PreGE2025 Mrisho Gambo: Mimi na yeye nani ameumiza wengi?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
4,395
Reaction score
14,502
"Kuna mambo mengine sikutaka kuyasema kwasababu nina uwezo mkubwa sana wa kupuuza lakini nimechokonolewa sana na baadhi ya watu kiasi ambacho inawezekana kuna baadhi ya watu mkachanganywa. Kwahiyo kwasababu nimelazimishwa, mengi nitapuuza, nitasema walau moja, naomba mnikubalie.

Kuna mtu mmoja ambaye amekuwa akijinadi siku nyingi anasema wakati anaenda kwenye SendOff alitumia Koti langu mimi mtoto wa muuza uji. Lakini leo hii anadiriki kufikia kusimama mahali anasema eti Gambo ameumiza watu wengi, leo nataka niwaulize hivi mimi na yeye nani ameumiza watu wengi katika nchi hii? hivi mnapajua Dar Es salaam ninyi? nendeni mkatafute habari zake kule hata kumsalimia mtaogopa.

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Nataka popote alipo mumuambie mikono yangu ni safi!sima changamoto yoyote na sijamuumiza yeyote badala yake nimesaidia watu wengi sana kote nilipopita. Nimesaidia watu wenye ulemavu, tumewapatia viti mbalimbali kwaajili ya kuwasaidia, tumewasaidia watu kupata miguu bandia ambao hawakutarajia kupata ulemavu, tumesaidia vituo vya yatima, tumesaidia kila mahali. Mwambieni hayo ni matendo mema hakuna hata moja la kumuumiza mtu."

Na nimeamua nisema kwasababu amesema eti nenda kwa wananchi wa Arusha, nenda kawaombe radhi, wananchi wa Arusha nimewahi kuwakosea?"- Mrisho Gambo, Mbunge wa Arusha Mjini.

Gambo, Sabaya na RC ni watu makatili sana. Ingekuwa vyema wangeheshimiana tu kwenye awamu hii ya Mama. Kwenye awamu ya 5 hao ndo walikuwa vinara wa ukatili. Gambo enzi zake kaweka mahabusu hadi viongozi wa dini waliokuwa wanaenda kutoa rambirambi kwenye msiba wa watoto wa Lucky Vicent kisa tu rambirambi hazijapita ofisi ya mkuu wa mkoa. Sabaya ana uovu mwingi zaidi ambao haukufika kwenye media. Kujitwalia viwanja kihuni ilikuwa ni moja ya mambo yao hao watatu.
 
"Kuna mambo mengine sikutaka kuyasema kwasababu nina uwezo mkubwa sana wa kupuuza lakini nimechokonolewa sana na baadhi ya watu kiasi ambacho inawezekana kuna baadhi ya watu mkachanganywa. Kwahiyo kwasababu nimelazimishwa, mengi nitapuuza, nitasema walau moja, naomba mnikubalie.

Kuna mtu mmoja ambaye amekuwa akijinadi siku nyingi anasema wakati anaenda kwenye SendOff alitumia Koti langu mimi mtoto wa muuza uji. Lakini leo hii anadiriki kufikia kusimama mahali anasema eti Gambo ameumiza watu wengi, leo nataka niwaulize hivi mimi na yeye nani ameumiza watu wengi katika nchi hii? hivi mnapajua Dar Es salaam ninyi? nendeni mkatafute habari zake kule hata kumsalimia mtaogopa.

Nataka popote alipo mumuambie mikono yangu ni safi!sima changamoto yoyote na sijamuumiza yeyote badala yake nimesaidia watu wengi sana kote nilipopita. Nimesaidia watu wenye ulemavu, tumewapatia viti mbalimbali kwaajili ya kuwasaidia, tumewasaidia watu kupata miguu bandia ambao hawakutarajia kupata ulemavu, tumesaidia vituo vya yatima, tumesaidia kila mahali. Mwambieni hayo ni matendo mema hakuna hata moja la kumuumiza mtu."

Na nimeamua nisema kwasababu amesema eti nenda kwa wananchi wa Arusha, nenda kawaombe radhi, wananchi wa Arusha nimewahi kuwakosea?"- Mrisho Gambo, Mbunge wa Arusha Mjini.
Haya mambo ni matamu mno.Hii ndiyo story ninayopenda kuisikiliza sana.
 
Back
Top Bottom