MSAADA : BMW 5 SERIES 2007 Vs TOYOTA CROWN ATHLETE 2008

MSAADA : BMW 5 SERIES 2007 Vs TOYOTA CROWN ATHLETE 2008

Bwana Chiniko

Member
Joined
Jul 18, 2016
Posts
20
Reaction score
9
Kwa mara nyingine tena, nimeona nimalize kiu na utata uliokuwa ukinisumbua kwenye kichwa changu kwa muda mrefu.

Mada mezani ni kati ya Bmw 5Series 2007 na Toyota Crown Athlete 2008, ishu imekuja kufuatia ubishani uliotekea baina ya magari haya mawili ya kampuni tofauti.

Nikianzia na BMW 5series, wapo waliosema kumiliki gari aina ya Bmw alafu ukawa nayo moja ni hatari sana hasa kwa mazingira ya bara letu la Africa.

Akidai ya kwamba joto na hali halisi kwa ujumla, hupelekea magari aina ya Bmw kushindwa kuhimili, ndio maana wamiliki wengi wa Bmw huwa wanakuwa na magari mengine ya ziada hasa kutokana na gari hilo kuwa la kilakshari zaidi.

Akaenda mbele zaidi na kudai kwamba hata service zake na vifaa vyake ni ghali zaidi, ndio maana unakuta kwenye baadhi ya magarage unakutana na Bmw bado inadai lakini imekufa tofauti na magari ya kampuni nyingine.

Akamalizia kwa kusema kwamba Bmw 5series toleo la mwaka 2007 hata kwa bei huwezi kulinganish na Crown Athlete, akiwa na maana ya kwamba Crown ipo juu zaidi ya Bmw 5series.

Pia Crown inauwezo mkubwa wa kuhimili hali ya hewa ya bara la africa na unaweza ukawa nayo moja na ukaitumia pasipo wasiwasi wowote hasa ukizingatia kampuni ya Toyota imekuwa rafiki sana wa kukopi na mazingira ya bara letu.

Nimeambatanisha picha na sifa za magari tajwa na specifications zake. Wajuvi wa mambo nahitaji mnisaidie mawazo yenu katika hili pia.

Nawasilisha
 

Attachments

  • bmw 2007 5series.jpg
    bmw 2007 5series.jpg
    25.8 KB · Views: 269
  • bmw 2007 5series1.jpg
    bmw 2007 5series1.jpg
    26.6 KB · Views: 268
  • BMW Specs 2007 bmw 5series.jpg
    BMW Specs 2007 bmw 5series.jpg
    21.3 KB · Views: 237
  • C Athlete.jpg
    C Athlete.jpg
    24.2 KB · Views: 265
  • Crown Athlete specs.jpg
    Crown Athlete specs.jpg
    23.9 KB · Views: 246
  • Crown Athlete.jpg
    Crown Athlete.jpg
    23.6 KB · Views: 344
Kwa ninachofahamu mimi magari mengi tunayotumia wabongo ambayo ni Used hayakutengenezwa kwa ajili ya kutumika kwetu na ndio maana hatuna uwezo wa kuyanunua yanapokuwa Mapya(Brand New). Hivyo linapokuja suala la ugumu na matunzo inategemea na uwezo wa mmiliki na aina ya mafundi tulionao. Kikubwa ninachokiona mimi ni tatizo la mafundi, mafundi wetu wengi ni watu wa kubahatisha sana..ni wachache wanaojua nini wanafanya. Hivyo naweza kusema magari yote hayo uliyoyataja yanaweza kuwa mazuri tu kutegemea na mfuko wako unavyotumika kuyamaintain.

Asante.
 
Watanzania hadi leo katika dunia ya sasa wana uwezo na hawaogopi kuagiza gari Japan ila hawana uthubutu wa kuagiza spareparts toka huko waliko agiza magari! Leo hii mfano ukiagiza spare toka German tuchukulie mfano Oil Pump ya BMW haizidi wiki mbili unakuwa umeshaipata kwa njia ya DHL au nyingine..ila cha ajabu unakuta mtu ananua (anaagiza) BMW spare anaenda kununua Kariakoo gerezani za magumashi na kuchonga!
 
Mh ila hiyo BMW mi naona kama haisogezi mguu kwa Toyota Crown s200 ya 2008,iko vizuri sana,hasa interior designing yake,isitoshe ni pana sana kitu kinachoifanya itulie sana barabarani.
 
Back
Top Bottom