Abdallahking
JF-Expert Member
- Mar 19, 2018
- 3,985
- 10,843
Simulizi : MREMBO ALIYEPOTEA
Mwandishi : ANDREW CARLOS
Imeletwa kwenu na: BURE SERIES
Sehemu ya 1
Umati wa waumini wa dini ya kikristo ulikuwa unaendelea kumiminika katika kanisa kubwa la Mtakatifu John. Shangwe kubwa ziliendelea kusambaa ndani ya kanisa hilo ikiwa ni msisitizo kwamba waumini wake wameguswa sana na mahubiri yaliokuwa yakiendelea ndani ya kanisa ambayo yalikuwa yakitolewa na mchungji Joseph.
Mmoja wa waumini katika kanisa hilo alikuwa ni Majaliwa na mkewe Juliana. Japokuwa alikuwa ni fundi mabomba na kila siku alitakiwa awe anafanya kazi hata kama ni jumapili, lakini kwake Majaliwa haikuwa hivyo kutokana na kuheshimu sana siku ya jumapili kwani aliitenga kama siku muhimu kwake na yakutubu dhambi zake zote. Upole na ucheshi aliokuwa nao Majaliwa ulizidi kumuongezea marafiki kila kukicha ikiwa ni kanisani mpaka mtaani alipokuwa akiishi.
Tatizo kubwa lililokuwa likimuandama Majaliwa ni juu ya mtoto. Pamoja na umri wake kufika miaka thelathini na tano lakini bado alikuwa hajabahatika kupata hata mtoto. Alihangaika yeye na mke wake kwenda karibu kila hospitali kujaribu kuangalia pengine mmoja wapo anamatatizo lakini karibu kila hospitali waliyoenda jibu lilikuwa ni hilo hilo kuwa wanauwezo wa kupata mtoto ila kinachotakiwa ni subira na kuomba sana kwa mwenyezi Mungu.
Ndani ya miezi takribani mitatu tayari mke wa majaliwa alikuwa ameshanasa mimba. Furaha ya ajabu ilimtawala Majaliwa na mkewe Juliana nakuamini kile kilio alichokuwa akikililia kila siku sasa kimepata ufumbuzi. Hakutaka hata kumwacha mke wake abaki nyumbani peke yake mpaka atakapojifungua. Kutokana na kuwa na kipata kidogo alichokuwa akikiingiza kupitia kazi yake ya ufundi mabomba hakikutaosha hata kutafuta msichana wa kazi japokuwa pia ilikuwa ni tatizo kubwa kwake kwanza sehemu aliyokuwa amepanga ni ya chumba kimoja. Majaliwa aliendelea kuwa bega kwa bega mkewe mpaka alipofikisha miezi tisa ambayo mke wa Majaliwa alizidiwa na uchungu wa mara kwa mara.
“..Mume wangu..?? sijiskii vizuri nakuomba nisidie kunyanyuka hapa!!”
Aliongea mke wa Majaliwa huku uchungu ukizidi kumzidia hali iliyomfanya majaliwa atafute usafiri na kumkimbiza hospitali haraka. Woga uliochanganyana na kutetemeka mara kwa mara huku akijihisi kama mkojo unamtiririka kupitia suruali aliyokuwa amevaa Majaliwa.
Muda wote alishikilia mikono yake kwa nguvu nje ya hospitali huku kila muda akionesha ishara kama ngumi juu kwa kusali na kuomba mkewe ajifungue salama hapo hospitali. Jasho jembamba liliendelea kumteremka Majaliwa kupitia kwenye kola ya shati lake huku dhahiri likionesha vifungo kupishana sababu ya haraka aliokuwa nayo ya kumuwaisha mkewe hospitali.
Kila mlango wa wodini ulipofunguliwa Majaliwa alikuwa akitetemeka nakuona kama analetewa majibu juu ya maendeleo ya mkewe huko ndani. Hatimaye ndani ya muda mchache akatoka daktari aliyevaliwa mavazi makubwa meupe huku mikononi mwake akilishikilia karatasi na kalamu,
“..Wewe ndio Majaliwa..?”
“ndio mimi dokta.. dokta..?”
Majaliwa aliitikia kwa kutetemeka huku akiendelea kumtolea macho yule dokta.