Ukiwa unatoka Dar kwenda Kilimanjaro na Arusha gari ya kwanza kufika ni Dar express ya Nairobi au Karatu,pia KLM yanatoka pale Shekilango saa 5:45,kwenye saa nane uko Moshi.Lakini ukiwa unatokea Moshi kuja Dar gari ya kukuwahisha ni Buffalo au Ngorika ambayo sio luxury na zenyewe kwenye saa nane uko Dar hizi zinaanzia safari Moshi na sio Arusha.hizo Ngorika,Buffalo,Kirumo na Machame Safari ni kweli zinakimbia lakini zinachelewa kuondoka na Kufika Moshi ni saa tisa au saa kumi.