Lasway.Jr
JF-Expert Member
- Jul 25, 2015
- 230
- 405
FAHAMU NJIA NZURI YA KUONDOA MAGADI(SALTS) SHAMBANI
AINA ZA MAGADI ZILIZOPO KWENYE UDONGO
Kuna aina nyingi za chumvichumvi zilizopo ardhini na huwa katika viwango tofauti kulingana eneo moja na lingine na tofauti hii husababishwa na asili ya udongo wa mahali husika chumvi hizi ni kama Sodium ambayo hupatikana kwenye chumvi ya kawaida(NaCl), Potasium, Boron,Magnesium, Calcium, Phosphorous madini mengine ni muhimu katika ukuaji wa mmea lakini kwa kiwango kinachotakiwa na huwa ni sumu endapo yatazidi kiwango chake
NAMNA AMBAVYO MAGADI HUDHOOFISHA MIMEA
Madhara yatokanayo ma magadi ni makubwa sana na huleta hasara kwa wakulima wengi sana, kitaalamu magadi huzuia mizizi ya mimea kufyonza maji kwenye udongo na kuufanya mmea kushindwa kukua kwani maji ni muhimu katika mfumo wa mimea kujitengenezea chakula chake hata kama utamwagilia maji ya kutosha katika shamba lenye magadi bado mimea haitaweza kupata maji hayo (salts induce water stress to crops through matrix forces build up between the soil particles and the salts ion and hinder plant water uptake via capillarity and osmosis). Pia magadi huharibu mfumo wa udongo(soil structure) na kuufanya udongo kuwa mgumu na kuzuia mizizi ya mmea kupenya vizuri kwenye ardhi na hivyo kupunguza udhabiti wa mimea iwapo shambani na kusababisha kuanguka angauka kwa mazao yanapofikia wakati wa kubeba matunda au maua kwani hukosa nguvu za kujishikilia kwenye ardhi na hali hii husababishwa sana uwepo na sodium nyingi shambani na mkulima hupata hasara kubwa sana.
VYANZO VYA MAGADI KWENYE UDONGO
- Asili ya udongo wenyewe
- Maji yanatumika kwa umwagiliaji
- Utumiaji wa mbolea za viwandani bila maelekezo ya kitaalamu
- Mfumo mbaya wa utoaji maji shambani(poor drainage system)
NJIA ZA KUONDOA MAGADI SHAMBANI
Hili ndilo lengo kuu la makala hii ili kumsaidia mkulima kuondokana na tatizo hili, nitaeleza njia za kitaalumu na za gharama nafuu za kuondoa na kupunguza magadi shambani.
- Kuzamisha chumvi(Leaching of salts)
2. Uwekaji wa Gypsum (Calcium Sulfate)
Gypsum hufanya kitu kinachoitwa neutralization ambapo hubadilisha chumvi iliyopo ardhini isilete madhara kwa mimea na katika maduka mengi ya pembejeo zinauzwa hizi gypsum kwa ajili ya mashamba ili kudhibiti chumvi na magadi lakini njia hii ni ya gharama kidogo
3. Utumiaji wa Samadi
Mbolea za wanyama na mimea husaidia sana kwenye kuongeza rutuba kwenye ardhi pia katika kuhakikisha na kupungiuza magadi kwenye udongo na njia hii matokeo yake ni polepole lakini ina uhakika na pia samadi ina faida nyingine nyingi katika kuimarisha udongo na kuongeza upatikanaji wa madini kwa mimea
4.Njia ya mafuriko (flooding)
Njia hii hufanywa katika maeneo yenye maji mengi na hasa kipindicha mvua , shamba lenye magadi hutifuliwa na kufurishwa au kumwagiliwa mpka maji yanatuama (wakati hamna mazao shambani) na baada ya hapo maji hutolewa kwa mifereji maalumu na maji hayo huchukua magadi katika shamba husika
NB. njia hii usiifanye kwenye mashamba yaliosongamana ili maji yaliyo na magadi yasiende kwenye shamba la jirani yako na kumpa hasara
5. Utumiaji wa njia za kisasa za kufanya umwagiliaji kama drip irrigation,sprinkler system hupunguza uwepo wa magadi kwenye udongo na kama unahitaji system hizi nitafute kwa mawasiliano mwishoni mwa makala hii
Lakini kwa maeneo ambayo yana magadi sana unashauriwa kupanda mazao yanayoshahimili ardhi yenye chumvi
mazao yanayoshahimili chumvi zabibu,mbaazi,Nanasi,Miembe hasa mazao ya miti ndio hushauriwa sana katika ardhi yenye magadi
mazao yasiostahimili udongo wenye magadi
Mahindi,Tikiti maji,Nyanya, Mbogamboga, na mengne mengi
fuata ushairi wa kitaalamu kabla ya kuanza kulima na kupanda
SOMA ZAIDI MAKALA MBALIMBALI ZA KILIMO HAPA
Eng(T) Octavian Justine Lasway
Bsc irrigation and water Resources Engineering
Sokoine University of Agriculture(SUA)
Phone. 0763347985
Email . octavianlaswai@gmail.com