Mrisho Gambo aongea na wanahabari

Mutwale

Member
Oct 20, 2010
67
19
Yule Kada wa CCM kupitia UVCCM aliyeanzisha sakata la akina EL na RA ataongea na wandishi wa habari leo saa nne asubuhi, hapa Dar es Salaam.

CHINI NI TAMKO LAKE FULL TEXT

=======================

TAARIFA YA NDUGU MRISHO GAMBO KWA VYOMBO VYA HABARI
JUMAPILI TAREHE 3 APRILI 2011

Ndugu zangu wahariri na waandishi wa vyombo vya habari, nimeona leo nikutane nanyi ili niweze kufafanua mambo machache maana mmekuwa mkinipigia simu sana pamoja na kuniandikia ujumbe wa maandishi kwa lengo la kutaka kupata maoni yangu kuhusu maazimio ya baraza la vijana la mkoa wa Arusha na yalio andikwa kwenye magazeti kabla ya baraza hilo na baada ya baraza hilo. Kwa kuwa yaliondikwa yamegusa utu wangu na kwa kweli nisingeweza kukutana na mtu mmommoja ili kuelezea hali halisi hivyo nikaona tukutane sote hapa ili tujuzane sote pamoja na kuweka historia sawa.

Kwenye baraza la vijana la UVCCM mkoa wa Arusha kama sote tulivyo ona kwenye vyombo vya habari maana walitangaza kwenye vyombo vya habari kuwa wamenivua uongozi wa vijana ndani ya UVCCM, japokuwa hadi leo hawajaniandikia barua kuhusu jambo hili, na wakaamua kupeleka kwenye vyombo vya habari taarifa hii kabla hata ya kuniita na kunihoji kama taratibu zilivyo kwenye chama chetu. Jambo hili lingeishia kwenye baraza na uongozi wa Mkoa ukaniandikia barua kimya kimya wala nisingekuwa na haja ya kuja kuzungumza na waandishi wa habari huku ukizingatia kuwa hawana mamlaka hayo ya kunivua uongozi .


Kabla ya kikao hicho cha baraza la Arusha nilipata taarifa mbalimbali kuwa kuna kikundi cha watu kinafanya vikao ili kuhakikisha kuwa ninavuliwa uongozi kutokana na yaliyo andikwa kwenye magazeti kuwa "
Kashfa za Richmond na Dowans zimechangia sana kukipotezea mvuto chama chetu cha Mapinduzi na inaonekana tija kwa wahusika kuwajibishwa kama sehemu ya kujivua gamba kwa chama chetu". Mimi niliwajibu kuwa kama wanachosema ni kweli chochote watakachopewa wachukue kwa kuwa Mungu ameamua kunifanya daraja la wao kurudishiwa kodi zao.

Pia nataka kuwakumbusha kitu kimoja kuwa agenda za hali ya kisiasa na tathmini ya uchaguzi zilisha fanyika kwa ngazi ya Jumuiya na chama mikoani na wala hapakuwa na malalamiko yoyote kuhusu mimi. Agenda hizi pia zilijadiliwa kwenye baraza la vijana la CCM Taifa hivi karibuni ambapo pamoja na mambo mengine lilipitia taarifa zote za tathmini kutoka mikoani huku Mkoa wa Arusha ukiwa ni miongono mwao. Chakushangaza kwenye tamko lao baraza la uvccm mkoa wa Arusha wakairudia agenda ya hali ya kisiasa na tathmini ya uchaguzi ili hali tayari taarifa yao ilishapelekwa kwenye vikao vya juu bila mimi kulalamikiwa chochote.
Hii ni ishara tosha kuwa ilikuwa ni njama maalum.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari na nakala ya tamko la uvccm mkoa wa Arusha kumesemwa kuwa wametangaza kunisimamisha uongozi kwa kuwa sikumpigia kura na nimemsema vibaya Dada yangu mpendwa Batrida Burhani. Kwa mtu yeyote mwenye akili timamu anajua kuwa kura ni siri na ni haki ya mtu ya kikatiba, hakuna mtu yeyote mwenye mamlaka ya kuhoji namna mtu anavyo tumia haki yake ya kupiga kura. Hili ni wazo dhaifu na halina tija kwa wao walio litoa na hasa kwa vijana wa Tanzania ambao wana changamoto nyingi kama vile ajira na matatizo ya bodi ya mikopo. Kwa mtazamo wangu binafsi kama wanafanya kazi hii kwa kutumwa na mtu yeyote basi wajue kuwa kazi wanayo mfanyia mtu huyo ni sawa na kupiga rangi upepo.

Watanzania wa leo ni watanzania wa Dot com na si wa BBC (Born before computer), kwa kuwa wana uwezo wa kupata taarifa mapema. Tamko la baraza la vijana mkoa wa Arusha lilitumwa kwa waandishi wa habari kabla hata ya kikao cha baraza kuisha. Ushahidi ninao wa kutosha, ikiwa ni pamoja na maoni ya baadhi ya wajumbe wa baraza wakiwataja watu walio husika na mpango huo. Miongoni mwao ni mjumbe mmoja wa baraza la mkoa kuwakilisha vijana kwenye mkutano mkuu wa CCM Taifa ambaye ana mtoto anae soma chuo kikuu huku bado akijiita kuwa na umri wa ujana kwa maana ya chini ya miaka 30 kwa taratibu za jumuia yetu.

Nimesikitishwa sana na tamko la baraza la vijana mkoa wa Arusha kulifanya tamko la vijana wa mkoa wa pwani kama sehemu ya azimio lao. Hawana uwezo wowote wa kikanuni wa kuujadili mkoa wa pwani na ukizingatia kuwa baraza kuu la vijana la UVCCM Taifa lilokutana karibuni halikutoa tamko lolote kuhusiana na tamko la vijana wa mkoa wa pwani.


Hofu yangu kubwa ni kuwa nini kinawafanya vijana wenzangu hawa watumie muda wao kujadili matamko ya mikoa mingine badala ya kushughulika na changamoto za vijana wenzetu kuanzia kwenye ngazi ya mashina hadi kwenye ngazi ya mkoa wetu.


Tunahitaji tafakuri ya kina sana kama vijana ili tuweze kufanya mambo kwa maslahi ya chama chetu cha mapinduzi na nchi yetu kwa ujumla.


Ahsanteni sana kwa kunisikiliza.

mrisho-gambo.jpg



MWISHO
 
Thanx, tujuze mkuu... But al n al bora atangaze kuhama tu... Atue cdm tupge kazi
 
Yule Kada wa CCM kupitia UVCCM aliyeanzisha sakata la akina EL na RA ataongea na wandishi wa habari kesho saa nne asubuhi, hapa Dar es Salaam.

Ukumbi tutapeana nyetishana baadae.

Namtakia heri kijana huyu mzalendo alieamua kujitoa mhanga kuelezea namna mafisadi wanavyoiharibu nchi hii.
sema yote uyajuayo na wananchi tupo nyuma yako.
Muda wa mafisadi kutuyumbisha umeisha.
 
thanx, tujuze mkuu... But al n al bora atangaze kuhama tu... Atue cdm tupge kazi
Hivi kwani mtu hawezi kuwa mpambanaji mpaka atoke ndani ya ccm? Mi sikubaliani na wote wanaotaka wanaopambana na ufisadi watoke ccm kwanza.

Wako wapi kina Mpendazoe, Mrema nk? Wote wamechemsha baada ya kuhama CCM.

Mpambano ni lazima uwe ndani ya chama ili kuwang'oa wezi wa nchi hii. Nashauri wapiganaji wote wasihame CCM ila wawe makini na michezo michafu inayofanyika ndani ya CCM.

"msiwaachie nguruwe wale shambani peke yao"
 
mrisho-gambo-mvua.jpg

mrisho-gambo-anaendelea.jpg

Mvua inayoendelea Jijini Dar imesababisha alowane na kahamia kwenye hema kama anavyoonekana pichani
 
Hivi kwani mtu hawezi kuwa mpambanaji mpaka atoke ndani ya ccm? Mi sikubaliani na wote wanaotaka wanaopambana na ufisadi watoke ccm kwanza.

Wako wapi kina Mpendazoe, Mrema nk? Wote wamechemsha baada ya kuhama CCM.

Mpambano ni lazima uwe ndani ya chama ili kuwang'oa wezi wa nchi hii. Nashauri wapiganaji wote wasihame CCM ila wawe makini na michezo michafu inayofanyika ndani ya CCM.

"msiwaachie nguruwe wale shambani peke yao"
Post yako nimeikubali mkuu.

Siku zote mie naamini hivo kuwa zengwe lianzishiwe mlemle ndani ya CCM na wanamageuzi wakamate madaraka ndani ya chama, lakini viongozi wa upinzani hawawezi kulikubali hilo kwani nao wamejimega kule kutaka kusaka madaraka, sasa ukileta point hii unawakera sana japo ni ukweli wa kuleta maendeleo ya kitaifa zaidi.
 
nakuunga mkono mkuu, vyama vya siasa vyote vya siasa vikiwa safi i,e uwajibikaji 100% maendeleo ya kweli yatapatikana
 
Kinachokera wanakwaruzana na kutukanana hovyo lakini bado wako humohumo ndani ya dubwasha lao lililooza. Vijana kama hawa hawakutakiwa kuwa humo.

Inakera na kuudhi.
 
Tuko nyuma yako kaka......sema yote yali ndani yako bila woga Watanzania ni watu wenye akili zao watachuja mbivu na mbichi.......!! Hii ndio Tanzania zaidi Uijuavyo Tujaze Mrisho!!
 
Nape Nnauye yuko wapi jamani?
kapewa pipi anamung'unya?
toka huko yasije kukupata ya kukupata!
Huwezi ukaona jahazi linazama wee uling'ang'anie eti wewe ni mpambanaji!
Toka tena toka mwanangu ccm ni mfumo usiwe mnafiki!
 
Kijana umejipanga vizuri saaana, sema yaliyo moyoni mwako na yale unayoona yamekiukwa. Waliokuvua madaraka ni vibaraka wa mafisadi, wanafanya hivyo bila kujua au kwa makusudi. Hawajui kuwa watanzania wamechoshwa na kufanywa wajinga na kudhulumiwa mali zao a watu wachache wenye tamaa ya mali na madaraka.

Pasua jipu, sie wote wapenda maendeleo ya nchi hii tupo nyuma yako. Usimuache hata mmoja, mtaje kwa jina, nafasi yake na upumbavu anaoufanya. Usiogope vitisho, tunajua njama wanazokufanyia ili ufukuzwe kazi, wamekufuata Chuoni, ulifanya maamuzi mazuri na ya kufaa.

Nataka kuona viongozi wa juu wa UVCCM watasema nini baada ya press conference yako. Na kama watakaa kimya bila kukupongeza au kutambua ujinga uliofanywa na viongozi wenzio wa Mkoa, na kama watakaa kimya bila kuwawajibisha basi hatutakuwa na jingine la kufanya zaidi ya kuwatoa ktk nafasi zao.
 
Hivi wakati haya yanatokea Benno Malisa alikuwa wapi? Au nae kishawekwa ktk kapu la mafisadi?

Nasema Benno kwa sababu hakuna asiyejua kuwa Shigela ni kibaraka wa mafisadi na yupo pale kulinda maslahi zao. Siku zenu zinahesabiwa, hakuna kupona ktk hili la kuiangamiza nchi. Hivi ni nani asiyejua kuwa suala la Richmond na Dowans, EPA na Kagoda, Deep Green na Meremeta ndio vilivyoipunguzia CCM kura ktk uchaguzi uliopita?

CCM sio ya watu wachache kama wengi wanavyofikiria, hiki ni chama cha wananchi. Wale wote wanaotuhumiwa na Ufisadi walioko ndani ya CCM waondoke kabla hawajaondolewa na nguvu ya Umma.
 
Nape Nnauye yuko wapi jamani?
kapewa pipi anamung'unya?
toka huko yasije kukupata ya kukupata!
Huwezi ukaona jahazi linazama wee uling'ang'anie eti wewe ni mpambanaji!
Toka tena toka mwanangu ccm ni mfumo usiwe mnafiki!

Ngoja kijana amwage radhi kwanza. Utasikia moto wake baada ya hapo. Vijana wamechoka na ubabaishaji huu. Utamsikia tu Nape, na wengine wengi saaana sasa watajitokeza hadharani.
 
Kama kweli UVCCM wanakitakia mema Chama chao na nchi kwa ujumla, basi wajitokeze na kutamka hadharani kuwa hawakubaliani na Ufisadi. Baada ya hapo wawataje Mafisadi hao kwa majina na nafasi zao ktk Chama, na kuwataka waondoke ktk Chama ili watu wafanye kazi za kujenga nchi badala ya kutumia muda mwingi kuchekea "upumbavu" ndani ya Chama.

Tualitaka hili lifanyike pia kwa CCM wenyewe. Kwanini munaoneana haya wakati munaangamia? Munategemea nini? Yaani Chama na nchi viangamie kwa sababu ya watu wachache saaana? Nani kasema maneno hayo? Wakati wa mageuzi ndani ya CCM ni sasa.
 
Back
Top Bottom