PreGE2025 Mrisho Gambo ashauri wenyeviti wa mtaa kulipwa Laki 3

PreGE2025 Mrisho Gambo ashauri wenyeviti wa mtaa kulipwa Laki 3

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Dalton elijah

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2022
Posts
780
Reaction score
1,831
Wenyeviti wa serikali za mitaa ndio msingi wa uongozi katika nchi hii, kama sasa hivi wanapita nyumba kwa nyumba, kuhakikisha kwamba wanatambua nyumba zilizopo, wanapiga picha ili mwisho wa siku serikali iweze kukusanya kodi kwenye sekta hiyo, wanafanya kazi kubwa lakini wanalipwa laki moja tu kwa mwezi...

Kwahiyo ningependa kwenye bajeti hii ya serikali badala ya kuwalipa kwa laki moja tu [Wenyeviti wa Serikali za Mitaa] kwasababu mapato tunayo mengi kama Jiji la Arusha, ukienda Mkoa wa Dar es Salaam majiji yote yale, ukienda Jiji la Mbeya na maeneo mengine...

Nilikuwa nadhani [Wenyeviti wa Serikali za Mitaa] wangelipwa angalau laki tatu kwa mwezi ingeweza kuwasaidi kupata nauli na masuala madogo madogo kulingana na changamoto za maeneo kama hayo.” Mbunge wa Arusha Mjini Mrisho Gambo akichangia hoja kwenye Bajeti kuu ya serikali Bungeni Jijini Dodoma June 17, 2025.
 
Back
Top Bottom