Msaada: Baba yangu anasumbuliwa na miguu

Msaada: Baba yangu anasumbuliwa na miguu

BradFord93

JF-Expert Member
Joined
Oct 11, 2017
Posts
921
Reaction score
2,246
Ana miaka 62 mpaka sasa,

Umri wake ni bado saana kwa haya anayoyapitia

Miguu inamuuma saana

Miguu pia inavimba

Kuna mda akinywa maji mengi haja ndogo inatoka yenyewe

Pia ana tatzo la kupoteza kumbukumbu.

Naombeni msaada kujua wapi pa kuanzia maana umri wake bado saana....wenzake wa umri sawa na yeye hata waliompita hata hawana shida
 
Ukishaenda hospitali? Au ndo umeanzia hapa kaka?
Tumeshaenda amana...mkoani alienda...pia tumejaribu hospital flan private ila bado..

Amana walisema presha ipo juu na pia ana infections kwenye njia ya mkojo...akapewa dawa lkn bado
 
Acha kumlinganisha na watu wengine Hilo la Kwanza.

La pili mpeleke hosipital.

Mwisho kabisa pole sana na punguza kupanic mzee atakaa sawa na Mungu amponye upesi.

Itikia Aamina.
Amen
 
ach kwanza kumlinganisha na wengine kila mtu na mtindo wake wa maisha, kuhusu miguu ebu chukua vitunguu katakata mtindo wa duara alafu muwekee chini ya unyayo utanipa mrejesho haya mengine ngoja wengine waje
 
Nimuwekee chini ya sendoz au??
 
Ana miaka 62 mpaka sasa,

Umri wake ni bado saana kwa haya anayoyapitia...
Mkuu miguu kuvimba atakuwa anayo maradhi kwenye figo lake halifanyi kazi vizuri nenda kampime figo lake je lipo sawa?na pia umpime UTI na njia ya mkojo ili tupate kujuwa sababu ya maradhi yake. Ukimtibia Hospitali hajapona nitafute mimi kwa wakati wako ili niweze kumtibia mzee wako auguwe pole.
 
Mkuu mleta mada Mzee anatumia dawa za presha? Aina gan ya Dawa?
Je ulisha mpima sukari majibu yapoje?
 
Mkuu mleta mada Mzee anatumia dawa za presha? Aina gan ya Dawa?
Je ulisha mpima sukari majibu yapoje?
Sukari hana...!!kwenye suala la presha kuna dawa anatumia jina mpaka nilitafute kwakweli...nlimpeleka hosptal wakasema kuna vitu inabd awe anapunguza kula...hasa mafuta na chumvi...pia kwakuwa miguu inamuuma wamesema awe anakula saana bamia....jana amesema angalau miguu imepungua maumivu....Mungu anasaidia
 
Sawa mkuu.Aongeze ulaji wamboga za majani aepuke matunda yenye sukari nyingi ,aepuke kula wali kabisaaaaa na ugali wa sembe.
 
Back
Top Bottom