basi leo asubuhi nimemuona
mrembo mzuri masikini hata
hawezi kugombania gari, nikaona
hapa hapa ndio pa kuchukua ujiko!
Nikapanda fasta nikawahi siti ya
watu wawili halafu nikakaa katikati
ili akija nimpishe,
dah! Si likatokea libabu moja
limevaa miwani kubwaa kama ya
kukatia vitunguu likaa! Duh linanuka
tu sigara,
Yule Mrembo akasimama, limoyo
likauma kweli!,
Daladala ilipofika Makumbusho
nikaona lile Babu linashuka, aisee
kama zali na Mrembo akakaa!
Jaman Bahati iliyoje,nikalianzisha,
MIMI : Mambo Mrembo.
MREMBO : poa,
MIMI : Karibu Karanga (nikatoa
viujugu vya kuzugia)
MREMBO : silagi huo Uchafu,labda
Pop Corn na Clips.
MIMI : Ok naitwa Chogomundu
Pangalashaba, mwenzangu?
MREMBO : He he heee! Jina kama
dawa!, mi naitwa Princess Rihanna!,
Wakati naendelea kupata majibu
Machungu ghafla Nikaona Gari
imefika Namanga, kwa kweli kama
huyu mrembo angekuwa anatoa
majibu ya kuridhisha ningeenda
kushuka nae popote
nikamwambia konda "Shusha
Namanga" ,
sasa wakati nashuka nikashangaa
kumbe na yeye anashuka hapo
hapo!
MIMI : haa kumbe na wewe
unashuka hapa?
YEYE : so what?
MIMI : ok umekataa karanga zangu,
basi twende hapo kwa Mama ntilie
tukagonge chai,andazi maharage,
YEYE : khaa! Unikome, mimi huwa
natumia vitu kama Burger,Kuku,
sausages,Pizza, Egg Chops na Chipsi
Mayai, yaani Uzuri Wangu woote
unilishe kwa Mama ntilie? KOMA!,
Dah Mrembo akasepa zake, nikaona
hakuna Noma nikaagiza zangu
Maharage ya 200,maandazi mawili
200 na Chai ya 100, nikaacha kajero
hapo nikasepa,
Nimefika Kwa Shangazi akafurahi
kweli kuniona.
SHANGAZI : mwanangu
Chogomundu Karibu Baba!,
MIMI: asante Shangazi
SHANGAZI: yule mwanangu wa
Mwisho unamkumbuka?
MIMI : Si yule Kipandauso?
SHANGAZI: huyo huyo!
MIMI : namjua vizuri,wakati
anakuwa namuona,hata nepi
nimembadili teh!, yupo wapi siku
hizi?
SHANGAZI : amekuwa mkubwa
kweli, anasoma Hapo Chuo Cha
Kodi TRA pale karibu na ITV, ila
yupo alienda Chuo akahisi homa
kaona arudi,ngoja nimuite,
Kipandausooooo!!!
KIPANDAUSO : beeee Mama!
SHANGAZI : Njoo mwanangu,kuna
Mgeni!
Hamad! Ndipo Macho yangu
yakakutana na Yule Mrembo wa
Kwenye daladala, kavaa vitenge vya
zamani vya Shangazi, hana Wigi
tena,muda huu komwe la ukoo
linaonekana, komwe la babu yetu!,
mrembo kashika sahani ya Maboga
na kikombe cha uji wa Mchele!,
Aliponiona Almanusura azimie!!!,
huyu ndiye Kipandauso, Mtoto wa
Mwisho wa Mjomba Dindoyogo!,
ukipenda Muite Kipandauso
Dindoyogo!
SHANGAZI : Njoo na Maboga ya
kutosha na kikombe kingine cha uji
uje unywe na Kaka yako!
Dah! akarudi ndani kinoma noma
kainamisha sura chini, mi nikawa
najiuliza wapi Pizza? Wapi Burger?
Wapi Sausage?,
anyway bado nipo hapa kwa
Shangazi mpaka baadae.