Mrisho Ngassa kucheza Norway? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mrisho Ngassa kucheza Norway?

Discussion in 'Sports' started by Lucchese DeCavalcante, Jan 24, 2009.

 1. Lucchese DeCavalcante

  Lucchese DeCavalcante JF-Expert Member

  #1
  Jan 24, 2009
  Joined: Jan 10, 2009
  Messages: 5,473
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Baada ya klabu ya Yanga kukataa kumruhusu mchezaji mrisho ngasa kwenda Norway kwenye klabu ya Lov-Ham Football kuwahi usajiri wa dirisha dogo, uongozi wa Lov-ham Football uliamua kuachana na Ngasa na kumchukua Mcameroon a mbaye ndiye atakayewahi ulaji huo uliokuwa dhahiri kwa Ngasa.

  Lakini juhudi za wakala wa Ngasa kuwashawishi Lov-Ham wawe na subira na waongeze pesa zaidi ya kiasi walichokubali awali cha Dola 50,000 za malipo kwa Young African F.C. Lov-Ham wamekubali kuwa na subira lakini wamekataa kuongeza pesa kwani wanaamini 50,000 USD ni nyingi kwa mchezaji wa kitanzania kutokana na ukweli kwamba hapajawahi kutokea mchezaji wa kitanzania kufanikiwa katika mpira wa kulipwa ulaya hivyo basi kumchukua Ngasa ni kama kucheza mchezo wa bahati na sibu.

  Lov-Ham wamekubali kwa sharti jipya kwamba laziwa iwe mwezi huu au mwanzoni mwa mwezi ujao na safari hii atalazimika kafanyiwa majiribio kwani hakuna tena ulazima na uharaka wa kuwahi dirisha dogo kutokana na Mcameroon kuchukua nafasi ya Ngasa

  Tayari Lov-Ham wameuandikia uongozi wa Yanga kama walivyoelekezwa na wakala wa Mrisho Ngasa anayetambuliwa na FIFA ndugu Yusuf Bakhresa.

  Klabu ya Lov Ham Bergen ni timu iliyopo ligi daraja la kwanza (inayofahamika kama Adeccoligaen) nchini Norway na iko mji wa Bergen. Ligi kuu ya nchi hiyo inafahamika kama Tippeligaen yenye timu kongwe kama Rosenborg BK, Valerenga IF Oslo na Lillestrom SK.

  Je wachezaji wetu wafanye nini ili wapete na kufanikiwa kucheza soka la kulipwa ulaya kama kina Shabani Nonda?
   
 2. Lucchese DeCavalcante

  Lucchese DeCavalcante JF-Expert Member

  #2
  Jan 24, 2009
  Joined: Jan 10, 2009
  Messages: 5,473
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Ngassa1.JPG

  Huyu Kiungo kwa kweli usakati wake wa soka ni wa kiwango cha juu sana
   
 3. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #3
  Jan 24, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Tatizo viongozi wa Yanga akili zao zooooooooooooote zipo kwenye mechi ya yanga na Simba lazima watambania huyu dogo wao wanawaza tu kucheza na Simba.
   
 4. Lucchese DeCavalcante

  Lucchese DeCavalcante JF-Expert Member

  #4
  Jan 26, 2009
  Joined: Jan 10, 2009
  Messages: 5,473
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  IWAPO uongozi wa Yanga ungetoa ruhusa kwa kiungo mshambuliaji wa timu hiyo, Mrisho Ngassa angefanikiwa kujipatia kitita cha zaidi ya Sh milioni 432 katika kipindi cha miaka mitatu.

  Klabu ya Ligi Daraja la Pili ya Lov-Ham ya Norway iko tayari kumlipa mshahara wa dola 10,000 (shilingi milioni 12) kwa mwezi kwa kipindi cha miaka mitatu na huenda ingeongeza kiwango kama angepata mafanikio.

  Iwapo Ngassa angepata ruhusa kujiunga na timu hiyo, bila ya marupurupu angekuwa anapata kitita cha shilingi milioni 144 kwa mwaka hiyo inamaanisha kwamba kwa miaka mitatu alikuwa na uhakika wa kitita cha shilingi milioni 432 au zaidi.

  Ilielezwa kwamba baada ya wakala huyo kuwasiliana na uongozi kulieleza suala hilo mwamuzi wa mwisho ni mfadhili wao mkuu, Yusuf Manji kwa kuwa ndiye anayesajili wachezaji.

  Mwanaspoti ilifanya juhudi za kumpata Manji aliyerejea nchini hivi karibuni kutoka Marekani lakini simu yake ilikuwa imezimwa.

  Hadi jana mchana tiketi ya Ngassa ya kuondoka kwenda Norway ilikuwa katika ubalozi wa nchi hiyo jijini Dar es Salaam lakini imeelezwa hakukuwa na maelewano mazuri kati ya uongozi wa Yanga na wakala wake, Yusuf Bakhresa.

  Habari za uhakika zimeeleza kwamba, klabu ya Lov-Ham ilikuwa tayari kutoa kitita cha dola 50,000 (zaidi ya sh milioni 60) kwa Yanga ili imuachie mchezaji huyo kwenda Norway.

  Mchana kutwa Mwanaspoti ilimsaka Ngassa bila ya mafanikio kutokana na simu yake kuwa imezimwa, ila ilifanikiwa kumpata Mwenyekiti wa Yanga, Imani Madega aliyekiri kupokea taarifa za mshambuliaji huyo chipukizi kutakiwa na klabu ya Norway lakini akasisitiza suala la kufuatwa kwa utaratibu.

  "Kweli niliwasiliana na wakala na akaniambia kwamba Ngassa anatakiwa Norway na tayari tiketi iko ubalozini. Lakini hivi tunaweza kufanya biashara ya mchezaji haraka bila ya kufuata taratibu namna hiyo?," alihoji Madega jana kutoka Nairobi, Kenya.

  "Nimemwambia tunataka tukutane na klabu hiyo, tufanye amzungumzo kuhusu suala la Ngassa na baada ya hapo tutamuachia, sisi hatuna tatizo, mbona Ivo Mapunda na Said Maulid wameuzwa kwa kufuata utaratibu. Sidhani kama njia ya kumuuza mchezaji kupitia wakala bila ya viongozi wa klabu kuwa ni sahihi.

  "Hapo hatujajua iwapo Ngassa atakuwa anauzwa klabu nyingine, Yanga itafaidika vipi. Hilo ni suala la kufuata utaratibu na kuwa na mikataba ya uhakika badala ya kufanya mambo kwa haraka tu," alisema Madega.

  "Hatuna kinyongo, wala msituhukumu, tuko tayari kumuuza mchezaji yeyote lakini utaratibu ufuatwe na wanaotaka mchezaji wa Yanga basi wawasiliane na kukutana na viongozi wa Yanga ili tumalizane kiutaratibu jamani," alisisitiza Madega.

  Habari zimeeleza kwamba, Lov-Ham ilikuwa tayari kutoa kitita hicho cha dola 50,000 kwa kuwa wachezaji wengi wa Afrika iliowachukua hawana mafanikio.

  Lakini uongozi wa klabu hiyo ukasisitiza kwamba uko tayari kuweka kipengele ambacho kitatoa nafasi ya kuongeza kiwango cha malipo ya mchezaji huyo.

  Wiki iliyopita, Mwanaspoti ilifanya mawasiliano na Kharthoum, Sudan na kupata taarifa namna ambavyo Ngassa ni lulu nchini humo huku klabu kubwa za Al Hilal na El Merreikh zikionyesha nia ya kutaka kumnasa katika dirisha la usajili la mwezi Juni.

  Klabu hizo zimeonyesha nia ya kumchukua kwa dau kubwa zaidi kuanzia dola 160,000 kutoka kwa Al Hilal huku El Merreikh wakiwa tayari kutoa kitita cha kuanzia dola 400,000 (zaidi ya Sh milioni 450).

  Mshambuliajia huyo, ambaye ni mtoto wa zamani wa mchezaji wa Simba, Khalfan Ngassa na Pamba ya Mwanza �TP Lindanda� ameonyesha kuwa lulu kubwa kutokana na uwezo wake uwanjani anapokuwa na Yanga pia timu ya taifa, Taifa Stars.

  Ngassa ni tegemeo kubwa la Taifa Stars katika michuano ya Kombe la CHAN itakayoanza mwezi Februali nchini Ivory Coast.
   
 5. Lucchese DeCavalcante

  Lucchese DeCavalcante JF-Expert Member

  #5
  Jan 26, 2009
  Joined: Jan 10, 2009
  Messages: 5,473
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Mimi inanishangaza kidogo kuona jinsi tunavyo yachukulia mambo. Kwa nini swala la kuuza mchezaji linakuwa ni issue hata kutaka kulifanya kwa namna ya zima moto? Mimi ninavyo jua timu ina taka kununua mchezaji kutokana na uwezo wake binafsi na si swala la kuwahi au kuchelewa. Mchezaji yeyote mwenye uwezo atanunuliwa na timu yoyote si kwa kuwahi wala kuchelwa. Ikiwa mchezaji hana uwezo hatakama mtamuuza haraka haraka kama wengi wanavyo dhania ataenda kushindwa na kurudi. Mifano ipo mingi ya waliofikiri wamefanikiwa kumbe viwango vilikuwa chini. Kama kweli Ngasa anakiwango kinacho kubalika hajanyimwa ulaji kama ambavyo wengi wemeanza kusema ulajiwake upo pale pale, tena kwa timu kubwa kuliko hata hizo zinazotajwa. Kwamba mchezaji wa Tanzania hawezi kuuzwa kwa $400,000 inaweza kuwa kweli na pia isiwe kweli kwani hilo linategemea mambo mengi, kwa hiyo jibu lake siyo rahisi hivyo. Mimi nafikiri Ngasa aongeze bidii katika kazi yake atapata mafanikio makubwa.Hawa wanaotaka mambo ya zima moto sidhani kama wanamsaidia huyu kijana, msingi ni uwezo wake tu ndio utamsaidia. Inaonekana Tanzania tunajirahisi mno katika kile kinachoitwa kuuza wachezaji ndio maana wanakwenda jioni kesho asubuhi wamerudi. We are also expensive,uwezo wetu utuonyeshe kwamba nasi ni wa gharama na si mitumba.
   
 6. MtuSomeone

  MtuSomeone Member

  #6
  Jan 26, 2009
  Joined: Dec 7, 2008
  Messages: 58
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wachezaji wetu waacha kubweteka na kuiga ubishoo usiokuwa na ulazima! Unakuta mchezaji hata hajakuwa wa kulipwa tayari anakimbilia kuweka hereni na kusokota nywele awe kama fulani!!
  Sisi na kusuka nywele wapi na wapi?? Sasa dada yangu kule Mwembesongo anasuka nywele na wewe mchezaji (unajiita staa) unasuku si ujinga huu?? Mazoezi hatutaki, tunataka kuwa watu wa viwanja na tunalewa sifa....Shaaban Nonda Papii yupo wapi? Alipita hapa hapa Kaunda, tena yeye hakuwa Star kama kina Kizota (RIP) na wengineo...lakini alijua nini anatafuta....kaenda kwenye majaribio sasa alhamdulillah!!
  Halafu kingine sisi tuna ujanja wa hapa hapa Manzese, wewe mchezaji unapokutana na wachezaji wenzio wanaosakata soka nje ya nchi...say timu imekuja kukipiga nanyi, sema nao baada ya mechi..badilishaneni contacts, uliza mwenzangu umefanikiwaje? Nawezaje kuja huko au kwenda kwingine kujipima?? Tatizo letu umaimun anao unatuumiiza!!
  Washkaji wengine siku hizi wabopngo wanatoka sana tu, semeni nao, waagizeni wawaulizie huko uwezekano wa kufanya trials...siyo mnaagiza simu na viwalo tu!!
  Huu si ulimwengu wa utandawazi jamani?? Waulizew wachezaji wetu wangapi wana email address usikie kazi.....

  Ina maana utafiti hatufanyi sisi kama wachezaji!!!!

  Nakaribisha hoja tofauti
   
 7. Lucchese DeCavalcante

  Lucchese DeCavalcante JF-Expert Member

  #7
  Jan 27, 2009
  Joined: Jan 10, 2009
  Messages: 5,473
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Marselle wa Ufaransa nao wanamtaka na hata England pia
   

  Attached Files:

 8. A

  Amwanga JF-Expert Member

  #8
  Jan 27, 2009
  Joined: Jan 11, 2009
  Messages: 294
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Wadu vipi yeboyebo imekula miwa au imepigwa kwa mabua ya miwa?
   
 9. A

  Amwanga JF-Expert Member

  #9
  Jan 27, 2009
  Joined: Jan 11, 2009
  Messages: 294
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Jamani tupeni matokeo kati ya Yanga na Mtibwa.
   
 10. Lucchese DeCavalcante

  Lucchese DeCavalcante JF-Expert Member

  #10
  Jan 27, 2009
  Joined: Jan 10, 2009
  Messages: 5,473
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Yanga imeshinda 1-0, bado mechi nne ichukue ubingwa kabla ya ligi kuisha
   
 11. Kireka1980

  Kireka1980 JF-Expert Member

  #11
  Jan 28, 2009
  Joined: Mar 18, 2008
  Messages: 304
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  YANGA siii mchezooo! big up Madega,
  "Ngassa tupo tayari kumruhusu aende kufanya majaribio Norway lkn taratibu zifuatwe, tutamrusu aende kwa mkataba i.e akishindwa majaribio arudi Yanga, akifanikiwa tupewe chetu na akiuzwa kwa timu nyingine (third part ) Yanga wapewe 10%"
   
 12. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #12
  Jan 28, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,869
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Na bao limitiwa wavuni na huyu huyu Ngasa!
   
Loading...