Msaada dawa ya wadudu shamba la matikiti

Msaada dawa ya wadudu shamba la matikiti

popo1986

JF-Expert Member
Joined
Jul 30, 2014
Posts
1,120
Reaction score
373
Wanajamvi naomba msaada nimepanda juzi matikiti na Leo yameanza kuchipua naomba msaada wa Dawa gani bora ya wadudu na hatua gani muhimu za kufuata katika Dawa binafsi sijui ila nafanikiwa mpaka sasa kwa msaada wa humu jamvini kwani nimekuwa nikifuata ushauri wenu humu na mpaka sasa miche imechipua sasa narudi tena kuuliza ni Dawa gani nzuri kwa wadudu au kwa hatua hii nifanye nini?
Karibuni maana nimeambiwa Dawa lazima japokuwa bado niche haijaanza kuliwa na wadudu
 
Tafuta DAWA ZA WADUDU-Kwa majina ya kibiashara huitwa- dudu all au Blast au Buffalo

Utakuwa ukipiga mls 20 kwa maji lita 15 kila baada ya siku 14.

Jitahidi upate na dawa za ukungu kama Power 78WP, au ebony 72 WP utakuwa ukimix ndani ya hizo dawa za wadudu

Baada ya siku 14 itabidi uweke mbolea za kukuzia kama CAN gram 5 kwa kila shimo kama ni mche mmoja, kama ni miche miwili kwa shimo ni gram 10, KIPIMO gram 5 ni sawa na kijiko kidogo cha chai, Gram 10= Kijiko kikubwa cha wali.

Baada ya siku 30 tangu tikiti zilipoota zitaanza kutoa maua, jiandae na kupiga booster starter booster kama Polyfeed starter au Super grow

Siku 14 baada ya siku hizo 30 matunda yataanza, anza kupiga finisher booster, kama vile Multi K, Wuxal Macro mix, au Potphos hizo utaendelea nazo unapiga kila baada ya siku 14 mpaka unavuna

Wakati wa maua na matunda usije kutumia dawa dume/dimethoate au Karate hizi dawa ni sumu kali daraja la pili, angalia makopo yake karibu na kitako cha kopo kuna ufito wa rangi ya njano

CHUKUA MUDA.. SOMA HUU UZI Je, unataka kulima mazao ya mbogamboga na matunda lakini unakosa maarifa sahihi?? Karibu tushauriane UNAMAJIBU MENGI SANA YA MAMBO UTAKAYOKUTANA NAYO SHAMBANI-TIKITI

KILA LAKHERI

Back
Top Bottom