Halisi
JF-Expert Member
- Jan 16, 2007
- 2,802
- 617
There is no substance in his tamko!
Duh, kazi kweli kweli... Akili ni nywele hata vipara wanazo
There is no substance in his tamko!
Kama kweli UVCCM wanakitakia mema Chama chao na nchi kwa ujumla, basi wajitokeze na kutamka hadharani kuwa hawakubaliani na Ufisadi. Baada ya hapo wawataje Mafisadi hao kwa majina na nafasi zao ktk Chama, na kuwataka waondoke ktk Chama ili watu wafanye kazi za kujenga nchi badala ya kutumia muda mwingi kuchekea "upumbavu" ndani ya Chama.
Tualitaka hili lifanyike pia kwa CCM wenyewe. Kwanini munaoneana haya wakati munaangamia? Munategemea nini? Yaani Chama na nchi viangamie kwa sababu ya watu wachache saaana? Nani kasema maneno hayo? Wakati wa mageuzi ndani ya CCM ni sasa.
Mengi aliongea baada ya Dr Slaa kuwataja mafisadi papa 11 pale kidongo chekundu. Walitangaza kuwa wataenda kumshtaki lakini hakuna aliyethubutu kwenda mahakamani. Na kumuandama JK ni kwasababu nae yumo kwenye list na vilevile ni kwasababu yeye ana mamlaka kwahiyo angeweza kuwachukulia hatua mafisadi lakini anaogopa.
Alaa, kumbe machalii wa Arusha hawawezi kupambana hadi mazagazaga ya ccm yaje kuwasaidia? Waombe radhi wana Chadema wa arusha tafadhali. Hawahitaji walioshindikana ccm
Kwanza kabisa, naomba tuweke rekodi zetu sawasawa, Kamati ya Utekelezaji na Baraza la mkoa vilipangwa siku nyingi kabla ya baraza kuu la taifa, kwahiyo tusimtafutie mtu sympathy, havina mahusiano. Yeye labda alilitumia baraza kuu ili apate umaarufu na ili asifukuzwe, kwasababu alikuwa anafahamu kwamba lazima atajadiliwa na kufukuzwa tu.
Mimi nilichoshangaa sana kikubwa leo ni jinsi huyu kijana alivyotoka na kumtetea Kikwete na Batilda, labda kwa wale ambao hawamfahamu, huyu kijana ni mzaliwa na mkazi wa hapa Kariakoo Dsm na alienda Arusha miaka mitatu iliyopita na huko akakutana na rafiki yake kipenzi James Millya, ambaye alimtambulisha kwa Wamasai, Wa-Iraq, Wachaga, Wameru, Waarusha, Wasonjo na makabila yote kwenye wilaya zote za mkoa wa Arusha na kumuombea kura, kwasababu hamna mtu aliyekuwa anamjua, na akachaguliwa kuwa mjumbe wa baraza kuu taifa kuwakilisha mkoa. Alipokuwa Arusha aliishi kwa Mlezi wa James Millya pale Sakina na baadaye akachukuliwa na Mzee Elisa Mollel, ambaye amemlea kwa miaka hii mitatu kama mwanawe - Ninashangaa leo anavyothubutu kutukana ufisadi. Elisa Mollel ndiyo aliyofilisi kampuni yetu ya National Milling Corporation, na Nyerere akamshughulikia ipasavyo, ni bepari na beberu kwelikweli. Akiwa Arusha alimtukana Batilda matusi makubwa sana na kumhusisha Kikwete kwa maneno ambayo siwezi kutumia hapa - Huyu kijana ameshakuwa MCHAWI, siyo mnafiki tena.
Chuki yote hii ya huyo kijana kwa CCM ilianza pale Elisa Mollel aliposhindwa kura za maoni na Ole Medeye, na tena aliachwa kwa mbali sana - Medeye zaidi ya kura 10,000 akifuatiwa na Sabaya aliyekuwa na kura 8,000 na baadaye Elisa kura 2,000. Huyu kijana ndiyo alikuwa kampeni meneja. Baada ya matokeo hayo wakaunda genge la mtandao wa kuhujumu CCM Arusha Mjini kwa rafiki yao Felix na Arumeru, na hapa ndiyo nasema nashangaa.
Akiwa Arusha alikimbia vikao vyote alivyoitwa, siyo mwanaume huyo! KIla akinusa, hapashikiki. Kwani hatujui kwamba ndiyo mbeba mikoba wa Mbunge wa Arusha, UVCCM Mhe Catherine Magige?? Na hapo amefuatwa nini?? Tumbo linamsumbua. Ni aibu hata kumjadili huyu kijana hapa, hasathili. NI UCHAFU
Huyu kijana akiwa Arusha anajigamba na tena kwa matusi mazito kabisa jinsi ambavyo amewachakachua CCM kwenye kompyuta za manispaa na kuisaidia Chadema, mimi ningetegemea kuwa angetoka kwenye vyombo vya habari na kusema NINAHAMA CHAMA na ni kweli nimefanya hayo niliyoyafanya, na ndiyo maana hakuweza kuita waandishi wa habari kule Arusha, wasingemuelewa. Kwa Mhe Membe akamuita Dsm na kumuandalia mtaalamu wa fitina-Mbaraka Islam, kuandaa waandishi wa habari pale TAMAL Hotel.
Huy kijana siyo msaada kwa CCM na anatikiwa kufukuzwa Chama kabisa, na pia simuoni kama anaweza kukisaidia Chadema, tayari Chadema kina vijana wenye msimamo wa ukweli kama wakina Albert Msando pale Arusha na hawayumbishwi kwa matumbo yao kama huyu kijana. Ni aibu kuwa na vijana kama hawa kwenye jamii. Hafai kwa Chama chochote. Alipewa kazi manispaa ya Arusha kwa kifua cha CCM, vijana wengi wenye ouwezo Arusha mjini wakanyimwa kwasababu ya u-CHAdema wao, ndiyo maana leo hajui pa kukimbilia
Hivi wakati haya yanatokea Benno Malisa alikuwa wapi? Au nae kishawekwa ktk kapu la mafisadi?
Nasema Benno kwa sababu hakuna asiyejua kuwa Shigela ni kibaraka wa mafisadi na yupo pale kulinda maslahi zao. Siku zenu zinahesabiwa, hakuna kupona ktk hili la kuiangamiza nchi. Hivi ni nani asiyejua kuwa suala la Richmond na Dowans, EPA na Kagoda, Deep Green na Meremeta ndio vilivyoipunguzia CCM kura ktk uchaguzi uliopita?
CCM sio ya watu wachache kama wengi wanavyofikiria, hiki ni chama cha wananchi. Wale wote wanaotuhumiwa na Ufisadi walioko ndani ya CCM waondoke kabla hawajaondolewa na nguvu ya Umma.
Jamani nyie mnaosema kuwa mtawatimua SISIEM hao mafisadi mtaweza?????????? Sasa wanajichimbia mizizi hadi watoto wao wana madaraka makubwa ndani ya UVWCCM na SISIEMU!!!!!!! Kwa hiyo si rahisi kama mnavyo fikiri, wana fedha na ukitilia maanani ni watu wachache wa kukataa mshiko, labda huyo kijana wangu Mrisho Gambo!!!!!!!Hivi wakati haya yanatokea Benno Malisa alikuwa wapi? Au nae kishawekwa ktk kapu la mafisadi?
Nasema Benno kwa sababu hakuna asiyejua kuwa Shigela ni kibaraka wa mafisadi na yupo pale kulinda maslahi zao. Siku zenu zinahesabiwa, hakuna kupona ktk hili la kuiangamiza nchi. Hivi ni nani asiyejua kuwa suala la Richmond na Dowans, EPA na Kagoda, Deep Green na Meremeta ndio vilivyoipunguzia CCM kura ktk uchaguzi uliopita?
CCM sio ya watu wachache kama wengi wanavyofikiria, hiki ni chama cha wananchi. Wale wote wanaotuhumiwa na Ufisadi walioko ndani ya CCM waondoke kabla hawajaondolewa na nguvu ya Umma.
Hivi kwani mtu hawezi kuwa mpambanaji mpaka atoke ndani ya ccm? Mi sikubaliani na wote wanaotaka wanaopambana na ufisadi watoke ccm kwanza.
Wako wapi kina Mpendazoe, Mrema nk? Wote wamechemsha baada ya kuhama CCM.
Mpambano ni lazima uwe ndani ya chama ili kuwang'oa wezi wa nchi hii. Nashauri wapiganaji wote wasihame CCM ila wawe makini na michezo michafu inayofanyika ndani ya CCM.
"msiwaachie nguruwe wale shambani peke yao"