figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,492
- 54,895
Dodoma. Mwenyekiti wa chama cha TLP, Augustine Mrema ameviponda vyama vya siasa vilivyokutana Zanzibar kwa madai ya kujadili muswada wa sheria namba 5 wa vyama vya siasa na kudai mkutano huo ni wa kiuanaharakati zaidi kuliko siasa.
Mrema ametoa kauli hiyo leo Ijumaa wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na muswada wa sheria ya vyama vya siasa unaoungwa mkono na vyama visivyo na uwakilishi bungeni.
Amedai vyama hivyo vilivyokutana Zanzibar vinapokea fedha nyingi kutoka nje ya nchi na ndiyo maana vinapinga muswada huo ambao utavibana vyama vya siasa nchini kuhusiana na fedha pamoja na matumizi yake wanazopokea kutoka nje ya nchi.
"Kwa hiyo moja ya jambo ambalo naliona ni lazima lifanyiwe kazi na linalopigiwa kelele sana ni hizi hela zinazoingia katika nchi kwenye vyama, hujui amechanga nani na anamchangia nani afanye nazo nini."
"Ila ukihoji utaambiwa ni demokrasia, sasa ukiruhusu kila mtu aingize hela zisizojulikana zisizofanyiwa mahesabu, hazikaguliwi ukisema zikaguliwe au zidhibitiwe wale wajanja hawataki," amesema
Mrema ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Parole amesema wanasiasa wenye uzoefu na nchi kama yeye hawawezi kukubali fedha chafu zisizo na mahesabu ziingie katika nchi kwa kisingizio cha demokrasia na hivyo watasikia kelele nyingi sana kwamba Serikali ni ya kidikteta kutokana na sheria zinazoitwa kandamizi.
Aidha ameiomba Serikali kutoa ruzuku kwa vyama visivyo na uwakilishi ili visije vikaingia tamaa na kupokea fedha kutoka nje ya nchi zenye lengo la kuvunja amani ya nchi.
Chanzo: Mwananchi