Msaada: Black screen baada ya window upgrade

Prince Nadheem

JF-Expert Member
Feb 25, 2012
1,259
1,053
Habari za week end wadau wa JF Tech? Niende kwenye point moja kwa moja, nilipata notification ya availability ya windows 10 kwa PC yangu ambayo ni HP 635. Niliweka bando ya kutosha na kupakua update yote na installation ikaenda vizuri tu. Sasa kwenye hatua ya mwisho ya PC kuwaka ndio kizungumkuti kimeanza sasa maana yake PC inatoa Black Screen na haiendelei though cursor inaoenaka.
naombeni msaada wa kuninasua kwenye hili janga....
Nimeambatanisha picha za hali halisi, moja ni kabla ya kusign in na hiyo blank ni mara tu baada ya kusign in
wp_20160117_19_41_51_pro.jpg
WP_20160117_19_39_52_Pro.jpg

NATANGULIZA SHUKURANI ZA DHATI​
 
Yawezekana window yako ya awali ilikuwa sio yalisi. Yaani Genuene na wakati unafanya upadate microsoft wameidaka. Jaribu ku restart hiyo pc. Unaweza bonyeza art+crtl+delete kwa pamoja then utapata option ya kurestart. Kama bado itasumbua tafuta window ingine kwasababu hawajamaa wakisha kamata huwezi ku crack tena window
 
Kama ume update kutokana na Windows waliyokupa Notification Microsoft wenyewe bado ni genuine... Inaweza PC ikawa inakosa kitu kimoja au viwili kwenye 'minimum requirement' ya kuweka Windows 10. Kuokoa jahazi tafuta tu boot loader ya windows 7 urudi ulipotoka uwe salama halafu ndo utaangalia utaratibu upya wa kuweka windows 10. Sio kila PC inaweza ikakubali windows 10 vyema.
 
Windows yangu ni genuine na ndio mana walinitumia notification ya availability ya update. Maana yake hapo shida ni hiyo blank black screen tu.
 
sidhani kama kuna kitu inakosa maana ina space ya kama 80GB kwenye drive C, RAM yake ni 2GB processor ni AMD vision. Pia nikitumia CTRL+ALT+DEL inaniletea options kama za kurestart, easy of access, restart, switch user na switch off. yaani ni full options zinakuja. kasoro ni hiyo moja tu. hata nikifungua task manager inaleta processes zote na naweza kuzi-end as I wish
 
Windows yangu ni genuine na ndio mana walinitumia notification ya availability ya update. Maana yake hapo shida ni hiyo blank black screen tu.
Kama ilikuwa genuine. Basi litakuwa tatizo lingine. Ila mie nawasiwasi sana na hapo. Jf wako ma expart weng pengine wao washa wahi kukutana na kitu ya hivo
 
Graphic driver siyo compatible na win 10.....washa pc ikifika ktk black screen bonyeza tna button ya kuwashia ikae ktk sleep mode,thn iwashe tena,itawaka vzuri thn update graphic driver....nilipata tatizo kma hilo na nilisolve hvyo.
 
Hapo kuna tatzo moja kati ya haya mawili.
1. Hardware Comfrict.
Hiyo window uloweka yan upgrading haiendani na hardware zako. Drivers zimegoma kwendana na software.

SOLUTION.
Toa hardware zote interna and external lakn acha HDD na RAM kisha washa Machine.

Printer na PCI Card zote, Cd Rom, Floppy na nyingnezo toa kisha washa machine ikiwa na hdd pamoja na ram.

Ukikwama nichek 0655/0767 033013

2. RAM (Memory)
Uwezo wa RAM ni mdogo ukilinganisha na windows uloweka.
 
Graphics drivers not compatible with your hardware after update.

Soln: Go back to your window 7 and enjoy the olds
 
Ni kweli walichosema wadau... Ambacho nilieleza mwanzo lakini wao wameeleza vizuri... Windows 10 ni incompatible na PC yako... Likiwa swala la drivers unaweza update online ila ni kama 'hardware' zenyewe zimekataa rudi Windows 7....
 
Pole mkuu... Fanya hivi ukiita taskmanager > opt kufungua new task kisha andika neno "explorer" halafu gonga enter
 
Au umeitoa kabla ya kumaliza installation hivyo missing some drivers au net uliyoitumia haikuwa stable tafuta net urudi katika link ya ms udownload upya itaricover bad sector outomatically
 
Ahsanteni sana wakuu, kesho nitafanya hivyo nikiwa kwa office maana hapa nimeshajilaza tayari kwa kesho kupambana na foleni za Jiji. Ila nawaahidi nitawaletea mrejesho kwa kila hatua nitayojaribu
 
Tatizo ni window 10 yenyewe.Hii window bado ni mpya so kunabaadhi ya vitu inakosa.Tatizo kama hilo wengi huwatokea pia.Chakufanya toa betri alafu zima pc.Subiri baada ya dk 5 then washa pc bila ya betri.
 
Back
Top Bottom