Mrisho Gambo: Wapinzani watapotea

Hii nchi wapinzani wanaonekana ni maadui wa Taifa! Sijui kwa nini? Tangu alipomtukana yule dada mwanasheria wa Korogwe nimetokea kummchukia sana huyo Gambo!
 
Mwambieini sawa maana kuna watu wanajiona watakuwa watawala milele mpaka wana ajenda za kupoteza wapinzani
 
Madaraka yanalevya kuliko kokeeni
 
ale tu kodi etu hata apende first class kwenda paris kuhongwa kwa kukosa utu na ubinadamu kwa marehemu kutafuta kiki ya kuzuiya uwanja lakini mwisho wake kama wasirra tu alitangaza sana kuisha kwa upinzani amuulize marehemu komba na kombani wapo wapi waliosema upinzani utaisha naye atawafuata huko
 
Ana tuhuma zakutukana wanawake huyu,kimsingi sihangaiki naye maana watu wanaotusi wanawake WAMELAANIWA.
 
Ngoja nimkumbushe Gambo yy si kateuliwa tu hajui mziki wa siasa ya ana kwa ana ikoje ila ataujua 2020 ambapo ikitokea upinzani ukachukua asilimia kubwa ya majimbo arusha ataona hicho kiti ni kinawaka moto atalaani maisha yake yote.Nawashauri hawa vijana wafunge midomo yao siasa hawaijui wawaulize nape na kinana wataambia halisi Mimi shaidi kinana alifika wilaya moja kaskazin huko na helkopita lakini alichokikuta polisi ndio waiokoa jahazi niwasihi hawa vijana wanaopenda madaraka ya sifa jifunzeni hekima jifunzeni hata kwa Kagame anapenda uongozi lakini hasimami na kutoa kauli za ajabu.Vijana jichungeni sana kauli zenu siasa haina urafiki miaka kumi ni michache sana usije kujutia kauli zako na kusababisha Vijana wengine wasiaminike ni Maoni tu ya mtu anayewaza kijinga kama mm.
 
Atapotea yeye kwenye siasa kwa kutegemea vyeo vya kupewa na mtu awaulize walio mtangulia wako wapi?
 
Tatizo hawa vijana wanahisi watatawala milele..Niwakumbushe tu kuwa uongozi ni mpito,wayafanyayo leo matokeo yake watayaona kesho
Umenena jambo la msingi mkuu wangejiuliza kina fulani waliokuwa wanatamba wakati wa utawala wa mswahili wako wapi?
 
UNAWEZA KUWA UNAFANYA JAMBO SAHIHI LAKINI KWA KUTUMIA NJIA MBAYA.
JE MKUU WA MKOA ANATAKIWA KUFANYA PROPAGANDA ZA KISIASA?
JIBU NI HAPANA.
MKUU WA MKOA NI MTENDAJI MKUU WA SHUGHULI ZA KISERIKALI.
MIJI MINGINE MADIWANI WENGI NI WA UPINZANI NA MEYA NI WA UPINZANI.
MADIWANI NDIYO WASIMAMIZI WAKUU WA SHUGHULI ZA MAENDELEO ZA MKOA NA WILAYA HADI KIJIJI.
MKUU WA MKOA LAZIMA AFANYE KAZI KARIBU SANA NA HAWA WATU.
HANA SABABU YA KUWASUTA KWENYE MAJUKWAA.
MAPAMBANO YOTE AYAFANYE KWENYE VIKAO HALALI VYA KISHERIA.
MAMBO YA PROPAGANDA ZA KISIASA AWAACHIE VIONGOZI WA CHAMA.
RAIS AMEKATAZA KUONGELEA MAMBO YA VYAMA WAKATI HUU, JE INAKUWAJE MKUU WA MKOA KUFANYA TATHIMINI YA KUPOTEA KWA VYAMA VYA UPINZANI BILA KUKAMATWA NA KUWEKWA NDANI.
JE TUNDU LISSU AKISEMA HADHARANI KUWA CCM ITAPOTEA KUFIKIA MWAKA 2020 JE HATAKAMATWA?
VYAMA VYA UPINZANI VIKIPOTEA TUTAKUWA NA CCM LEGELEGE. VYAMA VYA UPINZANI VIMEKUJA KWA RIDHAA YA CCM PAMOJA NA KWAMBA WANAINCHI WALIVIKATAA KWA KURA YA MAONI.
 
Kasema wanachofanya wanapotea na kudeal nao; wote ni binadamu na wote tunaishi na kufa baadaye!
 
Kuna watu wakisha tajwa kwenye vichwa vya habari huwa sisomi alicho sema akiwepo huyu Gambo, Bashite Ndugai ....na watu wa aina hiyo maana hawajui wanacho ongea leo kitakuwa na matokeo gani kesho... Akili za kuwekewa
 
HakHaka kajamaa nako huwa kanaonekana kamejaa kiburi sana!
Anyway muda huwa ni hakimu wa kweli IPO siku mtajutia
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…