Evelyn maneno makali sana, huyu mtu ana tatizo unajua, tumpe ushauri wa kujenga mahusiano yake pesa ni kiamsho cha mapenzi na sio mapenzi. Kama pesa ingekuwa kadi nyekundu kwenye kila mahusiano hata mimi nisingekuwa nimeoa hadi sasa.
Anaona uwezo wako mdogo na needs zake anajua ni nyingi to the extent anahisi hutoafford AU amekuwekea mazingira ya wewe kuwa aware she will need your support ambapo kama kweli umempenda sio kitu cha kukukimbiza hicho just talk to umpe assurance ya that u will be there for her kwa kadra ya uwezo wako so far lazima utakua ushamchunguza na kujua wat type of gal she is
Habari zenu wana MMU?
Leo nimerudi baada ya muda kupita, kiufupi mambo bado hayajakaa vizuri kwa upande kwani kila ninapojaribu kuwekeza mambo yanaharibika...
Kilichonileta ni hiki, kuna binti ambaye tumefahamiana takribani mwaka sasa. Mwanzo alikuwa rafiki yangu wa kawaida, ila baada ya muda kupita nikaona ana vigezo ambavyo nimekuwa nikiviitaji.
Baada ya kujridhisha niliamua kuvunja ukimya. Niliongea naye kwa kirefu na akaonesha kuelewa kile nilichokuwa nikimwambia. Alichonijibu ni kwamba yeye ana kazi mpaka sasa, hivyo anaogopa kuwa mzigo kwangu. Nilijaribu kumpa moyo kwamba asitie shaka, kazi atapata kwani toka amalize chuo hata mwaka haujaisha, bado alionekana kuwa na wasi wasi na kudai wanaume wengi hatupendi wanawake wasio na kazi.
Kinachonitatiza...
Mimi nimeajiriwa na bado sijamaliza hata mwaka, hivyo bado sina kipato cha uhakika.
Je nitumie mbinu gani kumuweka sawa na kumfanya ajue hali yangu?
Je hizi kauli za naogopa kuwa mzigo haziwezi kuwa mbinu za maandalizi ya kunigeuza ATM?
Natanguliza shukrani!!!!
::
Kwa kuwa hakuna miongoni mwenu basi uangalifu wa hali ya juu unahitajika sana.Muulize ktk hali ya utulivu maswali yafuatayo
::
1.ANATARAJIA NINI KUTOKA KWAKO?
Ni swali rahisi kwa kulitazama ila majibu yake yatakupa mwanga.Mf akisema anatarajia wewe umpe pesa,muwe na magari,,uwe msamehevu kila anapokukosea au suluhisho la matatizo yake yote.BASI ujue una mtu ambae ndoto zake ni kupata maisha ya fahari kwa haraka
Ila akisema anatarajia uwe msikivu,uwe tayari kuzungumzia tofauti za kimtazamo ktk ndoa yenu BASI mpe alama ni mwanamke aliyejiandaa kujenga familia na yeye kukuambia kuwa mzigo ni hofu tu.
::
JE,,ANASEMAJE KUHUSU MISAADA,PESA,KTK MAISHA YENU YA NDOA?
Ninachojua mimi kila mwanamke angependa kuolewa na mwanaume ambae atapata nafasi ya kujigamba mbele ya wenzake.Akiona social status yako ipo chini ila kuna mwingine anamnyemelea na atatimiza lengo lake basi ataanza kutoa visababu.
Pesa ndio general formula ya yeye kufikia haja hii,,je akipata hiyo kazi nani atakuwa na sauti ktk mshahara wake? Au mshahara wake atautumia vipi?
Kuwa makini na majibu yake,jua wakati gani anatania au anamaanisha.Itakupa picha fulani.
::
JE ANAFIKIRI NINI AKIKOSA KAZI?
Ingawa hatuombei ila yeye kama msomi anafikiri nin? Au ndio wale ambao wanatumia kazi kama silaha ya kuamua wapendavyo?
Nachojua mimi,,mwanamke anakupenda hayuko tayari kuchezea nafasi ya kumuoa kwa sababu zisizotabirika.Ni kweli ndoa ni kusaidiana kiuchumi lakin nyuma ya nafsi ya mwanamke angependa kwanza kuhakikisha amekuweka kiganjani ndio aanze sarakasi nyingine.
::
NAJUA UNAMPENDA..lakini usidanganywe na majibu rahisi..ikibidi jaribu tu kumwambia "O.K asante kunihurumia usiwe mzigo,,ur free to go" ukae kimya,,uone ata-react vipi! Ndio utajua anamaanisha nini?
=
Tindikali... So far naona you are handling the matter well (IMO). Kwa mtazamo wangu inaweza kuwa anajibu hivyo kwa sababu kati ya hizi mbili. Nazo ni sababu ambazo zinategemea circumstances, tabia zenu, muonekano na maisha yenu upande wa kujiweza.
Moja;
Anajua kuwa umempenda, na anajua fika kuwa uwezo wako ni mdogo ila huwezi ukakosa kumpa za mara kwa mara. Kwa kukuambia hivyo anaku commit ki intelligensia wewe ukubali kujitahidi kadri ya uwezo wako kumpa support inapostahili na take note hiyo itakuwa mara kwa mara.
Mbili;
Inawezekana kweli kakupenda... Na kakusoma kuwa you are the type of guy ambae una jali sana na you take care of the people around you hasa if she is your woman. Hivyo tokana na mengi aliyonayo anahofia kuwa anaweza kuwa mzigio katika mahusiano hayo na hivyo kuwa tatizo kwa afya ya mahusiano yenu.
Katika hili tatizo lako... Ukitaka kuhakikisha hilo siyo lengo lake (Kukutega kwa kutoa ahadi); mwambie ukweli... Mwambie kuwa wewe bado ni mchanga na ndiyo unajijenga.. Na kuwa sababu wote huu ni mwanzo taratibu mtakuwa mkipigana jerk pale inapowezekana. Na muulize anapokuambia anaogopa kuwa mzigo ana maanisha nini? Sababu niya ni kujenga urafiki ambao unaweza ingia katika ndoa na si kwamba ndio mnataka kuoana.
Habari zenu wana MMU?
Leo nimerudi baada ya muda kupita, kiufupi mambo bado hayajakaa vizuri kwa upande kwani kila ninapojaribu kuwekeza mambo yanaharibika...
Kilichonileta ni hiki, kuna binti ambaye tumefahamiana takribani mwaka sasa. Mwanzo alikuwa rafiki yangu wa kawaida, ila baada ya muda kupita nikaona ana vigezo ambavyo nimekuwa nikiviitaji.
Baada ya kujridhisha niliamua kuvunja ukimya. Niliongea naye kwa kirefu na akaonesha kuelewa kile nilichokuwa nikimwambia. Alichonijibu ni kwamba yeye ana kazi mpaka sasa, hivyo anaogopa kuwa mzigo kwangu. Nilijaribu kumpa moyo kwamba asitie shaka, kazi atapata kwani toka amalize chuo hata mwaka haujaisha, bado alionekana kuwa na wasi wasi na kudai wanaume wengi hatupendi wanawake wasio na kazi.
Kinachonitatiza...
Mimi nimeajiriwa na bado sijamaliza hata mwaka, hivyo bado sina kipato cha uhakika.
Je nitumie mbinu gani kumuweka sawa na kumfanya ajue hali yangu?
Je hizi kauli za naogopa kuwa mzigo haziwezi kuwa mbinu za maandalizi ya kunigeuza ATM?
Natanguliza shukrani!!!!
WOR NOT, just be strong and ready 4anythng, the matter is just real and true love. but chekn afya zen mpe moyo juu ya hayo anayofkri but mwambie kaz co mpaka aajliwe ila hata akjiajl mwenyewe ukmpga kampan ya capita baada ya kupata wazo la biashara.
Hapo kwenye blue. Ulijuaje! pia hakuna kaupendo hapo na hajavutiwa na wewe coz mtu akikupenda bwana mbona unakuwa accepted faster .......tafakari
Mbona unamshuku mapema, kukugeuza ATM wapi na wapi?