Karibu Kaka. Wakati ukisubiri Wataalamu wakushushie vitu, pata machache mepesi kutoka kwangu:
1. Elimu Haina Mwisho. Hata ungekuwa na Umri wa Miaka 65, ruksa kuingia Shule kusoma
2. Elimu ni Ufunguo wa Maisha. Elimu itakuwezesha kuyaona mambo kwa upana wake
3. Mwajiri mzuri na ajira nzuri ni wewe mwenyewe na Mradi/Biashara yako uliojiajiri. Usione watu wamevaa nadhifu wakiendea kwenye ajira za kuajiriwa, ni watumwa wa mishahara ya mwisho wa mwezi, wengine ni wadokozi, wala rushwa, wabadhirifu wa Mali ya Mwajiri, madeni mpaka shingoni, n.k. Huenda uko vizuri kuliko wengi wao! Ukijipanga vizuri ukafanikiwa, wewe ndio utakuja kuwaajiri Wahasibu, Wanasheria, Maofisa Ugavi, n.k.
4. Katika Kozi ulizotaja hapo juu, ninaipigia upatu Business Admin., pamoja na sifa nyingine, ni "Kozi Malaya". Soma ujiajiri ili uajiri na sio uajiriwe!
Wakongwe wanakuja kukudadavulia ma-vituz!
kwanini usianze na Kozi ya Ujasiriamali, nadhani unaweza anza soma hata kwa level ya diploma, then ukaanza hiyo Business admin Baadae
Kwa kufanya hivyo utaimarisha kilimo/biashara zako na utakuwa unafanya kwa ustadi zaidi....hiyo BA unaweza soma hata kwa Masafa....namaanisha Open and distance learning ukifanya hivyo biahsra zako hazitaathirika hata kidogo
all the best
Asante sana ndugu yangu,huu kwa kweli ni ushauri mzuri sana,hata mimi wazo langu ni kufanya open kwa level ya degree!ila mkuu mimi sivifahamu vyuo vinavyotoa kozi ya ujasiriamali kwa level ya diploma,je unaweza kunisaidia mkuu,either kiwe Morogoro au Dar es salaam!asante sana
Ujasiriamali....nakushauri kama utaweza UDBS- Chuo kikuu cha dar es salaam shule ya Biashara wana DIPLOMA ya Ujasiriamali pamoja na MA- ya ujasiriamali........cha msingi tembelea website yao ikiwezekana waandikie/wapigie/au watembelee kabisa.....Naamini itakusaidia kupanua mawazo yako na mwisho wa siku utafanya biahsara yakoi vizuri
Kila la kheri
Leo hata mimi nimefaidika, wakubwa mmetoa somo zuri sana, hata kwangu nimepata elimu zaidi. namshukuru mleta mada na wachamgiaji pia.
Mkuu kwanza karibu sana, Naomba nitietie nyama kwenye swala la kozi ipi ya kusoma,nafkiri pale Mzumbe kuna kozi inaitwa BBA in Enterpreneurship hii itakufaa sana mkuu
Leo hata mimi nimefaidika, wakubwa mmetoa somo zuri sana, hata kwangu nimepata elimu zaidi. namshukuru mleta mada na wachamgiaji pia.
Mkuu wanasema ukitupa mada yako jamiiforum wengi wataondoka na kitu kipya kichwani..
Kwa wale waliosoma mpaka degree moja au mbili na kisha kuanza kazi kwa maana ya kuajiriwa, wengi pamoja na uwezo wao wa kujimudu kimaisha hawafurahii sana kuwa waajiriwa.....
wengi wanatafuta namna kila leo za kuwa wafanya biashara, wajasiriamali au waajiri...lakini uoga mwingi na uzoefu kidogo pamoja na muda hafifu huwafanya kufeli kabla hata ya kuanza.....
Kwako...kwakuwa umeshaanza katika upande huo wa maisha (i.e kujiajiri) nakushauri soma kozi za biashara kwa minajili ya kupanua ufahamu na kuongeza ufanisi katika biashara zako, usifikirie kabisa kuajiriwa kwani pia kuna vikwazo chungu tele ambao wahitimu wa vyuo wanakutana navyo kupata ajira, na hata wakizipata bado sio suluhisho la hali duni ya maisha.....
kwa hivyo soma kozi ya biashara lakini ukiwa na mentality ya kupanuka kimawazo na kiundeshaji ili uwe mfanyabiashara wa level za kina mzee 'More' huko mbeleni...
oh asante sana hata mimi ngoja nijipange niongeze ujuzi japo diploma tuUjasiriamali....nakushauri kama utaweza UDBS- Chuo kikuu cha dar es salaam shule ya Biashara wana DIPLOMA ya Ujasiriamali pamoja na MA- ya ujasiriamali........cha msingi tembelea website yao ikiwezekana waandikie/wapigie/au watembelee kabisa.....Naamini itakusaidia kupanua mawazo yako na mwisho wa siku utafanya biahsara yakoi vizuri
Kila la kheri