Mnyanyembe wa Mboka
JF-Expert Member
- Feb 10, 2017
- 2,349
- 3,046
Sasa tunaanza kushuhudia watu wanajitekenya wenyewe na kujichekesha wenyewe, ni kama watu wanalazimisha hamasa ila kama ilivyo ada hamasa ya kutunga haiwezi kuonekana kamwe na itabaki kuwa sinema tu kama sinema zingine.
Watendaji kama wamepoteza mvuto, sikwambii hao wafuatiliaji ndio kabisa hawana bashasha hata kidogo yaani ni kama vile kumlazimisha Paka (Nyau) acheke.
Sasa watu wanatengeneza malumbano ili ionekane kuna amsha-amsha ya kukimbiza maendeleo bahati mbaya ndio wanazidi kuharibu kabisa.
Inaonekana kabisa mnacheza sinema za mzee yombayomba na kapu lake la vichwa vya samaki.
Anyways, tuliahidiwa kuishi kama Ulaya na ikasemekana wale ndio walikua wanachelewesha maendeleo haya sasa tunasubiri hayo maendeleo.
Msituletee mapichapicha ya kutengeneza hapa mrudi na visingizio hamna amsha-amsha yeyote hovyo!