata hiyo mbolea ya Nitrates na kustawi vizuri.

Je, ni miti ipi hasa ambayo ipo au inatumiwa Tanzania itumikayo kama Fertilizer trees or plants.

Kwa watalaam wa kilimo naomba msaada wenu.
 
asante kwa interest katika kilimo. mimea aina ya mikunde ina sifa ya kurutubisha udongo kwa kubadili nitrojen iliyoko hewani na kuwa protein katika mmea husika. ili hiyo nitrogen iweze kupatikana kwa ajili ya mazao mengine kama mahindi, yapasa uoteshe mikunde kwanza, ikianza kutoa maua uingie ulime ili uifukie/changanye na udongo. kisha ndo upande mahindi baada ya wiki tatu. baadhi ya mimea yenye uwezo huo ni kunde, karanga, marejea, ***** na maharagwe. ni-pm kwa maelezo ya kina.

Capital
 
  • Thanks
Reactions: FJM

Kwa nini aku pm? Elimu hii ni kwa faida ya wote.
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Japokuwa sitakuwa mchoyo wa elimu, nilitaka ani-pm ili nimshauri vema kulingana na eneo alipo. kwanza nitamuuliza maswali kisha akishanijibu, nitamshauri ipasavo. bahati mbaya, mazingira ya kila mmoja wetu ni tofauti, hivyo kila muhitaji anahitaji ushauri tofauti.

Capital
 
Back
Top Bottom