Mrisho Gambo: Ninao ushahidi wa watu waliotapeliwa Magari na Godbless Lema

Kumtetea gambo ni ngumu sana, aliulizwa maswali Star TV akajikoroga hadi aibu nikaona mimi! Arusha 2025 tunakwenda na Lema, huyu jamaa tumemchoka hakika, hatujui kafanya nini jimboni kwetu. Badala asikilize kero zetu na kuzipeleka kunakostahili, yeye anakomaa tu kumchafua Lema. Uzuri mmoja 2025 sio mbali, sisi ni pipo!
 
Pambana na serikali ilete maendeleo kwa wanna hi wako, hali ya barabara za mitaa, maji na madawati na uchakavu wa majengo hali ni mbaya.. Ya Lema ni ya jeshi la polisi hayakuhusu.
 
Kumtetea gambo ni ngumu sana, aliulizwa maswali Star TV akajikoroga hadi aibu nikaona mimi! Arusha 2025 tunakwenda na Lema, huyu jamaa tumemchoka hakika, hatujui kafanya nini jimboni kwetu. Badala asikilize kero zetu na kuzipeleka kunakostahili, yeye anakomaa tu kumchafua Lema. Uzuri mmoja 2025 sio mbali, sisi ni pipo!
Hakuna mwana Arusha mwenye akili Timamu atakayempigia kura ya ndio Lema.
 
Gambo hata wanaccm wenzake hawamkubali amegombana na watu wengi hivyo hana uhakika wa kupita kwenye kura za maoni.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Katika mahojiano yaliyofanywa kati ya mwanahabari Odemba na Mbunge wa Arusha Mjini Mheshimiwa Mrisho Gambo ameeleza mambo mengi sana kuhusu mbunge huyo wa zamani wa Arusha Mjini. ambapo ameeleza bila kusita wala hofu kuwa anao ushahidi wa kutosha wa watu waliotapeliwa Magari na Godbless lema,amesema hata leo hii anaweza kuutoa ushahidi huo ikiwa utahitajika, amesema hata sasa anahofia kuwa pengine Lema anaweza kuwa ameirudia kazi yake hiyo ya zamani maana kwa sasa hana kazi ya aina yoyote ile anayoifanya hapa nchini na hata ukimuuliza anafanya kazi gani hawezi kukwambia.

Ameeleza zaidi pia kuwa mbunge huyo anapenda sana dezo na mteremko ,na ndio maana ameshindwa hata kuilea familia yake na kuamua kuitelekeza nje ya nchi ambako inalelewa huko na watu.amesema kuwa anashangaa na kumshangaa kuwa Lema ni mchaga wa aina gani ambaye anashindwa hata kulea tu familia yake, maana wachaga wamezoea upambanaji tofauti na yeye lema anayependa dezo na mteremko kwa kila kitu.anasema alikimbia kwa visingizio lakini Rais Samia alipoingia madarakani akasema njooni nchini tujenge nchi yetu, lakini kwa kuwa Lema anapenda mteremko ameona familia yake ibaki huko huko inakolelewa bure.

Amesema mbona watu kama Mbowe au John Heche Wana familia zao hapa hapa nchini? Amesema kwani kuna tatizo lipi nchini kwa sasa? Amesema ni kutanga tanga na kuhangaika na kukosa kazi za kufanya kwa Lema ndiko kunakomfanya aogope hata kuleta familia yake nchini maana anajuwa watamdai mahitaji kama vile ada za shule na mahitaji mengine ndio maana anaamua aiche huko huko wanakomsaidia kulea.

Amesema kwa sasa Lema hata jimbo tu la kugombea haelewi agombee lipi maana anatanga tanga kwa kusema mara anataka kugombea hai ,mara atafute jimbo Dar .anasema anatanga tanga kwa kuwa hana kazi za kufanya na anaona Ubunge ndio ponea yake ya kuendeshea maisha yake .

Mimi mwenyewe namuunga mkono Mheshimiwa Mrisho Gambo kwa sababu haiingii akilini mtu alisema amekimbia nchi kwa sababu anawindwa na kukimbilia huko nje ya nchi nakuomba kusaidiwa kulishwa na mahitaji mbalimbali yeye na familia yake.lakini Dkt Samia alipoingia madarakani akasema njooni tujenge nchi yetu ,lakini cha ajabu baada ya kunogewa na mteremko wa kupewa msaada na matunzo na mahitaji yote kutoka kwa wazungu amegoma kabisa kuirejesha familia yake na badala yake karejea mwenyewe nchini nakuja kuwaporomoshea matusi watanzania kuwa kazi wanazofanya ni za laana na za kimaskini.

Kwa hakika ni jambo ambalo wana Arusha hawata kaa wasahau matusi haya waliyotukanwa na Lema ambaye walimchangiaga mia mia zao mpaka akapata ubunge na kwenda kula pesa bungeni, bila kuwatumikia wala kuwapelekea maendeleo ya aina yoyote ile zaidi ya kufanya mivurugu kuanzia Bungeni mpaka mitaani. Kwa hakika wana Arusha walikuwa sahihi kabisa kumfurusha Arusha mjini kwa kumnyima kura za ndio.kwa sasa akatafute kwa kugombea maana Arusha hakuna wa kumpatia kura maana alishawaambia kuwa wao ni maskini na wanafanya kazi za kimaskini ,ilihali alikuwa mbunge kwa miaka kumi na hakuwasaidia kwa chochote zaidi ya kuja kuwatukana tu baada ya kurejea kutoka kwa wazungu alikokuwa akilishwa na kuhudumiwa kwa kila kitu kama kuku wa kisasa wasio weza jitafutia chakula chao au Makinda ya ndege.

Sasa mwakani Ubunge hapati wala nini ili arudi huko huko kwa wazungu.maana hakuna wa kumpatia kura ili aje kuwalipa kwa matusi na kuwadhalilisha kama alivyokwisha kufanya baada ya kuwa amevimbiwa na kuzidiwa na shibe na kusahau alikotokea kisiasa na kimaisha.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

=====

“Godbless Lema anatanga tanga hayupo Duniani hata ahera hayupo, ni mtu anayependa mteremko, Lema anapenda dezo, hana mvuto, amewatapeli watu Magari Arusha na ushahidi ninao, hana kazi ya kufanya amekuwa kama jina lake… Godbless - Jobless” MRISHO GAMBO

Gambo amemrahi lema ahache kuwatesa watoto wake kwa kukaa Nchi za watu kwa sababu zake za kisiasa, arudishe watoto Nyumbani kwani Arusha hakuna shida yoyote, hayo mambo anayoyafanya ni aibu kwa kabila lake la wachaga, “wachaga si watu wa kulelewa, sijui hiyo tabia Lema ameitoa wapi” ….?

Ikifika hatua ya mtu kutoa kafara familia yake kwa maslai ya kisiasa huyo mtu anapaswa kuombewa, Odemba kama Lema ni rafiki yako mwambie Arudishe watoto wakamsalimie Babu yao..! Gambo.
View attachment 2940724
Lucas, hebu jiulize swali rahisi, hivi inawezekanaje ukawa shahidi wa aliyeibiwa wakati yeye aliyeibiwa yuko kimya? Wewe ukiibiwa na mwizi wako unamwona kila siku na kupishana naye barabarani na polisi wapo utamuacha kweli? Hizi tuhuma ni wajinga pekee ndio wanaziamini.

Vv
 
Lucas, hebu jiulize swali rahisi, hivi inawezekanaje ukawa shahidi wa aliyeibiwa wakati yeye aliyeibiwa yuko kimya? Wewe ukiibiwa na mwizi wako unamwona kila siku na kupishana naye barabarani na polisi wapo utamuacha kweli? Hizi tuhuma ni wajinga pekee ndio wanaziamini.

Vv
CCM ina hazina kubwa sana ya wapumbavu
 
Back
Top Bottom